CHA The GREAT
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 651
- 853
Nilipofika ofisi za PPF ili kujua taratibu za utoaji mafao kwa waliopoteza ajira, nilikuta kundi kubwa la vijana ambao wote case yao inafanana. Vijana wote hao (mimi nikiwa miongoni mwao) walikuwa wakitaka kujua utaratibu wa mafao hasa fao la kujtoa. Kabla ya zamu yangu kuhudumiwa kfika, wengi nilianza kuwasikia wakilalamika kwa kusema fedha zetu ila tunanyanyasika. Baada ya mimi kufika dirishani na kutaka kujua kipi ni kipi kuhusu tamko ama maagizo ya Rais kuhusu malipo ya fao la kujitoa, niliambiwa kwamba wao (PPF) hawajapokea maelekeo yoyote. Baada ya kuambiwa hivyo, niliondoka nikiwa nimeinamisha shingo chini kama mwana mkiwa.
Ninachoweza kukisema na kukitolea maoni binafsi ni kwamba, wahusika ambao ni SSRA na waziri mwenye dhamana wanapwaya kwa hili. Nasema hivi kwa sababu sintofahamu hii imekuwa midomoni mwa watu kwa takribani wiki mbili sasa.
Mimi nadhani waziri mwenye dhamana au SSRA ilitakiwa watoe ufafanuzi wa suala hili ili kuweka mambo sawa tofaut na hali ilivyo hivi sasa.