Wazima jamani!?
Leo nimeona niwashikilishe stori ya kweli iliyowahi kunitokea. Kwanza samahani sana Mimi siyo mtaalam wa kupangilia aya japo nimesoma Communication Skills. Wenye kuamini wataami wale wa kubeza watabeza sana.
Mimi naitwa Umomi, nimezaliwa mwaka 1994 huko wilayani Tarime. Jimbo la Tarime vijijini. Ni mtoto wa 3 ktk tumbo la mama tupo wato 4 kwa mama. Nilipozaliwa niliisha na familia yangu mpaka mwaka 2000 nilipo enda kwa Bibi yangu kizaa mama Kijiji jirani. Kwa Bibi nilikaa kama miaka 3 mpaka mwaka 2003 niliporudi nyumbani ili kuanza shule.
Nilisoma mpaka darasa 3. Kisha ghafula niliacha na kuanza kusaka life japo nilikuwa mdogo sana. Hapo ilikuwa mwaka 2005 mnamo mwezi wa 6. Aisee haya maisha asikwambie mtu, ni magumu sana. Nilitoka kijijini nilienda Tarime mjini nikaa sokoni (soko kuu Tarime) kama siku 3 hivi. Kipindi hicho nilikuwa nasaidia watu kazi ndogo ndogo kama kuchambua Karanga n.k mchana wakawa wananipatia chakula then usiku najijua pamoja na pakulala.
Nakumbuka siku ya 4 alipatika mmama mmoja pale sokoni japo jina lake silikumbuki but mme wake alikuwa anaitwa Fujo, huyo mama aniita mida ya saa 12 jioni na kuanza kunihoji tatizo la kutoondoka pale sokoni make nilikuwa nimeleta gumzo. Mi kwa weledi wangu nilimdanganya vya kutosha Kisha baada ya kengere ya kufunga soko kulia alifunga meza yake tukapitia kituo cha polisi stand ya mabas nikaandikwishwa Kisha tukaenda kwake. Yule mama kweli alinijali sana Kama mwanaye. Ila nilifanya kosa moja la kumwambia kijijini kwetu hivyo alianza kunitafutia watu wa nyumbani.
Baada ya wiki moja alikuja mmama kutoka kijijini kwetu alikuwa na kijana wake ambaye tulikuwa tunasoma darasa moja. Wakaja mpaka home kwa mama. Nikaulizwa hawa watu unawajua nikajibu NDIYO. Wakajieleza pale kuwa natafutwa sana na ndugu zangu bas nikawaelewa ila kichwani nilikuwa nawaza nipate sehemu niajiriwe ili nilipwe hata 1000 kwa mwezi ila nisikae kijijini. Basi baada ya maelezo na stori wakaruhusiwa kuondoka Mimi yule mama alisema haina haja ya kwenda polisi tena kwani angeweza kutoa taarifa hata kwa badaye.
Basi bana tukaanza safari, yule mama alikuwa anakaa karibia na maeneo ya machinjio ya zamani cjui mpaka saivi ipo pale pale? Tulipoondoka nikaanza kuwaza mambo mengi sana. Kwanza nyumbani naenda kupewa kichapo cha mbwa koko, pili sijatimiza lengo la kupata kazi. Basi tukaenda mpaka tukavuka barabara moja ya sirari-Mwanza (kojifa). Kisha tukavuka mto msati. Nikawa nimepata jibu kuwa hapa bora nikimbie tu. Make yule mama asingeweza kunikimbiza kwa wote na mwanaye walikuwa na mizigo. Basi nilitembea haraka na kuwa umbali wa 50m nikaanza kukimbia mdogo mdogo nikielekea kule kambi ya jeshi. Yule mama alilia sana akisema mie natoa wapi mtoto watu jmn! Sikumuonea huruma kabisaa niliendelea na safari yangu mpaka kule mto mori Kisha nikarudi tena town kuzungukia njia ya nkende kule wenyeji wanafahamu.
Basi nikaenda kuyaanza maisha mapyaa mjini nikiwa sina pakulala wala pa kula. Nilipata wazo la kwenda shangazi yangu nikamtapeli sh 5000 kwa kumdanganya kuwa baba kanituma ili akanunue kifaa fulani hivi cha jembe la plau afu baada ya wiki atamrudishi. Shangazi akaingia kingi akanipa hiyo pesa

Nikaamua Sasa kutafuta sehemu niishi kule mjini ili niuze Karanga make tayari mtaji nilikuwa nao. Nikaenda mtaa mmoja hivi upo shule ya sabasaba ila siujui kwa jina nikafikia sijui yule baba alikuwa ni balozi au mwenyekiti hata sikuelewa. Hapa ndipo shida ilipoanzia Sasa. Nikakaribishwa.
Baada ya kukaribishwa nilikabidhiwa chumba, nikaoneshwa choo n.k. usiku tukala vzr nikaenda kulala. Sasa mama alionekana kunipenda baada ya kumpa full story ila baba hakunielewa. Mama akawa ameniambia kuwa nitaishi pale kuanzia ule mwezi wa 7 mpaka mwakani Yani 2006 ndipo anipeleke kusoma na ningeanza darasa la 3 tena. Ila haya maisha hayana huruma kabisaa. Yule baba ambaye ni mwenyekiti Yani baba mwenye nyumba akaanza figisu na mke wake kumbe hakutaka niishi kwake. Baada ya wiki akanipeleka polisi ili nirudishwe kijijini kwetu hiyo no baada ya kutoa maelezo yote kwa yule mama niliumia sana kwani hata pale kituo cha polisi nilichapwa bakora na kupewa onyo kuwa nikionekana town bila kuwa na mzazi wangu nitakamatwa na kufungwa. Basi polisi wakanipandisha magari ya kwenda Kijiji jirani ili nikifika nikabiziwa kwa mwenyekiti Kisha nipelekwe mpaka kijijini kwetu. Nilipanda gari mnamo saa 4 asubuhi na kifika saa 1 jioni kweli safari ilikuwa ngumu sana utazania nilikuwa naenda mikoani. Haya maisha nimeona mengi sana. Baada ya safari ya karibia kutwa nzima nilipelekwa kwa mwenyekiti wa Kijiji jirani nikala Kisha nikalala.
Kesho yake nilipewa uji na viazi vtamu nikapiga Kisha tukaanza safari ya kwenda kwa mwenyekiti wa kijijini kwetu huku nikisindikizwa na vijana 3 wenye nguvu. Inaonekana zile taarifa za kukimbia yule mmama ziliwafikia polisi hivyo wakatoe taarifa kwa yule dereva na dereva akamwambia yule mwenyekiti wa Kijiji jirani. Basi tukafika kijijini kwetu nikaanza kuwapiga kiswahili wale watu kuwa hapa Mimi siwezi kupotea kwani nimefika tayari. Basi kwa vile wote walinogewa na stori wakamua kuniacha niende mwenyewe. Nikasema kichwani ninyi ni machizi sana Yani nawaingiza mkenge kiboya hivyo!? Kisha nikacheka sana nikijua nimeya win maisha kumbe natafuta matatizo.
Basi kwa vile lengo langu lilikuwa ni kusaka ajira ya utotoni ckutaka kwenda home baada ya kuachiwa na wale wenyeviti wa vjiji Yani wa kwetu na Kijiji jirani pamoja na wale vijana 3. Nikaenda tena Kijiji jirani ila kipo ndani ya Koo moja korofi sana pale Tarime. Basi nikafikia mji fulani hivi. Kulikuwa na mbibi mweupe akaanza kunihoji nikajitambulisha but kwa majina bandia hasa la baba. Huku nikisema kuwa Mimi ni mtoto yatima! Basi Kama kawa nikakabidhiwa chumba ila nilikuwa nalala na watoto wa kike 3 make ule mji ulikuwa hauna wavulana mmoja alikuwa ni wakuja Yani mdogo wake na mwanamke ambaye alikuwa kaolewa pale. Nikaishi pale Kama wiki 2. Nikaanza kufundishwa kuchunga ng'ombe dah! Niliwaza sana make na home kulikuwa na hao mifugo Kama 3 na walikuwa wananiliza nikiambiwa kwenda kuwachunga. Nilipoendelea kuishi pale walikuja vijana wa rika langu tukapiga nao stori Kisha wakaniambia kuwa naitwa nyumbani kwao. Nikaenda nikaanza kuhojiwa Kama kawaida huku wakiniogopesha kuwa ule mji ninaoishi siyo salama. Walinishawishi mpaka nikahamia kwao kumbe nia yao ilikuwa niwe nawacgungia wakiwa wapo shuleni watoto wao.
We bana we! Nilikaa takribani mwezi kwa huu mji, huku tukienda kuchunga ng'ombe zao dah! Nilitarajia kulipwa but mambo yakawa ndivyo sivyo. Nilichunga mwezi mzima, mwezi uliofata wakaanza kuniletea dharau huku wakijua Mimi sina wazazi wakati nilikuwa najua Mimi na Mungu wangu pekee. Cku moja nilienda kuchunga asubuhi mida ya 5 hivi tulikuwa wawili Mimi nikasima ukingo wa shamba ili ng'ombe wasiharibu mazao na yeye ukingo mwingine. Yule kijana akaanza kuongea vijembe vya kuniudhi mara ooh! Wewe huna kwenu....