Nilicho kigundua juu ya JamiiForums

Nilicho kigundua juu ya JamiiForums

Wazee wote wako kwenye vijiwe vya kahawa na ugoro, ukimkuta humu huyo sio mzee au labda ni mzee kijana
 
Hii ni platform ya kujenga hoja,ingawa maskhara pia yanakubalika,lakini matusi hapana yanachefua mno.
 
Ukitaka usitukanwe andika vitu vinavyoeleweka.
Mi nashangaa hilo utaskia wazee wa humu wanalalamika eti wameacha kuchangia kama zamani sababu ya matusi,sasa unajiuliza inakuaje mzee wa makamo na kula kwako kote chumvi bado unaogopa matusi tena ya ID fake mitandaoni.kama unaandika vitu vya maana,mtu akikutukana ama kukukwaza siumpotezee au kama imekuuma sana unamripoti tu ale ban shida iko wapi.
 
Majuz wakati natoka mkoa naelekea dar kwenye sit yangu nilikaa na Mzee mmoja .

Wakati tunapiga story mbili tatu tukajikuta tumeingia kwenye Jamiiforums .Mzee akasema naye ni member wa Jamiiforums na anapenda sana michango na hoja fikirishi za Mshana.

Wakati anasema hivyo tulikuwa tupo msata tukacheka sana na Safar ikawa inaendelea...

Sikujua kama Jamiiforums ina member wazee nilijua humu tupo vijana tu.Mzee akaendelea napenda sana kuchangia hoja mbali mbali lakin naogopa kuvunjiwa heshima yangu na watoto wadogo .....unaweza ukatoa hoja yako ukaishia kutukanwa maana hatujuani humu.

Nilicho gundua ni kwamba humu Jamiiforums kumbe wapo watu wazima sana kwa hiyo tusipende kutukana maana waweza mtukana baba yako au mama yako bila ya kujua ukaishia kupata laana..tu

Na ndio uzuri wa jf huo... where we dare to talk openly....
Na hatuhitaji kujuana we need to openly without kuvunja sheria
 
Kama ni hilo basi usiseme umegundua mkuu maana hilo liko wazi tangu siku nyingi na tunafahamu kwamba humu tupo mixture ya watu wengi, rika zote, jinsia zote mpaka akina james delicious wapo humu, watu wa hadhi zote mpaka pogba yupo humu, sadly enough mpaka Daudi mwana wa Bashite naye yumo humu.
Pamoja na kumnanga koote naye ni member basi yu kichwa maji
 
Raha ya jf ni kufunguka boss akikuzingua job jf kijiwe cha wanyonge unamchana
 
sawa kabisa nakumbuka kabla ya uchaguzi 2015 Bwana Lowasa hajakuja Chadema nilitoa post iliyosema MNAONAJE TUKIMCHAGUA LOWASA AWE RAIS WETU nitukanwa na vijana wengine wakaniambia nafikilia makalio
Haya Bwana Lowasa akaja ukawa wale wote walionituka wakawa upande wa mawazo yangu ndo mana niko makini sana na vijana au wazee hatuitajiki humu nijitoe
 
Mi nashangaa hilo utaskia wazee wa humu wanalalamika eti wameacha kuchangia kama zamani sababu ya matusi,sasa unajiuliza inakuaje mzee wa makamo na kula kwako kote chumvi bado unaogopa matusi tena ya ID fake mitandaoni.kama unaandika vitu vya maana,mtu akikutukana siunamripoti tu ale ban shida iko wapi.
Wala huhitaji kumbanisha,unajua tu akili yake ina walakini..utu uzima ni pamoja na kuwa na elimu jamii kama angekuwa mjukuu wako ina maana ungemchinja!si ungejua tu hii ni hasara ya familia.
 
sawa kabisa nakumbuka kabla ya uchaguzi 2015 Bwana Lowasa hajakuja Chadema nilitoa post iliyosema MNAONAJE TUKIMCHAGUA LOWASA AWE RAIS WETU nitukanwa na vijana wengine wakaniambia nafikilia makalio
Haya Bwana Lowasa akaja ukawa wale wote walionituka wakawa upande wa mawazo yangu ndo mana niko makini sana na vijana au wazee hatuitajiki humu nijitoe
Sasa mzee inamaana katika maisha yako yote hujawahi kutukanwa au kuwa challenged kiasi kuwa matusi ya mtandaoni yakufanye ujitoe Jamiiforums?,wazee mmekuwa walalamishi sana.
 
Ndio huku kuna wazee wengi sana mfano babu Dark City na babu Asprin wazee wa heshma.
-🙂 ingawa babu Asprin ameacha kukagua siku hizi. Na dhani ni uzee tu...........-🙁

Adabu ni muhimu na si ajili ya wazee tu. Bali ajili ya kuweka JF juu.
Weeeeee..... ukaguzi uko palepale...

Tena wewe sijakukagua siku nyingi...

Hebu come this way... chapchap sana....
 
Kama anatumia ID fake, anaogopa nini kutukanwa...


Mbona kawaida sana...


Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom