Nilichokishuhudia PPF, bado inasikitisha.

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
651
853
Nilipoingia jengo la PPF pale TAZARA, nilikuta kundi kubwa la watu ambalo idadi kubwa ni vijana. Wengi walikuwa na case moja tu inayofanana. Vijana hao walisikika wakizungumzia tamko la Rais kama lilvyotolewa tarehe 28/12/2018. Ila kadiri muda ulivyokwenda, mmoja alisikika akilalamika kwa kusema fedha ni zetu ila tunanyanyasika. Ilipofika zamu yangu, kwa unyenyekevu kabisa......nikauliza vipi kuhusu tamko la Rais...yule mhudumu akajibu kwamba, hawajapata maagizo yoyote. Nikamshukuru kwa huduma yake na kuondoka kama mwana mkiwa.

Nilichokisoma na ninachoweza kukisema ni kwamba, wahusika ambao ni SSRA, au Waziri husika wanapwaya katika suala hili. Nasema hivi kwa sababu ni takribani wiki mbili zimepita tangu tamko la Rais kuhusu mafao, na kwa muda wote huo kumekuwa na sintofahamu juu ya kauli ya Rais. Wapo wanaoamini kwamba tamko la Rais limerudisha fao la kujtoa.

Kwa uelewa wangu, watu wa SSRA au waziri mwenye dhamana, ilitakiwa wawe tayari wametoa maagizo kwa watendaji wao kuhusu suala hili ama ufafanuzi ili kuweka mambo sawa. Wakati PPF wakileta sarakasi, NSSF wameripotiwa kuanza utekelezaji wa agizo la Rais.

Hii ndiyo Tanzania!!
 
Hakuna watu wasumbufu kulipa kama Nssf mkuu,nafuu hata Ppf
....nenda hapo Ilala /Temeke Nssf utasikia watu wanavyozunguswa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Staff wa ppf wanaishi fresh wenye pesa zao mweee eh eh it's not fare wajameni huruma
 
Back
Top Bottom