Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 359,869
- 828,403
Hii sio hadithi bali ni simulizi yangu iliyobeba uhalisia wa yale niliyopitia nikiwa JF.. Mimi ni introvert.. Hivyo si mwepesi sana kusimulia maisha binafsi kama walivyo extrovert
Nilijifunza mambo ya kiroho pamoja na uchawi darasani na nje ya darasa na kutunukiwa madaraja niliyostahili kwa niliyojifunza.. Mimi ni mbobezi kwenye hiyo sekta.. Kwakuwa pamoja na kujifunza lakini baadhi ya mengi niliyafanya kwa vitendo.. Na machache kati yake yaliniacha na majuto. Kwakuwa kuna uumbaji niliutesa kutokana na hasira za kibinadamu. Mimi si mkamilifu
Nilijiunga JF na kukaa karibia miaka miwili bila kuandika habari zozote za kiroho ama ushirikina.. Nilikuwa naogopa nitafikiriwaje Halafu usiku mmoja nikapata ujasiri wa ghafla nikaandika mada kuhusiana na nywele..
Nilikuwa na utaratibu wa kufanya meditation saa nane usiku kisha baada ya hapo naandika! Ni kama vile kuna sauti ilikuwa inafanya narration cha kuandika siku hiyo.. Ama ni kaka nilikuwa naletewa mada akilini kisha nainakili
Mwitikio ukawa mkubwa sana.. Taratibu nikaanza kufanya ushirikina bila kutarajia.. Lakini nikawa na mgongano mkubwa kiroho kwenye maslahi ya Mungu na shetani
Nolijitahidi sana kuzipanga hizi falme mbili.. Lakini mara zote ufalme wa Mungu ulishinda.. Hata hivyo shetani naye hakukubali kirahisi kushindwa
Maisha ya ushirikina huku nikiwa namwamini Mungu na kusali sana yakanikutanisha na roho za ajabu hasa.. Tena hapa hapa JF.. Kuna wenzetu humu wamebebeshwa maroho ya ajabu mno.. (Hili linahitaji simulizi yake separate maana nilikutana na vitu vikubwa na vya kutisha sana) Kama sio kumshika Mungu leo wala nisingekuwa hapa
Nikaanza kukutana na changamoto na kupata upinzani mkali sana nje na ndani ya JF. JF ina maroho mabaya yaliyojivika maumbo ya watu.. Usiku ukiyatandika yanakuja kukutolea hasira JF kukicha!😀 ndio maana nilikuwa sijibishani nao.. Kwakuwa nilikuwa najua kinachoendelea..
Siku moja mwaka juzi nikiwa nimechoshwa na mapambano ya kiroho.. Nikachukua likizo nikasafiri mbali.. Nikatafuta location yenye ukimya na kuongea na Mungu wangu
Nilifanya hivyo kwa siku sita mfululizo bila majibu..lakini usiku ule wa kuingia siku ya saba. Nikaangaziwa kiroho na kupokea uponyaji na majibu niliyohitaji.🤔🙏🏿😔 ❗ Shetani akakubali kuyaaga mashindano japo kwa mbinde sana!!!
Nikajihisi nimetua mzigo mzito sana! Nikafanya toba nikapata wepesi wa mwili na roho.. Nikaokoka nikiwa penye yangu chumbani usiku...
Binadamu nilikuwa pekeyangu (nafsi na roho), Mungu alikuwepo Kama pumzi hai ya milele.. Shetani mshindwa pia alikuwepo
Tangu hapo nilianza maisha mapya na wiki moja baadae niliweka post hapa kutangaza rasmi kuachana na ushirikina na kuuza kilinge, mkoba na zana zake zote!
Wokovu ni jambo la kiimani na la kibinafsi sana.. Halina maelezo yanayoeleweka kwa wasio okoka.. Kwasasa naishi maisha ya amani ya afya yangu kimwili na kiroho vimeimarika sana!
Pamoja na wokovu nilio nao lakini sina ukamilifu wa kimungu hivyo naishi kwa maombi na toba kila wakati
Huyu ndiye mimi wa sasa... Na kule kwa neema kuu na ya Kimungu sitarudi tena🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿