Jinsi unavyotumika kulipa visasi vya mkeo

Stanley Mims

Member
Aug 29, 2020
47
86
1 Pet 3:7 SUV

Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.

........................................................................

Jumatano moja ya mwisho wa Mwaka 2023, yaani mwezi Disemba, saa 7:38 Asubuhi nilipokea simu kwa Mwanamume mmoja aliyejitambulisha kama James (Jina si halisi); aliniuliza kama namjua Agnes (Jina si halisi), nikamuuliza

"Agnes nani?" Niliuliza jina la pili ili kujua, ni yupi anamzungumzia kati ya Agnes ninao wajua. Nikamjibu "NDIO"

Akaniuliza tena mimi ni nani yake.

Kutoka hapo nikatambua tu kuna kitu hakipo sawa, Ila, ni Kaliba yangu kupokea taarifa za mitindo yote bila kutanguliza jazba.

Akaniambia yeye ni Mume wake; na akaanza kunipandishia sauti kuhusu mimi kuwasiliana na mke wake kwamba angenifanya chochote kile bila kumzuia na nikae mbali sana na mkewe; na kama namtaka yeye hana muda wa kumbembeleza Mwanamke, aende akadai talaka aje niishi nae, ila kama sivyo nimkome sana.

Ikabidi nishushe pumzi, nafsi yangu ikajaribu kuvaa kiatu chake, nilishindwa kwa kweli, nikaona ana kila sababu ya kuongea vile. Ila, nikajisemea moyoni "Amefanikiwa"; hapa sikumaanisha huyu ninayezungumza nae kwenye simu, bali Agnes.

Kisa kilianza hivi.

Niliwahi kuwa kwenye mahusiano na huyu dada; miaka kadhaa ya nyuma, mpaka mwaka tuliomaliza chuo; nilimuacha, ni Mwanamke aliyeharakia maisha, alikuwa na hulka ya kulazimisha ndoa kwa maneno kwa upande wangu, ilifika mpaka wakati tunakwazana. Sikuwa na amani kwa wakati fulani, kwa sababu ndoa niliitaka, sidhani kama kuna Mwanamume kwenye dunia hii awe mjinga kiasi cha kutomuoa Mwanamke kama Aggy, ila purukushani zake zilinitia mashaka; mbaya zaidi kuna kisa kilitokea kikafanya tusiwe wapenzi tena.

Kutoka pale mwenzangu alikuwa na kinyongo na mimi, na kwa sababu ya upendo wake kwangu, kuna namna yoyote alifanya kupata Mawasiliano yangu.

Mwanzoni mwa Mwaka 2021, alinipigia kwa namba fulani ambayo ilikuwa ngeni kwangu, ni wakati ambao hata mimi ndio nilikuwa naanza kujitafuta kimaisha.

"Unaishi wapi siku hizi?" Aliniuliza, na zaidi akapenda kuniona; Unajua nini?

Wanawake walioachika (Kimahusiano) wana tabia ya kujua hali za maendeleo kimaisha za Ma Ex wao, lengo afahamu kama alikuwa akililia kufanya maisha na mtu ambaye angemfikisha sehemu fulani..........

Kwa bahati mbaya ama nzuri, niliitikia wito wake; nikafungua moyo, "Karibu, chukua magari ya Mbezi......." nikamuelekeza, na baada ya nusu saa akafika.

.................................................................................

Alifika kwangu; ila mimi sikuwa nakaa kinyonge kwa sababu tangu tuachane, sikuwahi kumuamini tena, ilikuwa kila muda nakaa kuangalia response yake kwa habari nilizompa, yeye alikuwa cheerful (Samahani kama ulikimbia umande).

Tukapiga story, na kucheki movie (sikupasha of course); baadae nikaenda kuoga.

Wakati ambao mimi naoga, yeye kumbe aliingia kwenye simu yangu ya button, akacheki mesej, akakuta Mwanamke ambaye mimi nilikuwa nachat nae; akachukua namba yake.

Badae nikamsindikiza stendi, akapanda gari na kusepa, ilipofika Miezi kadhaa badae, kumbe alinivutia muda wote huo ifike siku ya birthday yangu ani "suprise" na kweli alifanya hivyo, aka screenshot DP ya mpenzi wangu, kisha akanitumia kwa WhatsApp; for sure nilim mind sana, tuligombana kwa sababu ya ile Incident, ila kama kawaida yangu, siku panic sana; uzuri ni kuwa, hakuwahi kumtafuta, na kuna namna nilimpanga mpenzi wangu akabadili ile namba, na sasa ana nyingine.

Kutoka hapo hatukuwahi kuwasiliana tena; Aggy ameolewa Mwaka jana, baada ya kuolewa akanitafuta tena; sikumpokea vibaya, ila safari hii sikumpokea kama ex wangu kama ilivyo awali, nilimpokea kama mtu nayepaswa kuwa naye makini, nilijua kama ameolewa...... kama kawaida, aliniuliza kuhusu kazi yangu na mahala napoishi, bila hiyana nikamwambia, japo si kiufasaha.

Mimi ni Mwandishi wa Matangazo (Copies) lakini naandika na nyaraka nyingine kama CVs n.k. akaniomba nimuandikie CV na Resume kama alivotaka, anataka kuhama kituo cha kazi, nikaona hakuna baya, nikamwabia anitumie taarifa zake (japo nazijua)

Baada ya kazi, nikamtumia Lipa Namba, lakini hakuwahi kulipa; sikuitazama hii kama shida bali fursa, nilimtajia kiwango ambacho nilijua hawezi kunilipa, lengo ni yeye asinitafute kwa sabaabu nilikuwa namkumbushia deni, and this time hatukuwa na mawassiliano ya mara kwa mara.

Sasa basi, sijui kama wewe ni muumini wa Coincidence ila kuna siku nilikuwa naelekea sokoni, kubeba vikorokoro, huku si kule nilipokuwa naishi mwanzo, ni pengine.

Ghafla bin vu!! Nikamuona anapita kwenye boda, anaelekea upande wa Bar Maarufu ya Mbuzi Online (Utajua mwenyewe ya Wapi); of course tukashangaana sana, akanifanyia ishara ya kuwa atanicheki kupitia simu, nikamwambia poa

Mi nikaendelea na mizunguko yangu, nikabeba vitu kumpelekea babyto alifika ilu apike pike badae nirudi kupiga msosi, nikaenda kukaa kijiweni ghafla meseji ya Aggy inaingia...

NTAENDELEA....
 
We jamaaa unataka kusema tutakuja kukutana na haya mmbo maana kama uhusika inanihusu ivi japo makasumba bado sio mengi
 
SEHEMU YA PILI (2)

...............................................................................

"Naelekea kwenye kikao, kumbe ndio unakaa huku? Naomba nikuone nikitoka" Text Iliingia.

Nikasoma kwa ku smile, kiukweli sio mtu ninayemchukia, naomba kuthibitisha kuwa, Aggy ni moja kati ya Wanawake walionifunza na kunijenga mimi kama Mwanamume, nilijuta sana kumuacha, ila nilikuwa tayari kulipa gharama zote ambazo ningekutana nazo kwa kumuacha, so mwaka 2020 nilikaa mwaka mzima bila kuwa kwenye mahusiano. Kupata Mwanamke mithili yake haikuwa kazi rahisi kabisa, kwa sababu mimi kihaiba sio malaya.

.....Nikaisoma ile meseji kwa kutabasamu sana, sikuwa na wasi nikamjibu "Yes, nakaa huku; unaenda kwenye kikao cha nini?" Nikauliza

"Kuna harusi, nina tenda ya kupamba so tunapanga bajeti na kupanga kamati, nimestuka sana kukuona ila nikitoka please Stan, naomba nikuone" akanisihi.

Mimi nikakubali, basi nikamlia timing baby wangu wakati anakaangiza vitu huko, nikamzuga kama natoka mara moja; nikaenda kukaa kijiweni namsikilizia Aggy, nikaagiza na kahawa kabisa chupa nzima, baada ya kama lisaa hivi, simu yake ikaingia.....

"Nipo hapa kwenye hizi bar, hii inaitwa Mbuzi Online, nakuona wapi?" Akaniuliza.

"Nyoosha na hiko kibarabara moja kwa moja, mi nipo mbele huku, tutakutana tu" Nikamjibu.

Kama dakika tatu hivi nikamtia machoni, tukasalimiana na baada ya hapo tukaenda kukaa mahala pana mgahawa mdogo hivi; tukaagiza vinywaji basi story zikaanza hapa na pale......

Katika story zote tulizopiga, stori hizi mbili zinaonekana kumtonesha moyo wake na kumuumiza.

Kwanza; inaonesha hana mapenzi na Mwanamume aliyemuoa. Ngoja nikwambie kitu; nina uhakika 100% Kwamba Aggy aliolewa kwa msukumo wa dada zake ambao wote wameolewa, ni yeye tu alibakia............ingawa mimi nilimwambia kwamba nina furaha kuona amepata hitaji la moyo wake, nikaona uso wake umekasirika na badae kuwa wa huzuni, mbele ya macho yangu Aggy alianza kububujikwa na machozi, nilijisikia vibaya sana.

"Sikuwa na mpango nae, na tuliachana tayari ni yeye ndiye alikuja home pale kulialia tukarudiana" aliniambia hivyo kuhusu mume wake.

Mimi nikajua tu hapa; jamaa anampenda sana mwanamke ambaye kwa msukumo wa maisha ya hulka za kuolewa, amekubali kuwa nae. Ila sio kwa mapenzi.

Jambo lingine linalomsikitisha; sionyeshi interest ya kutaka hata mawasiliano naye. Na hapa aliniomba kitu.

"Naomba nikapajue kwako" aliniomba

"Kwangu huwezi kufika, pili; kuna mtu, mamaa yupo so siwezi kukupeleka" nikamjibu. "Na nakuhakikishia, hata kama asingekuwapo usingekuja, wewe umeolewa sasa hivi, na sio dada yangu, naheshimu ndoa na mume wako; so be humble" niliendelea.

Nilimtaka ajue ni namna gani naheshimu ndoa yake, in short naiogopa ndoa yake. Kingine ni kwamba, huyu Mwanamke namjua kuliko hata mumewe anavyomjua, hata akilia hapa na kusaga meno, sitampa imani ya 100%.......labda 40% kwa sababu, ni mtu ambaye ana tabia ya kulipa kisasi kwa kupanga, na kutumia huruma.....tangu nikiwa nae kwenye mahusiano alikuwa hivyo, ingawa niwe tu mkweli; hakuwahi kunifanyia hivyo, na nilipiga marufuku hiyo tabia japo ni silka, yaani haiba ya kuzaliwa nayo.

Ni Mwanamke mpole, na anajulikana hivyo, so anatumia hiyo advantage hata kwenye mambo yake binafsi, ndio mana huwa nakaa nae kitaalamu sana.

Hatukumaliza hata vinywaji.........Tukaondoka!nilimpeleka stendi akapanda gari.

............................................................................

BAADA TA WIKI.

"Nimekuja tena kwenye kikao, naweza kukuona?" Ujumbe uliingia, na wakati huu mimi nikiwa Mbezi, sikuwa nyumbani; nikamwambia kwamba ningerudi badae kidogo na sio muda huo, so kama angechelewa kwenye kikao chake angeniona.

Bwana kumbe hilo sio tatizo kwa Mwanamke akupendaye, ni kweli sikuwahi kurudi ila aliningoja mpaka niliporudi ghetto, nikaingia kupiga maji kidogo, nika change kisha pale pale tulipokutana tukakutana tena, this time ilikuwa muda umeenda kidogo; nikamuuliza kulikoni mbona muda kama umeenda halafu bado yupo pale, akasema hamna shida, akatoa simu akapiga home, nahisi ni dada wa nyumbani yule akapokea akamuuliza kama watoto wameoga na kula......

Hapa niweke jambo sawa; Huu ulikuwa ni wakti wa likizo, so alikuja kutembelewa na watoto wa nduguze, yeye wa kwake akiwa mmoja tu.

Basi akahakikishiwa kwamba kila kitu kipo sawa; tukapanda kwenye bar moja hivi tukakaa pale; mwenzangu akaagiza grand malt, mimi nikaagiza Castle Lager tukaanza mdogo mdogo, nikamsikia anamwambia mhudumu kwamba aniletee bucket nzima, nikagoma, nikamwambia aachane nayo asilete nitaagiza taratibu.

Naomba ujue ni Mwanamke wa aina gani nimekaa nae hapa, so kila move anayofanya inapaswa niwe mbele yake kabla hajafika. Nikamwambia "Mimi ni mnywaji tu, ila sio mlevi" na hata hivo kiutani nikamwambia "sina siri za kukwambia" moyoni najua nachomaanisha, na asikwambie mtu, yule dada alikuwa hata tayari aje kwangu na angeweza kulala angelala. NAMJUA!

Ghafla simu ya mumewe inaingia, anamuuliza yupo wapi akamjibu yupo "kwenye kikao, ndio namalizia" mimi namsikiliza tu, moyoni najisemea na mimi nitadanganywa hivi. Nikameza mate tu.

Nilipoenda chooni, mwenzangu akaniagizia tena nyingine, narudi nakuta mzigo umejaa pale. Nilichofanya nikamuita muhudumu, nikamwambia apunguze mbili, aniachie mbili. Niliijua nia ya Aggy, sikutaka kwenda kichwa kichwa. Tulipiga story pale nyingine zilikuwa za ajabu sana; ila nyie ndoa zina siri hizi, kulewa nilewe mimi lakini pumba anaongea yeye...

Alichokuja kusema pale nikapigwa na bumbuazi na pombe zote zikaniishia kichwani, nikamnyanyua huku machozi yakimlenga na mimi nikiwa na jazba "Amka fasta tuondoke, ushaanza Use***"

NITAWAAMBIA.......
 
1 Pet 3:7 SUV

Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.

........................................................................

Jumatano moja ya mwisho wa Mwaka 2023, yaani mwezi Disemba, saa 7:38 Asubuhi nilipokea simu kwa Mwanamume mmoja aliyejitambulisha kama James (Jina si halisi); aliniuliza kama namjua Agnes (Jina si halisi), nikamuuliza

"Agnes nani?" Niliuliza jina la pili ili kujua, ni yupi anamzungumzia kati ya Agnes ninao wajua. Nikamjibu "NDIO"

Akaniuliza tena mimi ni nani yake.

Kutoka hapo nikatambua tu kuna kitu hakipo sawa, Ila, ni Kaliba yangu kupokea taarifa za mitindo yote bila kutanguliza jazba.

Akaniambia yeye ni Mume wake; na akaanza kunipandishia sauti kuhusu mimi kuwasiliana na mke wake kwamba angenifanya chochote kile bila kumzuia na nikae mbali sana na mkewe; na kama namtaka yeye hana muda wa kumbembeleza Mwanamke, aende akadai talaka aje niishi nae, ila kama sivyo nimkome sana.

Ikabidi nishushe pumzi, nafsi yangu ikajaribu kuvaa kiatu chake, nilishindwa kwa kweli, nikaona ana kila sababu ya kuongea vile. Ila, nikajisemea moyoni "Amefanikiwa"; hapa sikumaanisha huyu ninayezungumza nae kwenye simu, bali Agnes.

Kisa kilianza hivi.

Niliwahi kuwa kwenye mahusiano na huyu dada; miaka kadhaa ya nyuma, mpaka mwaka tuliomaliza chuo; nilimuacha, ni Mwanamke aliyeharakia maisha, alikuwa na hulka ya kulazimisha ndoa kwa maneno kwa upande wangu, ilifika mpaka wakati tunakwazana. Sikuwa na amani kwa wakati fulani, kwa sababu ndoa niliitaka, sidhani kama kuna Mwanamume kwenye dunia hii awe mjinga kiasi cha kutomuoa Mwanamke kama Aggy, ila purukushani zake zilinitia mashaka; mbaya zaidi kuna kisa kilitokea kikafanya tusiwe wapenzi tena.

Kutoka pale mwenzangu alikuwa na kinyongo na mimi, na kwa sababu ya upendo wake kwangu, kuna namna yoyote alifanya kupata Mawasiliano yangu.

Mwanzoni mwa Mwaka 2021, alinipigia kwa namba fulani ambayo ilikuwa ngeni kwangu, ni wakati ambao hata mimi ndio nilikuwa naanza kujitafuta kimaisha.

"Unaishi wapi siku hizi?" Aliniuliza, na zaidi akapenda kuniona; Unajua nini?

Wanawake walioachika (Kimahusiano) wana tabia ya kujua hali za maendeleo kimaisha za Ma Ex wao, lengo afahamu kama alikuwa akililia kufanya maisha na mtu ambaye angemfikisha sehemu fulani..........

Kwa bahati mbaya ama nzuri, niliitikia wito wake; nikafungua moyo, "Karibu, chukua magari ya Mbezi......." nikamuelekeza, na baada ya nusu saa akafika.

.................................................................................

Alifika kwangu; ila mimi sikuwa nakaa kinyonge kwa sababu tangu tuachane, sikuwahi kumuamini tena, ilikuwa kila muda nakaa kuangalia response yake kwa habari nilizompa, yeye alikuwa cheerful (Samahani kama ulikimbia umande).

Tukapiga story, na kucheki movie (sikupasha of course); baadae nikaenda kuoga.

Wakati ambao mimi naoga, yeye kumbe aliingia kwenye simu yangu ya button, akacheki mesej, akakuta Mwanamke ambaye mimi nilikuwa nachat nae; akachukua namba yake.

Badae nikamsindikiza stendi, akapanda gari na kusepa, ilipofika Miezi kadhaa badae, kumbe alinivutia muda wote huo ifike siku ya birthday yangu ani "suprise" na kweli alifanya hivyo, aka screenshot DP ya mpenzi wangu, kisha akanitumia kwa WhatsApp; for sure nilim mind sana, tuligombana kwa sababu ya ile Incident, ila kama kawaida yangu, siku panic sana; uzuri ni kuwa, hakuwahi kumtafuta, na kuna namna nilimpanga mpenzi wangu akabadili ile namba, na sasa ana nyingine.

Kutoka hapo hatukuwahi kuwasiliana tena; Aggy ameolewa Mwaka jana, baada ya kuolewa akanitafuta tena; sikumpokea vibaya, ila safari hii sikumpokea kama ex wangu kama ilivyo awali, nilimpokea kama mtu nayepaswa kuwa naye makini, nilijua kama ameolewa...... kama kawaida, aliniuliza kuhusu kazi yangu na mahala napoishi, bila hiyana nikamwambia, japo si kiufasaha.

Mimi ni Mwandishi wa Matangazo (Copies) lakini naandika na nyaraka nyingine kama CVs n.k. akaniomba nimuandikie CV na Resume kama alivotaka, anataka kuhama kituo cha kazi, nikaona hakuna baya, nikamwabia anitumie taarifa zake (japo nazijua)

Baada ya kazi, nikamtumia Lipa Namba, lakini hakuwahi kulipa; sikuitazama hii kama shida bali fursa, nilimtajia kiwango ambacho nilijua hawezi kunilipa, lengo ni yeye asinitafute kwa sabaabu nilikuwa namkumbushia deni, and this time hatukuwa na mawassiliano ya mara kwa mara.

Sasa basi, sijui kama wewe ni muumini wa Coincidence ila kuna siku nilikuwa naelekea sokoni, kubeba vikorokoro, huku si kule nilipokuwa naishi mwanzo, ni pengine.

Ghafla bin vu!! Nikamuona anapita kwenye boda, anaelekea upande wa Bar Maarufu ya Mbuzi Online (Utajua mwenyewe ya Wapi); of course tukashangaana sana, akanifanyia ishara ya kuwa atanicheki kupitia simu, nikamwambia poa

Mi nikaendelea na mizunguko yangu, nikabeba vitu kumpelekea babyto alifika ilu apike pike badae nirudi kupiga msosi, nikaenda kukaa kijiweni ghafla meseji ya Aggy inaingia...

NTAENDELEA....
Upuuzi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom