Nilichokiona kwenye simu ya mdogo wangu wa kike! So sad!

Nipe namba yake nimuulize

Sent from my Infinix NOTE 3 using JamiiForums mobile app
 
kaka kama hawa ndio huwa wanaingia kwenye vyumba vya dada zao na kuanza kunusu chupi za dada zao wewe umepewa umsetie simu unaaanza kusoma meseji haya sasa uliyokutano nayo huko unalia nn ssasa.
mkuu kiukweli alichofanya huyu mshkaji ni kuchuma janga...umbea wake umemponza.
 
Kwa dunia ya sasa hata ukimnyang'anya simu hitosaidia jambo la msingi mpe ushauri uliotukuka......kashakuwa mtu mzima huyoo

Sent from my Z5 Premium using JamiiForums mobile app
Rafiki chuma mboga ni nini?......sijamuelewa mleta uzi!

Sent from my Armor using JamiiForums mobile app
 
Dunia ina mambo sana hii lakn pole mkuu ndo maisha ya Dada zetu hawa na ukiwafuatilia sana wanakuita braza mkuda.

Sent from my VF685 using JamiiForums mobile app
 
Ni binti mdogo kamaliza kidato cha nne mwaka Jana kimwonekano ni mpole na mtaratibu sana niende kwenye mada;

Leo mida ya jioni simu yake ilikuwa kwenye lugha ambayo haielewi(Africanas) akaomba nimfanyie setting irudi katika kizungu nikafanya hivyo nikamaliza wakati yeye akiwa nje anaosha vyombo, ndipo akili iliponituma kukagua inbox zake za WhatsApp na SMS za kwaida, duh niliyoyaona nimejuta kuyafahamu.

Chatting nyingi ni mapenzi (mabwana wengi) japo sioni kama ni shida sana kilichokuja kuniuma na kunifanya niandike huu uzi nilipokuta message za wanafundishana mbinu mbalimbali za kufanya mapenzi, kuwatega na kuwachuna wanaume, amejiunga magroup ya WhatsApp ya ukahaba na makungwi wanafundishana mambo ya ajabu, ndo nikahamia kwenye gallery uko ndo basi.

Nimeumia sana japo sijafanya reaction yoyote mdogo wangu kaniumiza alivyo mpole msitaarabu sikutegemea ndo wa kufundisha wenzake mara chuma mboga mara nini.

Naombeni ushauri wadau nimchukulie hatua gani huyu dogo maana ni mdogo wangu ananiuma sitaki aharibikiwe.
simple sana mbona, wewe ndo unamlisha na kumvesha,sio? kama ndivyo makate makofi ya haja(hapa unamdogowesha) baada ya hapo nyang'anya simu, msajilie line nyingine(mnunulie simu ya kitochi tafadhali).. then baada ya wiki hivi kaa nae mpe shule!!! then no kutoka home bila kuaga... make sure anasali km muislam aswali.. ajiunge kwenye vikundi vya dini kama kwaya au madrasa kwa waislam.. huku ukimuomba Mungu.
 
Mkate kelbu za maana kwanza, alaf maelezo baadae
Amuite aongee naye tu taratibu...maana sikuhizi wamekua wajaja sana...mimi nilimshushi kelubu za maana dogo mpka akakimbilia kujifungia chumbani af akajifanya amekunywa sumu eti anataka kufa mpaka mama anatoka kazini kwasababu ya ujinga wake ....
Basi tulipofanikiwa kufungua mlango kila dogo akimshwa haamki, Amsha mtu wapiii haamki...
Nilichokifanya nilimtandika fito tatu kali za miguuni alinyanyuka kitandani na sumu yake kama hana akili nzuri ... mpka sahivi kanichunia mwezi wa sita hivi ila atanikumbuka.

Sent from my SM-G361H using JamiiForums mobile app
 
Mna wapa simu watoto za kazi gani? ana biashara gani kwamba bila simu mambo yake haya endi? ni kheri alaumu tu ila solution no 1 mpokonye simu mengine yafuate
 
mwache akae simu ya mtu ww umepekuaa ya nn yaan ww kaka gani unapekua simu ya mdogo wako wa kike??form 4 kwan mdogo mwache ajifunze asije kuwa gogo bure badae aje kusemwa cha msingi nyumbani ana heshima na anafanyaa yanayotakiwaa hapo nyumbani the rest ni ukuaji tu kitafika kipindi ataacha kama ww ulivyokuwaa unakuaa yapo mengi ya kijingaa uliyoyafanyaa mwache naye ayafaanye at the right tym muda utafikaa ataachaa trust me ..kuwa kwenye magroup dsnt mean kuwa anafanyaa hayo mambo noo ni anajifunzaa lazimaa mtu uwe na elimu dunia na elimu aheraaa cha msingi anawezaa kucontrol mambo yake lastly siku nyingine fanyaa ulichoombwa mengine hayakuhusu!!
Pure pumba
 
Kuna rafiki yangu alipata ajali akapoteza simu zote mdogo wake alikua boarding alimuachia kitochi jamaa akaamua kukitumia baada ya kurenew line, Alikuja kuona sms moja dogo wake anasifiwa ana kitumbua kizuri, naye alikua anamuigizia upole sana. Jamaa ilibid acheke badala ya kuchukia na akampotezea sababu alikua form six na alikua ana perform vizuri aliona atamchanganya kwa jinsi dogo anavyomuheshim bro
 
Pole sana ndugu yangu,dunia imebadilika sana sijui ndio unabii unatimia au la! Kizazi hiki watoto wana mambo makubwa kuliko watu wazima.Chakufanya kaa naye mwambie hali halisi bila kupepesa macho ili ukweli uwe wazi na hata ikiwezekana weka vikwazo kwa baadhi ya mambo kama kupiga marufuku mitoko na safari zisizo za lazima kwa sababu akiukwaa ukimwi wa kusumbuka ni nyie

Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
 
Ongea nae umshauli pengine anaweza badilika make pengine anajuwa hujui lolote

Sent from my TECNO-Y2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom