Niko njiapanda ya kuchagua dini sahihi

Niko njiapanda ya kuchagua dini sahihi

Kwanini mnaona ni sahihi kufuata imani tu ambazo waliamini wazee wetu bila kufikiri kwamba hizo zilikuwa ni imani ambazo zilikuwepo katika wakati wao tu? Hata hao waarabu kama wasingeletewa uislamu pengine hadi sasa wangekuwa wanaabudu masanamu ndio zilikuwa imani za mababu zao pia.
Mbongo ukishakua kwenye Imani zao toka utotoni ni ngumu kutoka na pia inatakiwa ujue ukweli ndio inakua nzuri zaidi kwa mfano mimi siwezi kumbagua mtu kwa sababu ya dini yake kwa sababu najua chimbuko lake kwa usahihi wasingekuja waarabu na wamisionary ningefata ya wazee wa kale tu..
 
Habari wana jf leo ninaswala gumu linanitatiza naitaji maoni yenu.

Kama binadamu wengine namuamini mungu.

Ila napata wakati mugumu kuchagua dini ya kuabudia. Nikisema hivyo namaanisha mini ni mtu ambaye napenda kujifunza sana.

Na kijifunza kwanga kumefanya nibadili jinsi ninavyo itizama dini yangu iliyonelea (ukristo)

Nimekulia katika familia inayo abudua kupitia roman Catholic ila miaka mitano nyuma baada ya kujifunza na kuelewa vitu fulani mimi kama binadamu ninahaki ya kuchagua wapi nikaabudu ivyo nikaamua kubadili na kuwa katika makanisa ya kilokole.

Now nimwaka wa pili sasa huwa najiuliza kama uamuzi niliofanya ni sahihi make najikuta naitaji kubadili tena na safari hii naonelea zaidi kuwa mwisilam (dini ninayoipenda zaidi).

Kinacho nisukuma kufanya hivi sio nafata mkumbo hapana ila kunavitu vingi uwa vinanipa mwaswali na hayo maswali yakikosa majibu basi huwa naitaji kubadilisha msimamo wangu.

Nitaepuka kuweka maswali hayo hapa ili nisianzishe mjadala wa kinidi.

Kiukweli kabisa niko njia panda na ukizingatia naelewa pia sio rahisi kumwamini mungu kwa kuto shiriki katika dini yoyote maana utakosa malezi ya kidini japo wengine ufikili kuingia kwenye dini ni kama kujiingiza kwenye jela yako mwenyewe.

Ntashukulu kwa maoni yako mwana jf.
Hautakaa upate dini sahihi na zote hazina majibu ya maswali mengi,
Zaidi sana utachanganyikiwa
 
Hakuna live free hata wewe kuna mambo na mitazamo unalazimika kuishikilia kwa sababu ni atheist.
Kila binadamu ni atheist kiasili.

Kila mtu huzaliwa bila kuwa na dini wala imani ya aina yoyote ile.

Hizo imani za kidini mlipachikwa na kuaminishwa na wazazi wenu tu.

Tunarithishana imani vizazi kwa vizazi.
Lakini hakuna anayezaliwa akiwa na imani ya aina yoyote ile.

Ukizaliwa kwenye ukristo utaaminishwa imani ya kikristo na utapingana na uislamu.

Ukizaliwa kwenye uislamu utaaminishwa imani ya kiislamu na utapingana na ukristo.

Religion is a fictional identity.

Emancipate yourself from mental slavery.
 
Shida unapotaka kulazimisha watu wafuate imani fulani kisa tu wao ni asili fulani, imani haipo hivyo. Imani sio sawa kabila kwamba kwa sababu baba yako ni msukuma basi na wewe kabila lako ni msukuma.

Hao waarabu walikuwa na imani za mababu zao pia kabla ya kuletewa uislamu na ndio maana kuna muda hadi panga zilitumika maana kuna waliyokuwa wakizuia huo uislamu kusambaa maana wenyewe walikuwa wanafuata imani za mababu zao.
Mkuu unajua maana ya ASILI....... ASILI maana yake ni chanzo kilichopeleka kutokea.
Hata kama Waarabu walikua na dini zao zingine kabla lakini Uislam pia nao ulitokea hapo kulingana na mila na tamaduni zao plus remix ya hekaya za Uyahudi na Ukristo

Ukisikia Singeli asili yake ni Tanzania haina maana kabla ya singeli hapakuwa na aina zingine za miziki.... Ilikuwepo sindimba mganda mdumange nk ambazo zilikuja kuzaa Singeli iliotokana na ngoma za asili plus vyombo vya kisasa kama vinanda nk

Hata Uhindu ukisambaa dunia nzima na kuwa dini kuu yenye wafuasi asilimia 100 hapa Tanzania bado tutasema Uhindu asilia yake ni India kwasababu ndiko ulikoa ANZIA
 
Kwanini tufikirie dini inapaswa kuwa na majibu ya maswali yote tuliyonayo?
Maswali ya dini unataka uyapatie majibu wapi? Kwenye science?
Dini ndio imani ya mtu na imani ni vitu ambavyo havifikiriki kwa akili za kawaida
 
Jiepushe na dini, epuka kujazwa hofu na matumaini hewa huku ukipigwa pesa zako taratiibu.
Maisha bila dini ni raha mustarehe tu. Hata watu wa dini wengi wanaishi kama sie tusio na dini. Wanaenda kanisani na misikitini mara moja au mbili kwa mwaka. Ila tu, wanaogopa kujiweka wazi kwamba hawataki mambo ya dini.
 
Kila binadamu ni atheist kiasili.

Kila mtu huzaliwa bila kuwa na dini wala imani ya aina yoyote ile.

Hizo imani za kidini mlipachikwa na kuaminishwa na wazazi wenu tu.

Tunarithishana imani vizazi kwa vizazi.
Lakini hakuna anayezaliwa akiwa na imani ya aina yoyote ile.

Ukizaliwa kwenye ukristo utaaminishwa imani ya kikristo na utapingana na uislamu.

Ukizaliwa kwenye uislamu utaaminishwa imani ya kiislamu na utapingana na ukristo.

Religion is a fictional identity.

Emancipate yourself from mental slavery.
Hakuna anayezaliwa akiwa na msimamo kwamba hakuna Mungu, atheist wanajulikana misimamo yao sasa utasemaje tunazaliwa tukiwa atheist? Kutokuwa na imani kunaweza kutokana na kutojua kabisa hizo imani au kuchagua kutokuamini kwa sababu zako, atheist hawana imani kwa madai ya kwamba hakuna uthibitisho.
 
Jiepushe na dini, epuka kujazwa hofu na matumaini hewa huku ukipigwa pesa zako taratiibu.
Maisha bila dini ni raha mustarehe tu. Hata watu wa dini wengi wanaishi kama sie tusio na dini. Wanaenda kanisani na misikitini mara moja au mbili kwa mwaka. Ila tu, wanaogopa kujiweka wazi kwamba hawataki mambo ya dini.
Maisha bila dini yana raha kvp mkuu?
 
Maswali ya dini unataka uyapatie majibu wapi? Kwenye science?
Dini ndio imani ya mtu na imani ni vitu ambavyo havifikiriki kwa akili za kawaida
Swali langu liko hivi, kwanini tunafikiri kwamba dini inapaswa kuwa na majibu ya maswali yote? Yani kila mtu awe na maswali na kutaka dini ijibu, mbona sayansi haina majibu kwa maswali yetu yote wala hiyo sio shida ila dini tu ndio tunataka tuulize maswali tu na iwe na majibu kwa kila swali.
 
Mkuu unajua maana ya ASILI....... ASILI maana yake ni chanzo kilichopeleka kutokea.
Hata kama Waarabu walikua na dini zao zingine kabla lakini Uislam pia nao ulitokea hapo kulingana na mila na tamaduni zao plus remix ya hekaya za Uyahudi na Ukristo

Ukisikia Singeli asili yake ni Tanzania haina maana kabla ya singeli hapakuwa na aina zingine za miziki.... Ilikuwepo sindimba mganda mdumange nk ambazo zilikuja kuzaa Singeli iliotokana na ngoma za asili plus vyombo vya kisasa kama vinanda nk

Hata Uhindu ukisambaa dunia nzima na kuwa dini kuu yenye wafuasi asilimia 100 hapa Tanzania bado tutasema Uhindu asilia yake ni India kwasababu ndiko ulikoa ANZIA
Point yangu ni kwamba kabla ya uislamu waarabu walikuwa na imani za mababu zao kama ambavyo sisi huku mnataka turudie na kutukuza imani za mababu zetu, na ndio maana waliupinga huo uislamu kwa sababu ni kinyume na imani zao wakati huo ambazo ni imani za asili za mababu zao kiasi kwamba hadi nguvu ilibidi itumike.

Sasa kwa mtazamo huo leo hii uislamu unaonekana ni imani asili kwao wakati mwanzo ulionekana ni kitu kigeni kipo kinyume na imani yao ya asili.
 
Nimekupa tafsiri ya ASILI na Nimekupa mfano mdogo sana wa SINGELI....... Huelewi nini mkuu?

Singeli haikuwepo kabla vinanda havijaingia Bongo, Kulikua na Sindimba na Mdumange
Singeli ilipokuja kuibuka Bongo itabaki kuwa ni mziki wa ASILI ya Tanzania....... Period(hata kama wahenga watapinga Singeli lakini ndio imeanzia Bongo na itabaki ni asili ya Bongo)
Lakini ukizungumzia Hip hop na Raggae hiyo sio miziki ya Asili ya Tanzania, Hip Hop ni muziki asili ya USA na Raggae asili yake ni Jamaica...... mind you that wakati Hip hop inaanza USA ilikuwepo miziki mingine pia na hii haiondoi ukweli kwamba HIP HOP ni asili ya USA licha kupingwa wakati unaanza kwa kuonekana muziki wa kihuni

Uarabuni kulikua na dini zingine lakini Mudi akaja kuanzisha dini mpya kwa kutumia mila na tamaduni za kiarabu...... Waarabu hawakupinga uislam kwasabu ni dini ya mapokeo toka jamii nyingine waliipinga kwasababu ilianzishwa dini mpya miongoni mwa tamamaduni na mila zao kwa nmana tofauti
 
Hakuna anayezaliwa akiwa na msimamo kwamba hakuna Mungu,
Unazaliwa bila kuwa na imani ya dini yoyote ile.

Automatically wewe ni Atheist.
atheist wanajulikana misimamo yao sasa utasemaje tunazaliwa tukiwa atheist?
Unazaliwa bila kuwa na imani ya aina yoyote ile.

Atheist ni mtu asiye na imani ya aina yoyote ile ya Mungu au miungu.
Kutokuwa na imani kunaweza kutokana na kutojua kabisa hizo imani au kuchagua kutokuamini kwa sababu zako, atheist hawana imani kwa madai ya kwamba hakuna uthibitisho.
Hata imani unayojidai kuiamini sasa hivi, Hukuchagua wewe, bali uliamuliwa na kuchaguliwa na wazazi wako.

Hukuchagua kuamini, ulichaguliwa kuamini na wazazi wako.

Ulivyozaliwa hukuwa na imani ya aina yoyote ile. Wazazi wako walikuaminisha na kukurithisha imani zao kwako.

Kila binadamu alizaliwa atheist bila kuwa na imani ya aina yoyote ile. Mpaka pale wazazi wako walipo kupandikiza imani zao walizopandikizwa na wao na wazazi wao.
 
Karibu kwenye dini ya haki ndugu utapewa na mwalimu wa kukufundisha Uislamu
 
Mkuu Huko nilikwisha toka siku nyingi sana kwenye kuamini invisible God......... Nilipitia exactly hatua kama unazopitia wewe kwa sasa hadi nilipokuja kubaini PASI NA SHAKA YA ZIADA kwamba HAKUNA MUNGU zaidi ya Hadithi tu za kisadikika

Keep digging.......
Ingekuwa hakuna Mungu basi kila kiumbe au kila binadamu angekuwa anajiamulia future yake na destiny yake.
Kwa mfano kila mtu angeamua tu awe bilionea kama Mo Dewji au Bakhresa.
Kila mtu angeamua awe na nyumba nzuri,usafiri mzuri.
Ulishawahi kuwaza ni nani anayeamua na kuyapanga haya yote?
Najua hapa utakuja na jibu la magumashi kwamba masikini ni wavivu ndio maana hawatajiriki utasahau kwamba kuna watu wanakesha kazini kila siku na hawatoboi wanaishia kupata hela ya kula tu.
Nakuongeza swali lingine la kutumia logic tu za kawaida.
Kwa mfano watu 50 wanasafiri kwa bus,bus linapata ajali watu 49 wamefariki lakini mmoja anapona na kuendelea na maisha.
Je unadhani huyu mmoja ni nani aliyemlinda hadi akanusurika na kifo hali ya kuwa na yeye alikuwa ndani ya bus hilohilo?
 
Back
Top Bottom