Nilimwambia atakufa akafa kweli

Nilimwambia atakufa akafa kweli

Mdomo huumba. Hata mi nikimnenea mtu mabaya yanaweza tokea kama Yale au nusu ya Yale not kifo tho. Mpaka naogopa kuongea kitu kibaya kama mtu akinikwaza. Mfano
Nakumbuka sekondari niliibiwa daftari kipindi cha mitihani,nikawa nalalamika sana mmoja ananikejeli "ulikuwa unaandika kwa machine kwamba una Lilia mwandiko mzuri au unalilia counter book ya buku jero" yaliniuma Yale maneno nikamwambia sasa wewe ndio utalilia begi lako la mia mbili...A week ahead toka ile Siku alikuta locker limevunjwa na kaibiwa madaftari yote mpaka begi lake,I was the first suspect...kilichoniokoa kuna mwanafunzi alimuona mwizi...
 
Imepita miaka mitano sasa lakini bado nakumbuka hili tukio
Ilikuwa ni mchana mmoja siku ya ijumaa nilikwenda bar ya Igongwe pale Mwenge karibu na vinyago kupata lunch
Kufika pale nikahudumiwa na binti mgeni hata wa kuhudumia, ndani ya nususaa alikuwa keshaniambia historia yake yote lakini wakati huohuo akiwa keshagonga safari 3,
Nilibaki pale mpaka saa kumi muda aliosema anatoka huku nikiwa nimeshamaliza mzinga wa konyagi... Alikuwa kanihoji na mimi kama ni mwenyeji mitaa ile nikamdanganya nikamwambia mimi mgeni
Baada ya hapo tukaondoka kuelekea Cafe la Tino si mbali sana kutoka pale
Cha ajabu na cha kushangaza kufika pale akajifanya amelewa na mimi ni mpenzi wake.. Mbele za rafiki zangu akawapa cheo cha mashemeji
Kugundua hili nikaamua kumtelekeza kiaina.... Lakini loh kufika tu kwenye gari huyo naye kafika
Nikamkatalia kupanda lakini timbwili alilofanya pale aliishia polisi mabatini
Pale Cafe la Tino alidai ana mimba yangu halafu najifanya kumtoroka, hiyo mimba atalea na nani? Duu .... Siku hiyo nilikuwa nimeingia cha shoga wallah
Kwa hasira nikamwambia kama kweli una mimba yangu mimi nitakufa ila kama hata kama unasema uongo na hatufahamiani kabisa basi utakufa!
Alikaa mahabusu Ijumaa ile mpaka jumatatu nilipoenda kufuta kesi... Alifariki ijumaa ya wiki ile aliyotoka selo! Alilala getho la Igogwe akiwa mzima.. The next day jumamosi ilikuwa zamu yake kufanya usafi, wenzake walipojaribu kumuamsha alikuwa wa juzi ..... Nilipata habari kwa meneja na nikatoa mchango wangu
 
Huko angani leo hakufai kabisa, wachawi saba wanenusurika kifo baada ya kupita mkondo mrefu mitaa ya Msata bila kutoa taarifa... Nimelishuhudia live hili tukio
 
Ww utakuwa mchawi Ila hujijui mheshimiwa, nenda kwa bulldozer wakashughulikie
 
Back
Top Bottom