Nilichojifunza ndani ya mwaka mmoja bila ajira

Nilichojifunza ndani ya mwaka mmoja bila ajira

Lakini kasema yuko geita...sehem zingine ukifuga bata utaishia kuwala mwenywew!nawaza tu..huko geita bloola hakuna kbs .hawawapendi!
Hao bata ni mifugo ya ziada tu madam ambayo haitompunguzia chochote sana. Na akiwa nao wengi akija humu tunaweza saidiana soko.
 
rejea thread kaka...sikupewa hata mia
Mkuu, labda uniambie ulikua hukatwi hela ya mafao kila mwezi.

Nilichosoma hapo ulikua unadai stahiki zako kwa mwajiri, kitu ambacho ingekua ni mafao ya asingeweza kukwambia nenda kashtaki popote, isitoshe yale ungepewa na mfuko husika.
 
Sasa safi, subiri wan JF waje hasa wenye uzoefu wa maeneo ya Kahama na Shinyanga. Bye the way, hebu nisaidie mimi kwa kuniunganisha na wachimba dhahabu, kama unawafahamu. Nina interest na eneo hilo.Anyway dengu vipi haiwezi kukutoa huko Shinyanga kwani nafahamu inastawi vizuri SHY na wanunuzi wapo wengi huku Dar.
Kahama mji umechangamka sana, hata ukiwa na duka la vitu mbali mbali huwezi kukosa pesa, boda boda na bajaji pia ni Idea nzuri maana ni kama usafiri mkuu pale, sehemu ya chakula mama ntilie huwezi kosa kuuza.
 
Mkuu, labda uniambie ulikua hukatwi hela ya mafao kila mwezi.

Nilichosoma hapo ulikua unadai stahiki zako kwa mwajiri, kitu ambacho ingekua ni mafao ya asingeweza kukwambia nenda kashtaki popote, isitoshe yale ungepewa na mfuko husika.
Alikuwa anakata NSSF lakini nimeenda kuangalia amepeleka pesa ya miaka miwili wakati nina miaka sita pale, halafu hata hiyo kapeleka nusu tu. Nimeenda kuonana na Meneja akamwandikia barua ya wiki mbili jamaa hakujibu akamwandikia nyingine ya wiki moja jamaa kimya. Juzi nimeenda kumwona Meneja ananiambia nivumilie sababu hawapendi kuwapeleka wateja wao mahakamani.
 
Kwa laki 5 yako kaka kwanini usiuze nafaka? achana na kulima kwanza Tafuta mchele, unga, sukari kwa bei rahisi uza kwenye maduka yanayokuzunguka, sehemu za mama ntilie inaweza kukusaidia kukusukuma kidogo.
 
alikuwa anakata NSSF lakini nimeenda kuangalia amepeleka pesa ya miaka miwili wakati nina miaka sita pale, halafu hata hiyo kapeleka nusu tu. Nimeenda kuonana na Meneja akamwandikia barua ya wiki mbili jamaa hakujibu akamwandikia nyingine ya wiki moja jamaa kimya. Juzi nimeenda kumwona Meneja ananiambia nivumilie sababu hawapendi kuwapeleka wateja wao mahakamani
Hapo sawa, ndo mana nilitaka kushangaa, inakuaje akwambie ukashtaki kokote. Hiyo ni yaki yako nilazima atoe ushirikiano kuwa alikua anapeleka hela yako kwenye mfuko husika.

Ingia website ya bunge, chukua namba ya Mavunde mpigie na umweleze kila kitu, atakusaidia.
 
Hapo sawa, ndo mana nilitaka kushangaa, inakuaje akwambie ukashtaki kokote. Hiyo ni yaki yako nilazima atoe ushirikiano kuwa alikua anapeleka hela yako kwenye mfuko husika.
Ingia website ya bunge, chukua namba ya Mavunde mpigie na umweleze kila kitu, atakusaidia.
Nashukuru sana ndugu, kama vilevile naweza kupata namba za wakubwa niwasiliane ili angalau nipate NSSF itakuwa vyema manake huo utakuwa ndo mtaji wangu.
 
Napenda sana nyuzi zenye mafunzo kama hizi. Ni sehemu ya changamoto tu hizo ndugu.
Nyuzi za hivi zinasaidia kuamsha akili na kuwaza mbele zaid mtu ujipange vema kwa lolote mbeleni


Pole mtoa mada bt hongera pia kwa kuamua kuthubutu,hope next time utajipanga vzuri zaid maana una experience sasa na weka tu juhudi utafanikiwa.
 
kwa laki 5 yako kaka kwanini usiuze nafaka? achana na kulima kwanza Tafuta mchele, unga, sukari kwa bei rahisi uza kwenye maduka yanayokuzunguka, sehemu za mama ntilie inaweza kukusaidia kukusukuma kidogo
ahsante mkuu...bahati mbaya au nzuri nimeilimia mahindi ya chakula
 
...nina miaka mi2 sina kazi,..nilifanyiwa figisu kama zako - nimepanga Tabata 250 k per month...watt wa2...mmoja anasoma std 6 Atlas na mwingine std 2 Christ the king...ntakomaa mpaka tone la mwisho hapa mjini

Nb:..figisu za mjini naziweza vizuri tu-wala sio muoga wa maisha.
Christ the king ,upo vizuri boss..
 
Back
Top Bottom