Kwanini Muhindi au Mwarabu hakupi chenji mkononi anakuwekea juu ya meza?
😅😅.. tena nafanya biashara ya risk vby sana nahesabu hela daily . Haijawah punguka hata 100!tena hela zang nazitaftia uswahilini vby mno!
Nimekuelewa vyema..ndo maana inatakiwa kusoma sana elimu kuhusu fedha.. sijisifu lakini mim mkoba wangu hukuti sijui lipstick..yaan ni kalamu na notebook..nanote kila hela ukikaa jioni mtiririko unaonekana..yaan kuwatoa kwenye akili hiyo itahiji ngv mno mnoTatizo biashara za waswahili hazina hesabu, kila akipata shida kidogo hela anachukua kwenye droo baada ya muda anasahau km alichukua hela anaanza kusingizia chuma ulete
Sio kwenye biashara tu, hata maisha ya kila siku. Naweza kutumia hela baadae naanza kujiuliza imepotelea wapi baadae sana ndio nakumbuka nilitumia kwenye nini au wapi.Tatizo biashara za waswahili hazina hesabu, kila akipata shida kidogo hela anachukua kwenye droo baada ya muda anasahau km alichukua hela anaanza kusingizia chuma ulete
[emoji1] [emoji1] [emoji41]"Nikazama mfukoni nikatoa kitita cha elfu 60"
Nimeishia hapo hapo.
Hhaahahaa Eh Mungu okoa hiki kizaz😅IPO chuma ulete nyingine ambayo anakuja mtu anakwambia niazime 10000 mkimpa unasahau na hutakumbuka uliemuazima
Miaka miwili iliyopita Mrs alifungua mgahawa maeneo fulani akishirikiana na rafikiye ,kiukweli biashara ilishamiri kwa kipindi cha miezi kadhaa.
Yalianza kujitokeza mapungufu mara kwa mara kwenye mahesabu,kiufupi hesabu inayofungwa ni ya kununua mahitaji ya kesho na faida kiduchu sana hata elfu tano max😀. Niliwatuhumu wife na mwenzie kwa uzembe nami nikajitwika jukumu la mahesabu kwa takribani wiki moja. Lahaulaaahh hakuna nilichosaidia,daftari langu na pesa iliyopo ni mbingu na ardhi🤣🤣. Biashara ile ilikufa kwa style hiyo kazi kubwa na faida ni kuzungusha mtaji ilihali Kodi ni kubwa.
Bibie baadae waliokua wafanyabiashara jirani na wateja walikuja kuuliza kulikoni kuacha biashara iliyokua na dalili za kufika mbali??Nyie hamjatujua wanawake hata chembe...jaman mwanamke ni zaidi ya umjuavyo...sio wife sio shogake!
Either hela mteja anatoa hailetw kwako mtu anauchuna balaa..akiondoka kila siku na 4000 ni hela kubwa..
Nimeifanya hiyo biashara vzr mnoo..nilipata jiko...ilishamiri balaa biashara ..lahaulaa mume akasema mbona wateja wako wote wanaume ..akaifunga ...sikuwa pata shot hata siku 1 na nilikua napika kila kitu..supu chapat nyama choma(mapande) mishikak, lakinj hesabu ilikua clear...yaan akija mteja anataka msos unaandika haraka kwa daftr...kila kinachotoka andika jion wanaokusanya hela watajizungusha weeee lakini lazima hesabu ikamilike jomba! Hao waliamua kuzungukana ..yaan mm ht niambie huyu hela zake ni chuma ulete namix kwa raha zote na hakuna inayopotoea
Aisee..so ss hv unazuia🤣Bibie baadae waliokua wafanyabiashara jirani na wateja walikuja kuuliza kulikoni kuacha biashara iliyokua na dalili za kufika mbali??
Tulieleza sababu na watu kadhaa walitushangaa na swali kubwa kwani ninyi mlikua mnauza hivi hivi(bila kuzuia hao chuma ulete)??😀😀
Hapana biashara ile ilishajifia,siwezi kumtegemea binadamu mwenzangu kamwe!!Aisee..so ss hv unazuia🤣
Alikuwa anazidisha chenji kwa wateja, au movement ikiwa kubwa anapagawa, na kuzidisha chenji, business ukikosa mtu smart wa kuhandle transaction nyingi at per, lazima upoteze fedha kwa mtindo huo wa kuzidisha chanji walasio chuma ulete....,,, chuma ulete zinatokea mara moja moja sana, sio kila wiki au kila siku, hvyo mkuu uliweka mtu kiazi kwenye goli lako akakufilisi huku ukiwa unaendekeza hurumaKuna dogo nilipata goli la chips, yai, vyuku, mishkaki na wenzie Obay huko nikaona si mbaya nimuweke ajiongeze maana alikua mzigo tu home. Goli lilikua linatema, Nikamuwekea mtaji mzuri tu vyombo, misosi na wasaidizi ye kazi yake adeal na malipo tu. Baada ya kuuza.
Na ilikua mi tukutane once a week niende kujua ngapi kaweka duh🤔.
Mwezi tu dogo kaleta hesabu mara 2.
Haya ukimuuliza ok mzigo ulikua nao wa kilo 3, kwa wiki tupate 5 we unakuja na 2 inakuaje?
Na sawa labda biashara ilikua mbovu viko wapi vitu vyote?
Vimeisha Bro.
Hela? anajibu hata mi sijui
Namboost tena tunanunua mazagazaga yote tunaweka golini.
Mara karibia 4 same shit,
kumbuka kuna kodi hapo inatakiwa ilipwe miezi mi3. na ni hela ndefu.
Ilifika mwisho nikimbananisha anaanza kulia kuomba misamaha mingi.
Nikaona kama namwonea tu.
Ilifika mahali mwenyewe akasema bro labda mi sihitajiki kufanya biashara.
Nilimwonea huruma lakini kumforce aendelee ingekua torture.
Kuna siku niliamka tu nikaenda beba kila kitu
Piga mnada,
Nikamrudisha home tutafute la kufanya.
Ilibidi ila hata mimi iliniuma.
Dogo mwenyewe sio mtu wa mademu wala kilevi.
Ndo naamini chuma ulete inawezekana kabisa walikuwepo pale.
Hiyo 2000+
Hamnaga hicho kitu. Kama hujapoteza basi umechanganya hesabu. Mtu hawezi ondoka na pesa kichawi.
Hivi mtu ukiataka kujua kama umerogwa unajuajeKwanza kabisa niwape pole kwa msiba mzito wa rais wetu Jpm.
Binafsi nimehuzunika sana kumpoteza mtetezi wa wanyonge, mzalendo, mkweli, mchapa Kazi, mbunifu, mcha Mungu, jasiri.
Niende direct kwenye Mada,
Aisee nimekua nashangaa watu nikiwaomba chenji wanapata wasiwasi na kuniuliza, pesa yako haina miguu??
Wengine wamekua wakinyima chenji kabisa mpaka unakasirika na kuwaona wana roho mbaya.!
Ipo hivii, kuna eneo la stend nikiwa nimetulia nasubiri wateja waje, akaja dogo amempakia abiria kwenye boda.
Walisimama Karibu yangu na kuomba chenji ya elfu 10 nikasema ninayo ila ni elfu tano tano, dereva boda akasema hiyo hiyo.
Nikazama mfukoni nikatoa kitita cha elfu 60. Elfu 10, kumi zilikua 3 nyingine zilikua elfu tano tano tu.
Nikatoa elfu tano mbili nikampa ile elfu 10 yake nikaikunja na zile nyingine, kwa hiyo elfu kumi kumi nikawa nazo 4.
Hee, baada ya muda kidogo kupita nikaenda mpesa nimtumie mtu elfu 20.
Kuchomoa kitita changu nakuta elfu kumi aliyonipa siioni, niliikariri maana zangu zilikua mpya nahisi second au first hand kabisa kutoka zitengenezwe ila ile ten yake ilionesha imetumika zaidi.
Nilijisachi mpaka kwenye soksi nikavua viatu lkn wapi.
Nilishangaa sana, ile narudi nikamcheki aliposhuka yule jamaa, akawa hayupo na wakati hakuna bus limepita na abiria wengine walikuwa wamekaa kwenye banda la kungojea usafiri.
Nikaja kuconnect na jinsi walivyofika pale nikaamini walikuwa kitu kimoja maana walipofika walikuwa wanaongea kwa sauti ya chini kabla ya kunifuata, sikuwafikiria sana mi nikawa busy tu na smart yangu nafuatilia matukio ya msiba wa taifa.
Wanaonyima chenji nimeamini hawajipendei, imewapasa kufanya hivyo kutokana na mambo ya kihuni kama hivi.
Kama una kisa cha kuibiwa pesa kimazingara kama hivi, tunaomba ushuhuda na jinsi ya kuzuia hawa chuma ulete.!
Wao ni Chuma uleteSababu nyote nyinyi hamna ibada sijamsikia muhindi mwenye duka akilalamika au mwarabu ni wafrika tu ndio wanaibiwa