otsward
JF-Expert Member
- Jan 14, 2018
- 300
- 244
Acha kupotosha watu, HIV rapid test bioline na Unigold zilizopo nchini hazipimi uwingi wa virusi bali hupima Ab-Ag reaction ambazo ni chemical zinazalishwa bada tu yamtu kupata mambukizi.Watu wengi licha ya kusoma na kufika level mbali mbali za elimu ambazo si za afya, tuna ule uelewa wa juu juu tu kuhusu mambo ya afya na hasa swala la maamnukizi ya UKIMWI.
wengi tunajua ni kutumia kinga tu.. Ambazo pia unakuta hazitumiwi kwa usahihi. HAPA NIONGELEE KUHUSU NAMNA GANI UTAAMBUKIZWA AU HAUTAAMBUKIZWA NA MTU MWENYE HIV/AIDS
unakuta mtu katembea na dem au jamaa ambaye baadae anashtuka kujua anatumia ARV 's halafu anapaniki na kuanza kulia.. Nikupe siri kwamba endapo utatembea na mtu ambaye ni mwathirika na kwa makusudi anatumia dawa na hajakwambia.. Endapo mtu huyo katumia ARV zaidi ya miez 6 hana uwezo wa kukuambukiza UKIMWI.
Niliona uzi wa mtu mmoja aliyetoa ushuhuda eti aliingia guest house na dada mmoja ambaye alizaliwa na maambukizi na akamkuta na HIV kwa kumpima,...Sidhan kama ni kweli sababu mtu aliyetumia ARV kwa miez 6 na kuendelea hata akipima anaonekana negative sababu ARV zinafubaza wadudu.. ndio maana kuna Nabii mmoja alijinasibu kuponya watu UKIMWI na anawaambie wakapime nje walete majibu. Akijua kabisa hawa watu. Ni watumiaji wa ARV muda mrefu.
Ni rahisi kupata UKIMWI kwa mtu asiyejua kama ameathirika na ukapiga peku.. Kuliko aliyeanza matumizi ya ARV
Hata wenye tabia ya kutembea na vipimo msije mkajipa uhakika wa kuwapima na kutotumia kinga kisa umekuta yuko negative siku hyo...
NB pima, kisha tumia condom.
Hivyo si kweli virusi vikiwa chini kwamba hivi vipimo vitakuwa havisomi.
Ila unachochonganya labda kuna vipimo vya uwingi wa virusi PCR. Na ndio hutumika kumonitor wagonjwa hao mahospitalin hasa kama dawa zinawasaidia, sasa bas hivi sio rapid test kwamba utapata pharmacy au utapima haraka haraka tu.
