Nilichokiona kwa huyu Bint Mdogo Mrembo kimenishangaza sana katika Ulimwengu huu wa Sasa

mi nahitaji vitabu vya forex mwenye navyo kidg hivo vinaweza kunipeleka kwenye mkwanja
 
Leo nimeshtushwa sana baada ya kumkuta binti mmoja mrembo amevaa kwa heshima ametulia sehemu anasoma kitabu cha Danielle Steel. Ni zaidi ya miaka 15 sikuwahi ona mtu wa age yake akiwa amekaa anasoma kitabu wakati akisubiria huduma sehemu.

nilifika ofisi moja Mjini kuonana na Jamaa yangu. nikiwa nasubiria huyo mhusika amalizane na mgeni aliye naye ndani katika kutembeza macho sehemu kuangalia tuliopo mapokezi nikiwa nimekaa. mbele yangu nlimwona binti huyu mzuri akiwa ameshika kitabu cha Danielle Steel. kilichonishangaza zaid ni utulivu na nidhamu ya hali ya juu aliyokuwa nayo.niliinuka na kumfuata.taratibu akainua macho yake na kunitizama.akaniamkia kwa heshima.niliitikia na moja kwa moja nikapeleka mkono wangu kukishika kitabu chake pasipo kumwambia neno.

hakufanya hiyana kwa kujiamini kabisa akanichia nichukue kile kitabu.,nikakisoma "Danielle Steel" kwa sauti.
"siamini kama leo hii namwona binti katika umri wako anasoma kitabu kama hiki" nlitamka nikiwa katikati ya mshangao na furaha. alitasabamu kwa aibu akiziba mdomo yake... (moyoni nikawaza "this girl is pretty and smart") niliongea naye sana yule binti nikafahamu ameshasoma vitabu 8 vya Danielle Steele na Pia Sidney Sheldon.

Katika tu maongezi nligundua the girl is bright and confident. Mungu kampendelea kumpa uzuri,akili na heshima.nlitamani yule mdogo wangu brother man asingekuwa heart breaker aje aoe msichana huyu.

Nmeshangazwa kizazi cha Dot Com kusoma novel kubwa kubwa kama za akina Danielle Steel ,Sidney Sheldon n.k alichonichosha zaidi aliponambia kuwa hicho kitabu amenunua tsh 19,000 kwa pesa yake mwenyewe.kama ambavyo alinunua na vingine 4 alivyo navyo.

Haraka akili yangu ikahama nikaanza kufikiria wakati kuna wanawake wanajinadi wanavyojua kukata kiuno na styles mbalimbali za sex.kuna wanawake smart wapo wanaishi nao duania hii hii? Kweli the world isnt fair
Picha yake tafadhali
 
Kati ya vitu ambavyo siwezag kusoma ni novel/hadith

ila haipiti wiki sijasoma kimoja kati ya
Historia,
Geographia
Nakala za afya, Techno lojia, sayansi kwa ujumla, na mambo meng meng ya utundu utundu wa electronics upande wa softiware
n.k
Kwa ufupi nimtundu sana wa upekuzi na ndio kula yangu ilipo, napendaga sana kua updated na mambo mengi hata kama hayanisaidii kiuchumi as long as sio siasa ya leo/sasa labda historia ya siasa maana ni ngumu kutenganisha historia na siasa

Mwanaume kuachana na Pesa na ile kazi yetu pale jimboni unatakiwa uwe mjanja/updated bana
Mwanaume hata ku restore simu huwez? Yan wewe ukipata demu, ukipata hela unabung'aa, kuongeza knowledge nje ya vitabu vya darasani ni kitu cha msing sana
 
Ni jambo jema pia. Maana la msingi ni kusoma na kupata kitu flani kiakili.sijawasoma hao uliowataja sijui maudhui yao yanakuaje

Mi najisomeaga vitabu vya wazalendo wenzangu kina Beka Mfaume, Hussein Tuwa, Richard Mwambe na wengineo wa hapa nchini wanaoandika vya kiswahili tu
 
Waandishi wamegawanyika pia.kuna waandishi ambao wapo very smart nsingependa kuwataja na kuna ambao waandishi but si smart.

Kuna baadhi ya vitabu ukinipa kusoma hata na pesa siwezi soma.mfano vya shigongo.binafsi nliwah jaribu soma hadithi yake kwenye gazeti miaka ya nyuma.nikaona ni ya kitoto sana.nikaachana naye.

Wapo waandishi kama kezihalab, bawji,e.hussein,eddie ganzel n.k hawa wakongwe wamekuwa na uandishi wao unaovutia kwa njia moja au nyingine.
 
iPad,Kindle,simu
... na KOBO eReader
1544241670699.png


Kitabu pichani Download hapa:
 
Back
Top Bottom