Nilikuwa siamini mapenzi yanauma, leo nimeamini

Nilikuwa siamini mapenzi yanauma, leo nimeamini

Katika maisha yangu, nimewahi penda kwa dhati mara moja tu, mitihani ya maisha na mikosi kwa miaka 3 ikaniandama, kwa kiasi fulani Kuna sehemu ilibidi nitumie uongo kuweka mambo sawa. Leo umenigharimu.

Tarehe 01/01/2023 nilikabwa nikaibiwa viatu, pesa na simu ndogo.

Tarehe 02/01/2023 napoteza vyeti vyangu vyote vya taaluma.

Tarehe 03/01/2023 napigiwa simu kuitwa nimepata kazi (faraja inarejea).

Tarehe 05/01/2023 anakuja ndugu yangu japo sio wa damu yeye ndiye aliyenisomesha anaomba nimkope laki 3 sikua na hiyo hela wakati huo anaomba nimpeleke hata kwa mtu nimchukulie dhamana ,kwakua namuamini tunaenda kwamtu namuwekea dhamana anapewa laki 3 kwa ahadi alipe tarehe 09 siku zimekata hapatikani na amehama nyumba na mji bila kusema nalazimika kulipa Deni.

Tarehe 14/01/2023 Mpenzi ameniblock.

Tarehe 16/01/2023 Naanza kazi kwa Mara ya kwanza Ila napokea ujumbe kua mimi na yeye basi na hataki kuniona na kuanzia siku yangu vibaya.

NAKIRI WAZI NIMEACHWA NA MWANAMKE WA NDOTO ZANGU NIMEACHWA NA MPENZI WANGU WA KWANZA(MWANAMKE NINAYEMPENDA) KWA UZEMBE WANGU MWENYEWE.

Sina wa kumlaumu, presha ilishuka nikajisikia kufa kufa (vibaya hakuna maelezo) nimewekewa drip 2 now angalau nimekaa sawa nimepewa ruhusa ya kwenda nyumbani.

NAJUA UNA AKAUNTI YAKO HUMU, NAJUA UTASOMA HUU UJUMBE KWA NAMNA YOYOTE NIMEUMIZA MOYO WAKO NIMEKUANGUSHA ULINIAMINI ILA SIJATIMIZA WAJIBU WANGU NAOMBA UNISAMEHE "MASAI" WEWE NI MWANAMKE WA THAMANI SANA NAJUA PENGINE HAITAWEZEKANA HATA CHEMBE KURUDI KWANGU ILA NAOMBA TUSIWE MAADUI NIPO KWENYE TRAUMA NAUMIA.
Mkuu shusha pcha yake, bila ya hivyo uzi hauna maana
 
Kaka umepata kazi halafu unalia lia ungekuwa huna kazi si ungejiua piga kazi kaka tunza wazazi wako kama wapo.
 
Kwa sasa kijana ndio umekomaa, hautayumbishwa na mahaba tena, nadhani ulikuwa na utoto bado ila kwa hiyo ngeo ya penzi uliyopata utakuwa umekomaa sasa.

Karibu kiumeni bwana mdogo
 
Mkuu pole sana, naelewa sana situation unayopitia,

Mimi jana nimemcheki mwenzake, jibu alilonipa limenifanya nikose furaha na amani kabisa... kwamba siku zote nilikuwa nampotezea muda kwamba alidai nimuoe ikiwa mimi kuna malengo bado nilikuwa sijayakamilisha mwenzangu akaamua kutafuta mwanaume mwingine,... sasa hivi tunavyoongea hapa ana mimba yake.

Kiukweli nimeumia sana ukizingatia nilikuwa nampenda sana, sana, sana, tena sana... ila ndio hivyo maamuzi yake nayaheshimu sana...inabidi ni move on hakuna namna.
 
Bro sikia!! Huyu masai ndo kifo chako, kama tu umemkosea wewe kakuacha na uko hoi unataka kufa, Je akikutenda yeye kama yeye, you are dead bro!! ACHANA NA HUYU TAFUTA MWANAMKE ANAEKUPENDA SIO UNAEMPENDA
 
Inasemekana ukiumizwa kwenye mapenzi tayari ushakuwa malay** polee bro tayari ushakuwa...,😂
 
Back
Top Bottom