Nilichoshuhudia nyama choma za usiku Mombo, Korogwe - barabara kuu ya DSM Arusha

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,587
Habarini za hapa ndugu zangu.

Juzi, nilipata msiba Marangu, Moshi Kilimanjaro, hivyo kutokana na majukumu ya harakati DSM, nikaamua kudrive Alteza yangu Dsm - Marangu usiku usiku. Nikaamua nishuke Mombo, Korogwe kwa ajili ya kupata kinywaji kidogo ili niendelee na safari. Niliwakuta wachaga wenzangu nao wakiwa na msiba mwingine kuupeleka Machame.

Nikaagiza mbavu nyama choma ili nishushie na lite baridi. Nikaona mchoma nyama kapotea ghafla, aliporudi akaja na nyama mbichi nyingine ili anichomee. Nikamuuliza, kwann huchomi hizi ambazo ziko jikoni?Akanijibu zina watu. Nikamwambia sitaki hiyo uliyoleta.

Jamaa mmoja mlanguzi wa ticket ambaye nilimpa bia 1 anywe nikamuuliza, n wapi naweza pata mbuzi 200 wa mkupuo? Akaniambia, labda nisubiri kama mwezi au wiki 3 hivi.Na akanielekeza kijiji cha kufuata (Siyo mbali na Mombo). Nami nikamuuliza, hawa mbuzi wote wanaochinjwa hapa wanatoka wapi?Akanijibu:-

"Bro nyama za hapa siyo. Nyingi n tumbili na nyani toka msitu huu wa kwenda Lushoto. Wanapigwa usiku na kuchunwa.Halafu wanawauzia watu wa misiba wanaopita usiku hapa. Mbuzi n kidogo sana Mombo".

Asanteni.
 
Usipende kula vyakula vya kupikwa ukiwa safarini bora ununue hata soda za azam na biscuits au kabla ya safari mkeo akuandalie bites soda nunua njiani.

Nilijifunza Singida huko tunauziwa nyama sijui za ndege gani wale nishaapa sitakula vyakula vya kupikwa na wabongo maana watu wamekua hovyo sana siku hizi
 
Ngumu kuamini.
Nyama ya tumbili au nyani ina harufu tofauti na mbuzi.
Labda useme ni mbuzi waliokufa kibudu bila kuchinjwa lakini siyo nyani wala Tumbili, Mlevi mwenzio uliomnunulia Bia alitaka kukufurahisha ili uendelee kumpa offer.

Nimekaa Handeni kuna wafugani wengi sana wa mbuzi na ndiyo wanawauzia wafanyabiashara wa Mkata na Mombo.

Hii ni fix ya wazi kabisa
 
Habarini za hapa ndugu zangu.

Juzi, nilipata msiba Marangu, Moshi Kilimanjaro, hivyo kutokana na majukumu ya harakati DSM, nikaamua kudrive Alteza yangu Dsm - Marangu usiku usiku. Nikaamua nishuke Mombo, Korogwe kwa ajili ya kupata kinywaji kidogo ili niendelee na safari. Niliwakuta wachaga wenzangu nao wakiwa na msiba mwingine kuupeleka Machame.

Nikaagiza mbavu nyama choma ili nishushie na lite baridi. Nikaona mchoma nyama kapotea ghafla, aliporudi akaja na nyama mbichi nyingine ili anichomee. Nikamuuliza, kwann huchomi hizi ambazo ziko jikoni?Akanijibu zina watu. Nikamwambia sitaki hiyo uliyoleta.

Jamaa mmoja mlanguzi wa ticket ambaye nilimpa bia 1 anywe nikamuuliza, n wapi naweza pata mbuzi 200 wa mkupuo? Akaniambia, labda nisubiri kama mwezi au wiki 3 hivi.Na akanielekeza kijiji cha kufuata (Siyo mbali na Mombo). Nami nikamuuliza, hawa mbuzi wote wanaochinjwa hapa wanatoka wapi?Akanijibu:-

"Bro nyama za hapa siyo. Nyingi n tumbili na nyani toka msitu huu wa kwenda Lushoto. Wanapigwa usiku na kuchunwa.Halafu wanawauzia watu wa misiba wanaopita usiku hapa. Mbuzi n kidogo sana Mombo".

Asanteni.

Duh aisee hiyo kali
 
Sidhani kama kweli, Mimi nikiwa Congo DRC nimekula sama tumbili ladha yake na nyama ya mbuzi ni tofauti kabisa hata hafuru, wangegundulika tu. Tumbili ana ladha Fulani kama nyati, maana hao wote nimewala sana.
Nimemwambia kadanganywa halafu na yeye anakuja kudanganya Hadhira hapa JF
 
Mleta mada unataka niache kula mbuzi wa Mombo mkuu..

Tena huwa napenda wanavyoonjesha nyama zao

Hadi uagize unakuwa umeshiba

Mimi nitapita tuu Mombo no way...

97244a4c24305757495259d4fc29310c.jpg
 
duuu mkuu unatak kuniambia miaka mitatu yote niliokuwa nasoma Arusha kumbe nilikuwa nalishwa tumbiri pale mombo aiseeee daaaaaa
 
Usipende kula vyakula vya kupikwa ukiwa safarini bora ununue hata soda za azam na biscuits au kabla ya safari mkeo akuandalie bites soda nunua njiani.

Nilijifunza Singida huko tunauziwa nyama sijui za ndege gani wale nishaapa sitakula vyakula vya kupikwa na wabongo maana watu wamekua hovyo sana siku hizi
Pole sana ndugu
 
Uongo mtakatifu kabisa huyo jamaaa kakuchota ili uone ni mwema uendeleze ofa, mimi nawashikaji zangu huko so nimekaa sanaa na watu wanafuka mbuzi na kondoo sanaa japo wote huita nyama ya mbuzi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom