Nilimfumania, sasa ananitishia kuniua

Nilimfumania, sasa ananitishia kuniua

Jamani huyo mwanaume wako si mzima inawezekana kati ya wale wanne yeye ndio mmoja wapo.Haiingii akilini mtu ufumaniwe halafu wewe tena utake kuua.
Ila na wamama sisi tuna tabia mbaya sana sasa huyo mama mwenye nyumba anabariki kabisa mwanae kubanduliwa humo humo ndani ilihali anajua mkaka ana mchumba mbali na hilo yeye ndio anakuwa mlinzi wao aiseeee kweli ni shidaaa
Tabia za pwani ni jambo la kawaida...tanga to mtwara mwambao wote wa pwani hasa wale wenyeji kwao ni kawaida sana
 
Komaaa na maamuzi yako Liwalo na liwe, mrembo kama wee lazima uheshimiwe. Akafie mbele msaliti mkubwa
 
Vitu vidogo vidogo kama hivi huwa vinavuruga sana wadada.

Sijui kwa nini.
Mkuu nitakujibu
Mwanamke ni kiumbe mvumilivu sana kwenye maswala mengi lakini mapenzi uvumilivu ulimshinda mwanamke. Roho ya huruma ni chanzo
 
Amefanya jambo la maana kabisa,maana nyie wanawake sio wakuonea huruma.Hata ndugu yangu wakike akifanyiwa hayo sawa tu,maana wanawake mkiaminiwa hamuaminiki.Mkipendwa hampendeki.

Huyo jamaa awe mstarabu tu asije kufungwa.
 
Kweli jamaaa amekosea alipaswa kumsingizia shetani kutokana na kile kilichotokea na kuaahidi kiachana na binti wa mama (ikiwa hiyo ndio nia yake). Hivi ni kweli mlipendana au ulikuwa ukimpenda? Haiwezekani kutoka kuwa lembebez mpaka mambo ya polisi na kuuana kwasababu tu kafumwa...kweli kuna ukaraibu sana kati ya love and hate.
 
Hapo lzm hata mama mwenye nyumba nae anatumiwa ndo maana maana akahalalisha na bintie ili baba asije pewa taarifa na mwanae
 
Kuna watu ukiachana nao katika mahusiano wanakuwaga kama wehu.
Yaani mtu umemuacha kwa amani ila utajuta mana anakukosesha raha.
Na ukishaona mtu yupo hivo na aliondoka kwa mbwembwe jua alipoenda yamemshinda hivo anataka kukurudia.
Chamsingi simama imara huyo hamaanishi anakutisha tu ili uogope umrudie ila ukikomaa ataona humpapatikii hivo atakuacha.
Asante feitty kwa ushauri wako binafsi simpendi tena wala sina mpango nae ,sina dhiki ya wanaume
 
Mkuu nitakujibu
Mwanamke ni kiumbe mvumilivu sana kwenye maswala mengi lakini mapenzi uvumilivu ulimshinda mwanamke. Roho ya huruma ni chanzo
Umesema kweli pakawa
 
Bora mimi nilifumaniwa nikasingizia nimelogwa, nikapelekwa kwenye maombi kabisa
Hahahaha,! Unatisha lkn kwangu mm kitendo cha kukufumania tu inatosha haijalishi umelogwa au umebakwa!
 
Amefanya jambo la maana kabisa,maana nyie wanawake sio wakuonea huruma.Hata ndugu yangu wakike akifanyiwa hayo sawa tu,maana wanawake mkiaminiwa hamuaminiki.Mkipendwa hampendeki.

Huyo jamaa awe mstarabu tu asije kufungwa.
Unaongea kama wewe ndiye muhusika vile
 
Huna kosa

Lakini ungewaacha wadumishe ujirani mwema jamani
 
Pole na shughuli za siku wakuu.

Nilikuwa na mchumba ambaye tumedumu nae kwa miezi tisa. Pia uchumba wetu ulishakuwa wazi kwa wazazi wa pande zote mbili, japo bado hakikuwa kimefanyika chochote katika kuhalalisha mahusiano yetu.

Mwezi uliopita nilikwenda nyumbani kwa mchumba wangu bila kumtaarifu, nilikuta mlango umerudishiwa tu, nikataka kuingia mama mwenye nyumba akanifanyia ishara ya kuniita kwa mkono nikaenda kumsikiliza.

Alichoniambia eti nirudi nyumbani nisiingie kwani mpenzi wangu hajisikii vizuri na ameagiza mtu yoyote akija asiingie. Nikatafakari nikaona kama mtu hajisikii vizuri kwanini nisijue shida yake.

Nikamuitia yule mama na kumshukuru kwa taarifa lakini nikaingia ndani, kweli sebuleni hapakuwa na mtu.

Nikasukuma mlango wa chumbani na kuingia. Sikuamini macho yangu nilichokiona inauma sana nilimkuta mpenzi wangu akifanya mapenzi na binti wa mama mwenye nyumba wake.

Niliona hakuna haja ya kugombana kwakuwa hakuwa mume wangu nilichomwambia aendelee na huyo mimi basi tena.

Siku iliyofuata alikuja home alipogonga geti nilichungulia nilipotambua kuwa ni yeye nilimuuliza anasemaje.

Alinijibu kwa dharau kwamba amekuja kunipa taarifa kuwa yule niliyemkuta nae ndiye chaguo lake mimi sina hadhi ya kuwa nae sikuwa na maneno mengi nilimjibu kifupi asante kisha nikafunga geti nakurudi ndani.

Nilipata uchungu sana nililia hata kesho yake sikuweza kwenda kazini
Nikaamua kumtoa moyoni na kwakweli nilimtoa kabisa, nilichukua zawadi zote alizonipa nikamtuma mdada wa kazi ampelekee. Nikajua ndo mwisho wa mawasiliano.

Baada ya wiki kupita akajirudisha nimekataa na simtaki sasa anatishia kuniua nimeripoti polisi na nimepewa RB.

Je, hapo mimi nina makosa?

!!.........Wanawake wa Dar ni noma,sisi huku kwetu Tarime mwanamke kwenda polisi ni mwiko kabisa!
 
Back
Top Bottom