Nilimuamini nikaenda kwake akataka kunibaka

kiss ov love

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2025
Posts
9,363
Reaction score
16,092
Kuna kijana alikuja kupata huduma ofisini kwetu akawa amechukua namba yangu yeye ana ofisi yake huko town anauza viatu vya kike.

Mwanzoni alikuwa mpole tukawa tunawasiliana vizuri tu, kwa vile ana ofisi yake nikajua atanipa ushauri mzuri wa biashara na kujiajiri hivyo nikawa nimemuamini, na kumchukulia kama kaka au rafiki wa kiume.

Ikatokea siku akanialika kwake nikitoka kazini, kwakuwa siyo mbali na ofisini kwetu nilivyotoka nikaenda, tukakaa tukapiga story tukala chakula, baada ya hapo nashangaa mtu mara anisogelee atake kunishika, akaninyanyua kanipeleka chumbani weee hapa nilibadilika nikawa mbogo, maana mimi sikujia hayo mambo iweje atake kunibaka bila ridhaa yangu kisa nimekuja kwake ndiyo aone kuwa nimekubali kila kitu.

Tulivutana sana hiyo siku nakumbuka, mimi hadi nimefura kwa hasira ndiyo kumlazimisha akanipeleka home maana ana usafiri wake, tangu hiyo siku nimetoka sijapokea simu yake wala kujibu meseji zake, nimemuona ni mwanaume wa hovyo sana tangu lini mapenzi yakalazimishwa? Mwache mwanamke akupe kwa kuridhia mwenyewe.
 
Pole sana, mtu asiye Kaka yako wa damu kwenda nyumbani kwake mmm hata siwezi kabisa, wanaume wakati mwingine akili huwa inahama kabisa, sasa wewe na mkia wako mkae wawili dhubutu yake!
 
Kuna kijana alikuja kupata huduma ofisini kwetu akawa amechukua namba yangu yeye ana ofisi yake huko town anauza viatu vya kike.

Mwanzoni alikuwa mpole tukawa tunawasiliana vizuri tu, kwa vile ana ofisi yake nikajua atanipa ushauri mzuri wa biashara na kujiajiri hivyo nikawa nimemuamini, na kumchukulia kama kaka au rafiki wa kiume.

Ikatokea siku akanialika kwake nikitoka kazini, kwakuwa siyo mbali na ofisini kwetu nilivyotoka nikaenda, tukakaa tukapiga story tukala chakula, baada ya hapo nashangaa mtu mara anisogelee atake kunishika, akaninyanyua kanipeleka chumbani weee hapa nilibadilika nikawa mbogo, maana mimi sikujia hayo mambo iweje atake kunibaka bila ridhaa yangu kisa nimekuja kwake ndiyo aone kuwa nimekubali kila kitu.

Tulivutana sana hiyo siku nakumbuka, mimi hadi nimefura kwa hasira ndiyo kumlazimisha akanipeleka home maana ana usafiri wake, tangu hiyo siku nimetoka sijapokea simu yake wala kujibu meseji zake, nimemuona ni mwanaume wa hovyo sana tangu lini mapenzi yakalazimishwa? Mwache mwanamke akupe kwa kuridhia mwenyewe.
kwamba unaenda kwenye chumba cha mwanaume na hujui anachohitaji? hukwendea hili? tangu lini mwanaume akawa rafiki wa mwanamke? never. pia, hivi unafikiri unaongea na watoto? kwamba tuamini ulitoka bure na akakupeleka kwa gari yake hadi kwenu. acha uzinzi, ni dhambi, itakugarimu, mpokee Yesu na uache dhambi au la ujinga wako hauna mwisho mwema.
 
Pole sana, mtu asiye Kaka yako wa damu kwenda nyumbani kwake mmm hata siwezi kabisa, wanaume wakati mwingine akili huwa inahama kama kabisa, sasa wewe na mkia wako mkae wawili dhubutu yake!
Mimi nimeshangaa sana huyu kijana kwanza anaonekana ana mademu kibao nikajua mimi atanichukulia kama mdogo wake tu loh! Kumbe alikuwa ananipigia mahesabu nikimaliza kula kitimoto anile na mimi
 
Lakini na nyie mnazingua! Eti nilimuona kama kaka yangu au rafiki wa kiume ... nilienda anipe ushauri wa jinsi ya kujiajiri.... Mweeeh! Hakuna kitu kama hicho. Nyote mlizingua! Na yeye angekuandaa na kuchukulia fursa kutega nyavu akunase kimasihara! Ona sasa, kamwaga mboga, wewe ugali! Mmekosa nyote!😝
 
Pokea simu yake huenda iyo siku upwiru ulimkabia kwa juu .

Umeenda ghetto umekula na connection ya maokoto unataka for free ? Seriously! ungempa muungwana hata Ahadi ya chochote kitu .
 
Lakini na nyie mnazingua! Eti nilimuona kama kaka yangu au rafiki wa kiume ... nilienda anipe ushauri wa jinsi ya kujiajiri.... Mweeeh! Hakuna kitu kama hicho. Nyote mlizingua! Na yeye angekuandaa na kuchukulia fursa kutega nyavu akunase kimasihara! Ona sasa, kamwaga mboga, wewe ugali! Mmekosa nyote!😝
Mimi sijapoteza kitu maana sijawahi kuwa na hisia naye kabisa
 
Back
Top Bottom