Niko njiapanda ya kuchagua dini sahihi

Niko njiapanda ya kuchagua dini sahihi

Dini ni utapeli usiweke usiriazi sana tupo kwenye hizi dini kwasababu ya kujihusanisha na kuunganika vizuri na jamii.
Nakushauri urudi RC dini uliyoirithi kutoka kwa wazazi wako.
Sahihi
 
Unazaliwa bila kuwa na imani ya dini yoyote ile.

Automatically wewe ni Atheist.

Unazaliwa bila kuwa na imani ya aina yoyote ile.

Atheist ni mtu asiye na imani ya aina yoyote ile ya Mungu au miungu.

Hata imani unayojidai kuiamini sasa hivi, Hukuchagua wewe, bali uliamuliwa na kuchaguliwa na wazazi wako.

Hukuchagua kuamini, ulichaguliwa kuamini na wazazi wako.

Ulivyozaliwa hukuwa na imani ya aina yoyote ile. Wazazi wako walikuaminisha na kukurithisha imani zao kwako.

Kila binadamu alizaliwa atheist bila kuwa na imani ya aina yoyote ile. Mpaka pale wazazi wako walipo kupandikiza imani zao walizopandikizwa na wao na wazazi wao.
Atheism ni kuamini kuwa hakuna Mungu sio kutokujua kuwa hakuna Mungu. Ni sawa tu na anayeamini kuna Mungu(deism) hivyo hakuna anayezaliwa anajua hayo na kuamini au kutoamini uwepo wake ni matokeo ya mazingira uliyopo.
 
Bado hujaiva ktk Critical Thinking mkuu. Ukiiva utakuja kugundua kwamba dini zote zina uimara na zina mapungufu yake. Utakuja kufahamu kwamba Mungu ni mmoja tu na dini ni utamaduni wa wanadamu katika struggles zao za kuitafuta nguvu ya Mungu na kamwe Mungu hakuasisi dini yoyote kwa hiyo zote mbele yake ni sawa tu

Baada ya kufahamu hilo basi ungegundua kwamba ingekua ni advantage kwako zaidi kujenga maisha yako ktk dhehebu ulilokulia kwa sababu una bond kubwa tayari
 
Nimekupa tafsiri ya ASILI na Nimekupa mfano mdogo sana wa SINGELI....... Huelewi nini mkuu?

Singeli haikuwepo kabla vinanda havijaingia Bongo, Kulikua na Sindimba na Mdumange
Singeli ilipokuja kuibuka Bongo itabaki kuwa ni mziki wa ASILI ya Tanzania....... Period(hata kama wahenga watapinga Singeli lakini ndio imeanzia Bongo na itabaki ni asili ya Bongo)
Lakini ukizungumzia Hip hop na Raggae hiyo sio miziki ya Asili ya Tanzania, Hip Hop ni muziki asili ya USA na Raggae asili yake ni Jamaica...... mind you that wakati Hip hop inaanza USA ilikuwepo miziki mingine pia na hii haiondoi ukweli kwamba HIP HOP ni asili ya USA licha kupingwa wakati unaanza kwa kuonekana muziki wa kihuni

Uarabuni kulikua na dini zingine lakini Mudi akaja kuanzisha dini mpya kwa kutumia mila na tamaduni za kiarabu...... Waarabu hawakupinga uislam kwasabu ni dini ya mapokeo toka jamii nyingine waliipinga kwasababu ilianzishwa dini mpya miongoni mwa tamamaduni na mila zao kwa nmana tofauti
Tunapishana kidogo mimi nilikuwa nazungumzia hoja ya watu kutaka turudie ama tufuate imani za mababu zetu, hadi nimekuwa nikiuliza kwamba ni kipi spesho kwa hao mababu hadi tuone kuwa imani walizoziamini wao ndio zilikuwa bora au sahihi? Na ndio maana nikatoa huo mfano wa waarabu ambao wao nao walikuwa na imani za mababu zao.

Nachokielewa mimi mtu anapofuata imani basi huchukulia kuwa ni kitu sahihi, waarabu waliyokuwa wakiamini katika miungu ya kisanamu na kila kabila ama familia ilikuwa na sanamu lao la kuliabudu na wakati waliabudu hadi mawe ukiacha waliyokuwa wakiabudu nyota, mara anakuja Muhammad na kupinga imani zao hiyo miungu yao pamoja na ibada zao na kuwaambia habari ya Mungu mmoja na kuabudu Mungu mmoja tu ndio maana wakampiga vita maana ni kinyume na yale waliyokuwa wakiamini na kuona ni sahihi.

Suala la tamaduni ukiangalia utaona kuwa mambo mengi tu yaliyokuwa sehemu ya utamaduni wa waarabu yalionekana sio sahihi na sheria za hiyo dini uislamu ndio zinakaamua kipi sahihi na kipi sio sahihi.
 
Ingekuwa hakuna Mungu basi kila kiumbe au kila binadamu angekuwa anajiamulia future yake na destiny yake.
Kwa mfano kila mtu angeamua tu awe bilionea kama Mo Dewji au Bakhresa.
Kila mtu angeamua awe na nyumba nzuri,usafiri mzuri.
Ulishawahi kuwaza ni nani anayeamua na kuyapanga haya yote?
Najua hapa utakuja na jibu la magumashi kwamba masikini ni wavivu ndio maana hawatajiriki utasahau kwamba kuna watu wanakesha kazini kila siku na hawatoboi wanaishia kupata hela ya kula tu.
Nakuongeza swali lingine la kutumia logic tu za kawaida.
Kwa mfano watu 50 wanasafiri kwa bus,bus linapata ajali watu 49 wamefariki lakini mmoja anapona na kuendelea na maisha.
Je unadhani huyu mmoja ni nani aliyemlinda hadi akanusurika na kifo hali ya kuwa na yeye alikuwa ndani ya bus hilohilo?
Mkuu Ni nani kakwambia kwamba kama hakuna Mungu inapaswa kuwa hivyo?...... Au ni imagination zako tu zinazotokana na athari za kukaririshwa kila kitu anafanya Mungu?

Tumia akili yako vizuri kutafakari haya...... Kwenye ajali wakifa 49 akapona mmoja hiyo ni COINCIDENCE(wanaweza kufa wote au asife hata mmoja au wakafa baadhi) inategemea tu na position, namna gari lilivyo anguka na namna alivyotingishika wakati gari linapata ajali nk nk.
Hebu chukua watu bilioni moja uwake vichwa uone kama kuna hata mmoja Mungu atamponya...... Hatapona kwasababu kwenye kukatwa vichwa haku COINCIDENCE

Unataka kuniambia Mungu ANAPANGA kila kitu?....... Aiseeee

Kwamba ni Mungu amepanga wale waathirika wa vita kule Sudan, Somali, Congo, Palestina na hata Mdude na Mzee Kibao wapitie madhila wanayopitia kwasababu aliwapangia? Na je wauaji wananafasi gani kwa Mungu ikiwa Mungu ndio aliwapangia waue ili kutimiza MIPANGO yake?

Kama kweli unaamini Mungu anapanga kila kitu kwenye hii dunia Mkuu utakua na matatizo makubwa sana ya Afya ya akili
 
Ingia Katika Dini iliyokuwa kama taasis sio dini IPO mkoa mmoja tu.

Eagt,Moravian, na nyingine kikubwa rohoni umfuate Mungu kweli usibip
 
Unazaliwa bila kuwa na imani ya dini yoyote ile.

Automatically wewe ni Atheist.

Unazaliwa bila kuwa na imani ya aina yoyote ile.

Atheist ni mtu asiye na imani ya aina yoyote ile ya Mungu au miungu.

Hata imani unayojidai kuiamini sasa hivi, Hukuchagua wewe, bali uliamuliwa na kuchaguliwa na wazazi wako.

Hukuchagua kuamini, ulichaguliwa kuamini na wazazi wako.

Ulivyozaliwa hukuwa na imani ya aina yoyote ile. Wazazi wako walikuaminisha na kukurithisha imani zao kwako.

Kila binadamu alizaliwa atheist bila kuwa na imani ya aina yoyote ile. Mpaka pale wazazi wako walipo kupandikiza imani zao walizopandikizwa na wao na wazazi wao.
Sawa tunazaliwa tukiwa hatuna imani ya aina yeyote ile ila pia tukiwa hatuna misimamo ya kupinga imani yoyote ile, lakini kwenye makuzi katika jamii tunakutana na misimamo ya kupinga baadhi ya imani au kupinga imani zote.

Sasa suala la kuzaliwa na kutokuwa na imani yeyote ile haina maana ya kwamba imani zote sio sahihi au hazipaswi kuwepo, maana pia tunapozaliwa tunakuwa hatujui wala wana hatuna maadili yeyote yale ila tunakuja kuyakuta na kujifunza kwenye jamii.
 
Sasa, huoni kama hili jibu unalotafuta ni maelezo katika mfumo wa simulizi?
Kwa sababu hata mtu wa dini naye anaweza kukwambia kufuata dini fulani ni raha sana kuliko kuishi bila dini.
 
Habari wana jf leo ninaswala gumu linanitatiza naitaji maoni yenu.

Kama binadamu wengine namuamini mungu.

Ila napata wakati mugumu kuchagua dini ya kuabudia. Nikisema hivyo namaanisha mini ni mtu ambaye napenda kujifunza sana.

Na kijifunza kwanga kumefanya nibadili jinsi ninavyo itizama dini yangu iliyonelea (ukristo)

Nimekulia katika familia inayo abudua kupitia roman Catholic ila miaka mitano nyuma baada ya kujifunza na kuelewa vitu fulani mimi kama binadamu ninahaki ya kuchagua wapi nikaabudu ivyo nikaamua kubadili na kuwa katika makanisa ya kilokole.

Now nimwaka wa pili sasa huwa najiuliza kama uamuzi niliofanya ni sahihi make najikuta naitaji kubadili tena na safari hii naonelea zaidi kuwa mwisilam (dini ninayoipenda zaidi).

Kinacho nisukuma kufanya hivi sio nafata mkumbo hapana ila kunavitu vingi uwa vinanipa mwaswali na hayo maswali yakikosa majibu basi huwa naitaji kubadilisha msimamo wangu.

Nitaepuka kuweka maswali hayo hapa ili nisianzishe mjadala wa kinidi.

Kiukweli kabisa niko njia panda na ukizingatia naelewa pia sio rahisi kumwamini mungu kwa kuto shiriki katika dini yoyote maana utakosa malezi ya kidini japo wengine ufikili kuingia kwenye dini ni kama kujiingiza kwenye jela yako mwenyewe.

Ntashukulu kwa maoni yako mwana jf.
Unatuuliza vitu gani hivyo? Yaani ufuate dini tutakayokushauri hapa jukwaani? Huo ni undezi!
 
Kwa sababu hata mtu wa dini naye anaweza kukwambia kufuata dini fulani ni raha sana kuliko kuishi bila dini.
Nakupa challenge ya kuishia bila kujihusisha na mambo ya dini kwa mwaka mmoja tu, u-experience raha yake.
Raha za kuambiwa si kitu.
 
Njoo rastafari ila usiwe na uroho wa kula nyama. Fanyia kazi mawazo ya wajumbe na kama haiutapata ufumbuzi Kwa majina yote yaliyotolewa hapo juu basi badili chanel zako uende Kwa waganga wa kienyeji na wao wanadini zao ambazo naamini hujawahi kuzionja
 
Nakupa challenge ya kuishia bila kujihusisha na mambo ya dini kwa mwaka mmoja tu, u-experience raha yake.
Raha za kuambiwa si kitu.
Shida yako ni kudhani kwamba kila mtu ata experience hivyo hivyo mkuu wakati uhalisia haupo hivyo hata kama mimi nikijaribu na ikawa hivyo haina maana kwamba na wengine wote wata experience hivyo hivyo na kwamba hakuna watu wenye kuhisi raha kwenye dini. Kuna watu walikuwa hawana dini ila wakatoka huko na kufuata dini sasa utasema walikuwa wana experience raha ila wakaacha?
 
Shida yako ni kudhani kwamba kila mtu ata experience hivyo hivyo mkuu wakati uhalisia haupo hivyo hata kama mimi nikijaribu na ikawa hivyo haina maana kwamba na wengine wote wata experience hivyo hivyo na kwamba hakuna watu wenye kuhisi raha kwenye dini. Kuna watu walikuwa hawana dini ila wakatoka huko na kufuata dini sasa utasema walikuwa wana experience raha ila wakaacha?
Hakuna sehemu nimesema kila mtu atapata raha kama tuipatayo sisi wengine. So, usiniwekee maneno yako kwangu. Sijihusishi kwa namna yoyote na tafsiri zako na hitimisho la 'shida yako'.
Fikiri kwa umakini zaidi.
 
Back
Top Bottom