Rozanna Agro Africa
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 809
- 796
Aseh, kwann mwanaume rijali mwenye akili zake anamtia mimba mwanafunz, basi mtumie hata mipira aseh kama kuacha ubakaji mmeshindwa
Hizo ndo hasara mkuu, kuwa na moyo wa uvumilivuNilimuacha akiwa mdogo sana na alikua anasoma shule ya msingi wakati ule Mimi nilikua naondoka mkoani kuja dar kutafuta Maisha..
Miaka ilienda baadae akakua na akawa anaanza elimu ya sekondari , wakati huo Mimi nilikua nimeanza kupata vijihela kidogo nikaona ni bora dogo akasome private ili muda wake mwingi uwe ni shuleni
Ada kwa mwaka ni mil 1.6 amesoma miaka 4 mwaka huu alitakiwa amalize kidato cha 4 ,lakini napigiwa sim na mwalimu wake eti ana mimba tena ya miezi 4
Na Ada nimelipa miaka yote mi nne ,ni zaidi ya milion 7 imetumika,,hapa nawaza naona bora ningeliacha mapema nisinge hangaika nalo..
Mwalimu wake ananiambia tuma nauli mtoto arudi nyumbani , nimemwambia kama hawezi kutembea kwa miguu basi atembelee Tumbo kurudi nyumbani kwao
Aiseee nimecheka sanaIsije kuwa ni matapeli wanataka pesa ya nauli!
Naunga mkono hoja..!Isije kuwa ni matapeli wanataka pesa ya nauli!
mkuu kwenye mpira tunaita "own goal"
so huwa inatokea
Ktk maisha yangu nilishaapa kuwa mwanangu wa kike ana second chance pindi akibeba mimba... Rudi home zaa na umlee, akitimiza miaka miwili peleka Kwa baba yake na urudi shule.. Ukibeba tena mimba usinitambue Kama baba yako Kwan tutakuwa tumeandikishana makubaliano before hujarud shule kuwa Endapo utabeba mimba Kwa Mara ya pili shuleni Mimi na ww we're strangers ... Hata ukijakufanikiwa mbeleni it's for ur own good never consider me.
Uchungu ulioupata na hasira uliyonayo wewe kaka iwe somo... (Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu) kwa wanaume wote wanaofanya mapenzi na wasichana na wanawake bila kinga ya kuzuia mimba.
Asilimia kubwa ya ngono mwanaume Ndo kisababishi hata kama mwanamke Ndo anajilengesha ngono itafanyika tuu iwapo mwanaume ataamua.
Ifahamike kuwa mwanamke hawezi kumbaka mwanaume Ila mwanaume anaweza kumbaka mwanamke.
Aliyempa mimba ni mwanaume kama wewe, awe mkubwa kwako au mdogo, huyo ni mdogo wako tena wa damu ukimtupa umetupa damu mliyoshiriki tumboni kwa mama yako, nasema ni mdogo wako wa damu iwapo mmezaliwa mama mmoja...
Pole kwa yaliyokusibu huo ndo ity uzima, na kuonesha umekasirika na umechukizwa na kitendo alichokifanya mdogo wako, bends kamfate shuleni kwao umrudishe nyumbani kwa wazazi wenu na uwaambie wazazi nampenda sana mdogo wangu na nilimtakia maisha mema Hata nikajitolea kuja kumsomesha mjini.
Kitendo cha yeye kushika Mumbai ambapo amefuta ndoto zake za kujiendeleza kimasomo basi Mie msaada wangu unaishia hapa Ila mpwa wangu akizaliwa (mtoto wa mdogo wako) uko nae bega kwa bega kuhakiki haingii kwenye kosa alilofanya mama yake.
Yeah nimekumbuka kitu, historia huwa inajirudia.... Mmeshajiuliza kati ya baba au mama yenu hakuna aliyepata mtoto akiwa na umri mdogo wa shule au baada tu ya balehe?
Je wewe kaka mtu huna mtoto wa ujanani? Unauhakika hukuwahi kuacha mimba kwa mschana yeyote kwenye makuzi yako ya ujana? Hata kama hukuacha mimba, msaidie dada yako arudi kwa wazazi salama tena Wala usimsemeshe Wala kumuuliza acha wazazi wakaseme na binti yao.
Pia iwe somo kwako utapo oa angalia watoto wako wa kike kwa kiume wasijepata watoto wakiwa bado wadogo, ukaitwa Babu ukiwa na miaka 40 au 45.
Kuna mahali malezi kwa mdogo wako hayakukaa sawa, simtetei sababu mimi ni mwanamke, bali nimelichukulia suala kisaikolojia zaidi na kutokusababisha maumivu zaidi na chuki.
#SAMBAZA UPENDO..
K' Mahaba.
Dah nimekumbuka watoto wa mama ntilie.. NANI ANAJALI?Jamii haijali, wazazi hawajali, watoto hawajali, serikali haijali. Hakuna anayejali