Nilifikiri anatania ....anakuja kweli!

Nilifikiri anatania ....anakuja kweli!

kukimbia sio solution, akizima simu, ipo siku wataweza kutana popote, nafikiri ni kheri kuongea nae kwa simu ili ajue kabisa kama ni kugeuza ageuze, saa 4 (nadhani ni usiku) mume wa mtu kwenda kumpokea mwanamke mwingine ghafla, italeta picha mbaya sana, ukienda kumpokea na kumpangishia gesti house mume wa mtu, hotokua na la kujitetea habari hiyo ikifika kwa mkeo, mwambie kabisa kwa simu achague mwenyewe.
 
Balaaa huo nayo mtego!sijui utafanyaje maana huyo anakuja kibiashara na pia kukuona!usipoangalia pia unatakiwa kuongeza mtaji huo!
 
Kwa nn hukumwambia kuwa umeoa? Mpaka akapata nafasi ya kukubusu? Yeye alikufanyia ungwana huna budi kulipa fadhira.
 
Uliharibu tokea mwanzo kwa kukosa kuweka mambo hadharani! Labda hofu ya kukataliwa! We mtu mzima. Unajua cha kufanya. Pia usisahau wajibu wako kwa familia yako. Huo ni nambari wani! Mengine yatakuja na kupita! ITS ONE OF MENS' DAYS! Si unakumbuka wenzetu hivi karibuni waliadhimisha WOMAN'S DAY??
 
Makribishe nyumbani na mueleza mkeo kwamba atakuja fulani bin fulani na umwambie namna alivyokupokea wakati ule kule ulipokwenda.Kama una chumba cha ziada alale hapo au ukamwombee kwa ndugu yako aliye karibu.Ukifificha saaana utakuja kuumbuka...
 
Back
Top Bottom