nikope shiling ngapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

nikope shiling ngapi?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by rebeca, Dec 19, 2011.

 1. r

  rebeca Senior Member

  #1
  Dec 19, 2011
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani nataka kufanya biashara ya gari ya tax pamoja na bajaji moja,zote nataka kununua second hand....ila zisiwe zimechakaa sana zisije kuanza kunipa tabu matengenezo,je shiling ngapi nikope kama mtaji???milioni sita zinatosha kwa vyote viwili?kwa week/siku zinaingiza kama shilingi ngapi?/baada ya muda gani nitegemee kurudisha mtaji?.....wapi nitapata hivi vitu vikiwa in good conditions? nilisikia bandarini wanauza kwa nji ya mnada magari....huwa unafanyika lini?na magari huanzia shiling ngapi kuuzwa???

  thanks in advance......
   
 2. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Labda nikuulize Rebeca, kwa nini umechagua biashara hiyo kama huielewi vizuri?
   
 3. r

  rebeca Senior Member

  #3
  Dec 19, 2011
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwali hakuna aliyezaliwa anajua,kuuliza maswali ni part ya kujua.
   
 4. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  Habari dada Rebeca,
  kwa ushauri wangu mimi kwa kuwa ndo unataka kuanza hiyo aina ya biashara uliyoifikiria, ni vyema ukabadili idea kwa kuwa mtaji wenyewe ni wa kukopa mahali, na kama unavyojua biashara huanza kama mtoto anapozaliwa yaani unahitajika kuwa mvumilivu hadi ikue na kukomaa ( kuanzia miezi 3, miezi 6 hadi mwaka 1). Pili kwa biashara za taxi kwa siku unaweza kupata Tsh 10,000 hadi 20,000 na bajaji ni Tsh 10,000 hadi 15,000 kulingana na hali ya chombo, msimamizi (dereva), mahali zinapofanyia kazi nk.. hivyo kwa hiyo Milioni 6 hata kama ukifanikiwa kupata gari na bajaji nzuri, itakuchukua zaidi ya mwaka hadi miaka miwili kurudisha mtaji.. Una nafasi ya kukopa hadi kiasi gani? kwa riba gani? marejesho ni ya muda gani?..nakushauri fanya biashara hizi zifuatazo kwea huo mtaji (mda mfupi unaweza kurudisha mtaji na kuanza kupata faida):
  - Jiko la Bar
  - Kibanda kizuri cha kuuza chips
  - Choo cha kulipia
  - Duka la vyakula
  - Duka la jumla
  - Kuuza mayai kwa jumla
  - Ufugaji wa kuku
  - Vipodozi
  - Salon ya kiume
  - Fast Food Cafe etc etc
   
 5. r

  rebeca Senior Member

  #5
  Dec 21, 2011
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  thanks,naweza kujaribu hio ya vipodozi.....
   
 6. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Basi acha uwezekano wa kubadili biashara ikiwa utakuta hii hailipi kama ulivo tegemea. Alafu nadhani millioni 6 ni dogo kwa biashara yote mbili. Anza na moja, ikianza kuingiza lipa deni, alafu ndio uanzishe ya pili. Ni mtazamo wangu tu.
   
 7. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Ml6 ni pesa nyingi kwa kuanzia mtaji.ila hiyo biashara ya tax&bajaji sikushauri kuifanya.kuna changamoto nyingi sana ktk biashara hiyo kama kukamatwa mala kwa mala,matengenezo,ajali na mengine kibao.kwa mtu kama wewe ambae pesa unakuwa umeipata kwa mkopo ni hatari kwa afya yako,unaweza pata bp.
   
 8. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Usiende huko fungua duka la dawa na vipodozi na butique ya kina dada u'll make it
   
 9. Ibang

  Ibang Senior Member

  #9
  Dec 22, 2011
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 122
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Habari Dada Rebeca
  kwa biashara yeyote unayotaka kuifanya sisi tutakusaidia na kuifanya kuwa ya kimataifa zaidi
  kama ulivyoambiwa na kushauriwa na wadau hapo juu sisi tutakusaidia kuitangangaza biashara yako online ....
  tu pm kwa maelezo zaidi
   
Loading...