Sidhani kama wewe ni mtumishi wa afya, na kama ni mtumishi wa afya basi wagonjwa wetu wanapata tabu sana !
Bila shaka hujui maana ya kufubaza VVU na hujui maana ya hiyo NEGATIVE inayoonekana baadaya ya mtu kupima Viral load baada ya kutumia dawa ndani ya miezi 6.
Kwanza sio kila mmoja anaetumia kwa miezi 6 VVU itakuwa TARGET NOT DETECTED yaani kufubaza VVU kwa kiwango cha Juu bali kwa wale tu waliotumia vizuri kwa kufata masharti. Kwa maana hiyo kuna waliotumia dawa hata miaka kadhaa lakini wana virus vingi sana
Hii hutokana na kutozingatia matumizi mfano kunywa pombe, kutokunywa kwa muda elekezi, kufanya ngono na kupata maambukizi mapya n.k
Kile kipimo hakionyeshi NEGATIVE bali kinaonyesha idadi ya VIRUS ambapo kwa mtu alie tumia vizuri anatakiwa awe na PCs 0 hadi 20 na juu ya hapo inasomeka kama sio mtumiaji mzuri.
Kuhusu kuambukiza au kutoambukiza iko pale pale kutegemeana na mazingira ya kufanya sex. Usidanganyike maambukizi yapo na wote wanaotumia na wasiotumia dawa wanaweza kuambukiza.
Kwa elimu zaidi nitafute!