Sipendi Uchawa
JF-Expert Member
- Dec 19, 2016
- 8,089
- 12,811
Barabara ya lami mpaka 2015 kwa tarime ukiachana na ile ya sirari, ile ya tarime mugumu mpaka leo haijawekwa lami zaidi ya kipande kutoka mjini mpaka mogabiri (ilianza kuwekwa mwaka jana.) Kisha kutoka mogabiri unaikuta tena nyamwana nayo ni kipande cha 1 km ambayo imekuja mpaka jirani na barabara ya nyamongo (wanapaita kipimio) kwenye kona. Hiyo lami ya mwaka 2005 wewe umeitoa wapi ukaiweka tarime nzima? Ni kweli 2005 kulikuwa na michomoko, lakini niambie mchomoko gani ulikuwa unaenda kuanzia bwirege kule. Hii njia ya kwa Gachuma kuelekea nyamongo mpaka leo haina usafiri zaidi ya raia kukodi bodaboda au kusubiri basi la jioni la kwenda nyamongo ndipo wapate usafiri.2005 njia zilikuwa Safi kabisa, tena Chambiri alikuwa amelima kujiandaa na uchaguzi, kulikuwa na lami mpaka Sirari, halafu kulikuwa hamna Landover ni michomoko tu, hata ukitembea kwa mguu toka Tarime hadi Nyabirongo, kiongera, matamankwe, au korotambe huwezi kutumia masaa hayo.