Niliona/nauona udhaifu mkubwa kwenye mifuko ya Serikali na namna yao ya kuwafikia walengwa

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Kwanza nikiri nilikuwa naifahamu mifuko michache ya Serikali, ambayo pia walengwa wengi hawakuwa wakiifahamu. Jana nimemsikia Rais akisema mifuko ipo 18. Aisee ni mingi na ingekwenda sawa basi tungeona tija ya kila mfuko.

Awali niliwahi kumuuliza Afisa Vijana wa Morogoro kuwa wanatumia njia gani kuhakikisha vijana wanakuwa na ufahamu na mikopo wanayotoa, jibu lake halikujibu swali nililokuwa nimeuliza.

Lakini ni suala la wazi kuwa watu mtaani wana ufahamu na mifuko binafsi kama Finca, Pride, nk huku mifuko ya serikali ikiwa inafahamika kwa wanaofanya kazi ndani ya mifuko husika pekee.

Kuifanya mikopo hii iwe na tija, mfano ile ya halmashauri, ni heri itolewe 9% ya mapato ya halmashauri ili 1% itumike kuitangaza ili walengwa waifhamu na kuitumia ili kujikwamua kiuchumi. Na mifuko mingine iangalie namna ya kujitangaza ili walengwa wanufaike.

Ni suala zuri kuwa na mifuko inayosaidia makundi mbalimbali nchini, lakini haina maana kama mifuko husika itabaki na majina tu huku kiutendaji ikiwa haifahamiki.

TAKUKURU kwa miaka mitano iliyopita wamekuwa wakikamata watu wengi wanaotoa mikopo umiza, hata kwa watumishi wa serikali kama walimu nk. Hii inaonesha hata hao watendaji hawana ufahamu na mifuko hiyo ambayo pengine ingewasaidia kwa namna moja au nyingine kwenye kujikwamua kiuchumi.

Kwa kweli nimestuka na kushangaa sana kuona tuna mifuko 18, huku wananchi wakiendelea kulia na mikopo umiza au kulipa riba kubwa kwenye baadhi ya mikopo kwenye makampuni binafsi.

Katika research niliyowahi kuifanya, kimsingi niligundua hii model ya mikopo tunayotumia ilianza kuisha muda wake mwaka 2,000 na tangu hapo ikaanza kuwa mwiba kwa wanaoitumia, najua ni model hiyo hiyo inayotumika na makampuni mengine ya mikopo lakini kuna haja ya kubadili model.

Lakini ktk tafiti niliyoifanya niligundua kuwa mifuko ya serikali inakosa convinience na kuna hassle nyingi sana kiasi ambacho wengi huona hawawezi kuhangaika nayo, kwa kufahamu pande zote mbili vizuri naona haja ya wachumi walioko halmashauri kutafiti vizuri kuhusu umasikini wa watu na kuja na model ambayo inaweza kufanya kazi vizuri.

Nahitimisha kwa kusema
Mifuko ya serikali inahitaji marketing kubwa ili kuwafikia walengwa.
Model ya mikopo husika inapaswa kubadilika ili kuwa na convinience kwenye utoaji mikopo husika.
 
Mkuu niseme tu umeniwahi, ila nashukuru kwa bandiko hili. nilitaka kuleta mjadala humu jamvini juu ya mifuko hii na hili lilichagizwa na hiyo hiyo hotuba ya rais ulioitaja. Kimsingi imetajwa kuwepo mifuko mingi ya uwezeshaji wananchi ilio chini ya ofisi ya waziri mkuu. tukiachana na asilimia 10 ya halmashauri ambayo kwa kiasi chake wamejitahidi kuitangaza,hii mingine je, ni kwa kiasi gani walengwa wana ufahamu wa mifuko hii? Kwanini kilio cha mitaji bado ni kikubwa mno miongoni mwa makundi mbalimbali ya kijamii ilhali mifuko hii ipo? Ni wakati sasa mamlaka zinazohusika na mifuko hii zijitokeze kuitangaza mifuko hii ikalete tija hasa kutatua tatizo kubwa la mtaji.
 
  • Thanks
Reactions: OLS

Naamini, Serikali itaongeza kuifanyia marketing ili makundi lengwa yasiendelee kulalamika mitaji au kuibiwa kwenye mikopo umiza ambayo TAKUKURU ndio wameanza kuistukia hivi sasa
 
Umeongea pointi ya msingi ila kama hujui hata pride ni mfuko wa serikali uliochukuliwa na wajanja, kama serikali inataka kufanya vizuri ni heri mifuko hii ikapunguzwa na kubaki michache lakini ikawa na tija kwani mingi imebaki kwa ajili ya kuweka connection kwa wachache
 
Back
Top Bottom