Nilipata ulemavu sababu ya Mapenzi

hongera ndugu yangu kwa ajira na pole kwa tatizo la masikio, najua jinsi unavyoumia na unayopitia, yani tatizo la masikio ndo limefanya hata nje nisitake kutoka mtu anakwambia hujambo unasema salama inaumiza sana, mazungumzo unapata kwa asilimia 40 tu hizo nyingine unabaki kusema ndio hivyo au kucheka inaumiza sana,

nandio kikwazo kikubwa kwangu kuanza kujiajiri nawaza nitahudumiaje wateja wa hizo nguo au ndio nitaulizwa hii bei gani nitasema salama tena Mungu anihurumie tu.
 
mimi kama SALIMU nachukua fursa hii kukuomba samahani sana, na kiuhalisia NAIMA alinifata mwenyewe, halikua lengo langu kumtafuna,.

pole sana mkuu, yule dada ni mkatili sana.


MZUSHI FLANI was here.
 
mkuu, pole sana. . unaweza kua na mtu wa kukusaidia pembeni kama mdogo wako ambae hana ishu mtaani saivi itasaidia sana.. mimi pia nina tatizo la masikio, nmekosa michongo mingi sana ila nna imani bado mapambano yanaendelea..
 
Hayanaga ushauri hayo hadi yamfike mtu ya kumfika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu, pole sana. . unaweza kua na mtu wa kukusaidia pembeni kama mdogo wako ambae hana ishu mtaani saivi itasaidia sana.. mimi pia nina tatizo la masikio, nmekosa michongo mingi sana ila nna imani bado mapambano yanaendelea..
asante iwa ushauri mkuu, Mungu aendelee kutupigania tupige hatua
 
Kama hii stori yako ni ya kweli basi ulimwengu ni katili sana kwa baadhi ya watu.
ndugu yangu bado sijafikia hatua ya kuilaumu dunia mimi naamini maamuzi yangu ndio chanzo cha haya yote
 
dada yangu najitahidi kuwa na moyo wa kusamehe ila hali yangu ya ulemavu na majuto yananiumiza na kunitesa mimi siwezi sahau na kusamehe nimejitahidi nimeshindwa
Hili ndilo kosa lako kubwa mkuu, ukisamehe utapata uponyaji wa roho na amani. Msamehe kabisa, ondoa kinyongo, mwambie Mungu naomba uanze maisha mapya na mimi. Utapata amani moyoni na maisha mapya yatasonga mbele bila ya kumuwaza Naima.

Pole sana mkuu
 
Kaka polee sanaa Sema nini mi nikifanyiwa hivyo naenda kigoma Kule kwa Yule mganga aliyempa mtu mimba ya Kuku yan mtu anarogwa Heavy .... Wache wacheze na Akili zetu
 
Ukiandika usisaha 'kuni-tag' mkuu.

Mtoa mada pole sana.
 
Pole sana mtangulize Mungu kila jaribu lina mlango wake wa kutokea.
 
Pole sana mtoa mada.
Matendo ya wanawake kama haya huwa yanawachukiza sana wanaume na wengine wanashindwa kuvumilia na kujikuta wanafanya mauaji na gunia la mkaa kuhusika.

Kuna haja ya kuzijua tabia za wanawake na kujifunza namna nzuri ya kuweza kuishi nao. Mfano, Kwa kubadilisha mitazamo yetu kwamba unaamini kuwa mpenzi ni mtulivu na hawezi kuwa na mahusiano na mtu mwingine. Pia tuache kujitoa kimwili na kiroho kwa wapenzi wetu, tuishi nao kwa staili ya kuwachukulia poa. Ukibaini haendani na itikadi zako achana nae kistaarabu kisha endelea na mishe zingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…