Nilijaza fomu ya ajira ila hadi sasa sijaitwa kazini, ajira yangu bado ipo?

Jul 12, 2016
7
2
Habari za asubuhi wadau,
Mimi ni mgeni kabisa humu hata kamba haijatoka. Naombeni kuuliza, mimi nilifanya interview UDOM na kufanikiwa kufaulu sasa January 2016 nikajaza fomu ya ajira. Hadi leo sijaitwa kazini, hivi ajira yangu itakuwa bado ipo kweli?

Nafuatilia sana ila jibu ni cheque number haijaja. Hebu nisaidieni hapo
 
Sio jukwaa lake ila tunaweza jaribu shauri.

UDOM wanafanya interview wenyewe, hawapitii UTUMISHI kwahiyo HR wa hiyo college au kitengo au chief HR ndio hajapeleka taarifa zako Hazina.

Ni form ya ajira au Mkataba uliojaza na kusaini?

Baada ya kufahuru Interview, kiutaratibu ilibidi ukaripoti kituoni hafu ndio uanze kazi. Cheaue Number zitakukuta.
 
Kituoni yaani udom niliripoti nikajaza mkataba na vitu vyote vinavyotakiwa, nikaambiwa sehemu ya kuanza kazi lini nisijaze, wakasema siku hizi huwezi anza kazi kabla cheque number haijaja wanaepusha kuibebesha mzigo serikali
 
Back
Top Bottom