kwenzi
JF-Expert Member
- Aug 25, 2016
- 669
- 666
Majuzi wakati natoka mkoa naelekea Dar kwenye siti yangu nilikaa na Mzee mmoja. Wakati tunapiga story mbili tatu tukajikuta tumeingia kwenye JamiiForums. Mzee akasema naye ni member wa JamiiForums na anapenda sana michango na hoja fikirishi za Mshana.
Wakati anasema hivyo tulikuwa tupo Msata tukacheka sana na Safari ikawa inaendelea...
Sikujua kama JamiiForums ina member wazee nilijua humu tupo vijana tu.Mzee akaendelea napenda sana kuchangia hoja mbali mbali lakini naogopa kuvunjiwa heshima yangu na watoto wadogo, unaweza ukatoa hoja yako ukaishia kutukanwa maana hatujuani humu.
Nilicho gundua ni kwamba humu JamiiForums kumbe wapo watu wazima sana kwa hiyo tusipende kutukana maana waweza mtukana baba yako au mama yako bila ya kujua ukaishia kupata laana tu.