Niko njiapanda ya kuchagua dini sahihi

Niko njiapanda ya kuchagua dini sahihi

Adam alikuwa Muislam
Nuhu alikuwa Muislam
Ibrahimu alikuwa Muislam
Isaka alikuwa Muislam
Yakobo alikuwa Muislam
Musa alikuwa Muislam
Daudi alikuwa Muislam
Zakaria alikuwa Muislam
Mariam alikuwa Muislam
Yesu alikuwa Muislam

Kama Kuna mtu alikuambia kuwa hao walikuwa wapagani kama wewe au walikuwa wakristo kama Papa Francis basi huyo amekudanganya
Hii sasa ndio remix ya Mudi dhidi ya original version ya hekaya za wayahudi na wakristo
 
Ukiikomalia sana dini unaonekana una matatizo kwenye mfumo wako wa kufikiri, kutafakari, kuchambua, kuchanganua na kuamua mambo
 
Duuh ndicho kiko akilini mwangu kwasas
So wew hauamini kuhusu mungu ??
Mkuu Huko nilikwisha toka siku nyingi sana kwenye kuamini invisible God......... Nilipitia exactly hatua kama unazopitia wewe kwa sasa hadi nilipokuja kubaini PASI NA SHAKA YA ZIADA kwamba HAKUNA MUNGU zaidi ya Hadithi tu za kisadikika

Keep digging.......
 
Mkuu kwanini husiandike uzi ili kuuliza kitu hicho maana naitaji pia kufahamu maana yake ni nini na nahisi hawajibu kwasababu hawaoni comment yako.
Sio kama hawaoni..wapo wengi sana humu wenye elimu ya quran ila hawana majibu..kuna siri kubwa sana hapo mzee
 
Habari wana jf leo ninaswala gumu linanitatiza naitaji maoni yenu.

Kama binadamu wengine namuamini mungu.

Ila napata wakati mugumu kuchagua dini ya kuabudia. Nikisema hivyo namaanisha mini ni mtu ambaye napenda kujifunza sana.

Na kijifunza kwanga kumefanya nibadili jinsi ninavyo itizama dini yangu iliyonelea (ukristo)

Nimekulia katika familia inayo abudua kupitia roman Catholic ila miaka mitano nyuma baada ya kujifunza na kuelewa vitu fulani mimi kama binadamu ninahaki ya kuchagua wapi nikaabudu ivyo nikaamua kubadili na kuwa katika makanisa ya kilokole.

Now nimwaka wa pili sasa huwa najiuliza kama uamuzi niliofanya ni sahihi make najikuta naitaji kubadili tena na safari hii naonelea zaidi kuwa mwisilam (dini ninayoipenda zaidi).

Kinacho nisukuma kufanya hivi sio nafata mkumbo hapana ila kunavitu vingi uwa vinanipa mwaswali na hayo maswali yakikosa majibu basi huwa naitaji kubadilisha msimamo wangu.

Nitaepuka kuweka maswali hayo hapa ili nisianzishe mjadala wa kinidi.

Kiukweli kabisa niko njia panda na ukizingatia naelewa pia sio rahisi kumwamini mungu kwa kuto shiriki katika dini yoyote maana utakosa malezi ya kidini japo wengine ufikili kuingia kwenye dini ni kama kujiingiza kwenye jela yako mwenyewe.

Ntashukulu kwa maoni yako mwana jf.
rudi kwa paroko wako mwelezee haya uliyoandika hapa atakupa mwongozo. huku mitandaoni utapotea.
 
Mkuu Huko nilikwisha toka siku nyingi sana kwenye kuamini invisible God......... Nilipitia exactly hatua kama unazopitia wewe kwa sasa hadi nilipokuja kubaini PASI NA SHAKA YA ZIADA kwamba HAKUNA MUNGU zaidi ya Hadithi tu za kisadikika

Keep digging.......
Ahaaa, kwa hiyo Mkuu, ulimwengu ulitokea ghafla ghafla tu (kibahati bahati), na vitu vikajipanga vyenyewe (kwa ustadi) kibahati bahati tu?

Fikiria mfano wako (binadamu):

1. Mdomo umetokea kibahati bahati ukakaa mahali hapo ulipo, na pamefaa/endana kabisa na kazi yake—haikutokea mdomo ukajiweka begani, tumboni, au katikati ya miguu—na mdomo una meno, ulimi, na ukaunganishwa na mfumo kamili wa usagaji chakula. Na mfumo huo ukabeba viungo mbalimbali vyenye sifa/muundo maalumu unaopelekea ufanisi wa kazi mfumo huo.

2. Mfumo wa usagaji chakula ukaunganishwa kikamilifu na njia ya kupumua na kuzungusha virutubishi mwilini, kwa usahihi wa ajabu (imetokea kibahati bahati tu?).

3. Viungo vya uzazi vipo katikati ya miguu, sehemu inayovilinda, na sio kichwani mfano pale penye mdomo au macho au utosini. Na kila jinsia ina mpangilio wake wa kipekee na adaptations zinazowezesha uzazi kufanikishwa.

4. Mfumo wa seli na sehemu zake zote, ikiwemo DNA (ndani ya chromosomes)—ambayo imehifadhiwa sana (highly conserved) na hubeba taarifa muhimu zinazofafanua sifa na muundo wa binadamu (traits).

Ikawa ktk uzazi, idadi za chromosomes (46) kwa kila jinsia zinagawanyika kuwa nusu, na zinaungana na nusu za jinsia ya pili kuwa 46 kamili?

Hivi vyote, vinavyofanya kazi kwa usahihi na kwa kushirikiana, vingewezaje kutokea tu kwa bahati bahati pasi na kuwepo aliyevitengeneza na akaamua kuvipanga ktk huo mpangilio wa ajabu usioleta mushkeli ktk ufanyaji wa kazi wa vitu/viungo/mifumo hiyo kwa ujumla?

Mkuu, Vipi nyumbani kwako au chumbani kwako, imewahi kutokea vitu vikajipanga vyenyewe kibahati bahati? Asiwepo aliyevipanga?

Au sofa likajitengeneza lenyewe pasi na kuwepo mtengenezaji (fundi), rangi ya nyumba ikatokea yenyewe kwenye kuta za nyumba yako pasi na kuwepo mtengenezaji wala mpakaji?
 
Mkuu Huko nilikwisha toka siku nyingi sana kwenye kuamini invisible God......... Nilipitia exactly hatua kama unazopitia wewe kwa sasa hadi nilipokuja kubaini PASI NA SHAKA YA ZIADA kwamba HAKUNA MUNGU zaidi ya Hadithi tu za kisadikika

Keep digging.......
Duuh naitaji kusikia meng kutoka kwako kaka
 
Mkuu Huko nilikwisha toka siku nyingi sana kwenye kuamini invisible God......... Nilipitia exactly hatua kama unazopitia wewe kwa sasa hadi nilipokuja kubaini PASI NA SHAKA YA ZIADA kwamba HAKUNA MUNGU zaidi ya Hadithi tu za kisadikika

Keep digging.......
Hivi ulishaga fikilia sayansi ya anga huwa nashindwa kuelewa inawezekanaje yale yote yawe yamepangiliwa kwa usahihi kiasi hicho bila kuwepo nguvu ya kuyafanya yawe katika usahihi huo.
 
Hao budhism wana upekee gani ambao uliuona?
Upekee ni kuwa Buddhism sio chumba.
Sio gereza la fikra.
It is a preachless religion.
Hakuna mtu atakuhubiria au kukulazimisha kuwa Buddhist..
Ni Kwa ajili ya wale wachache waliochoka kutafuta ukweli Kwenye dini za maandiko.
Zen inakurudisha nyuma kujifunza jinsi ulivokuwa indoctrinated na hizo dini.
Zen infact sio dini.
Zen is a realization.
Utarealize kuwa dini ni gereza la fikra., ambalo unalazimishwa kuconform..
Ambalo kiuhalisia hakuna anayeweza kuconform.
Sio mitume,sio masheikh sio wachungaji.

Infact Kila mtu ni Buddhist.
 
Hivi ulishaga fikilia sayansi ya anga huwa nashindwa kuelewa inawezekanaje yale yote yawe yamepangiliwa kwa usahihi kiasi hicho bila kuwepo nguvu ya kuyafanya yawe katika usahihi huo.
Hujawahi kushangaa hiyo nguvu iliwezaje kuyapanga yote hayo? Na hiyo nguvu ilipangwaje?
Au uliishia hapo hapo?
 
Habari wana jf leo ninaswala gumu linanitatiza naitaji maoni yenu.

Kama binadamu wengine namuamini mungu.

Ila napata wakati mugumu kuchagua dini ya kuabudia. Nikisema hivyo namaanisha mini ni mtu ambaye napenda kujifunza sana.

Na kijifunza kwanga kumefanya nibadili jinsi ninavyo itizama dini yangu iliyonelea (ukristo)

Nimekulia katika familia inayo abudua kupitia roman Catholic ila miaka mitano nyuma baada ya kujifunza na kuelewa vitu fulani mimi kama binadamu ninahaki ya kuchagua wapi nikaabudu ivyo nikaamua kubadili na kuwa katika makanisa ya kilokole.

Now nimwaka wa pili sasa huwa najiuliza kama uamuzi niliofanya ni sahihi make najikuta naitaji kubadili tena na safari hii naonelea zaidi kuwa mwisilam (dini ninayoipenda zaidi).

Kinacho nisukuma kufanya hivi sio nafata mkumbo hapana ila kunavitu vingi uwa vinanipa mwaswali na hayo maswali yakikosa majibu basi huwa naitaji kubadilisha msimamo wangu.

Nitaepuka kuweka maswali hayo hapa ili nisianzishe mjadala wa kinidi.

Kiukweli kabisa niko njia panda na ukizingatia naelewa pia sio rahisi kumwamini mungu kwa kuto shiriki katika dini yoyote maana utakosa malezi ya kidini japo wengine ufikili kuingia kwenye dini ni kama kujiingiza kwenye jela yako mwenyewe.

Ntashukulu kwa maoni yako mwana jf.
Bakia hapo hapo njia panda huenda ni sahihi zaidi kwako.
 
Ahaaa, kwa hiyo Mkuu, ulimwengu ulitokea ghafla ghafla tu (kibahati bahati), na vitu vikajipanga vyenyewe (kwa ustadi) kibahati bahati tu?

Fikiria mfano wa binadamu:

1. Mdomo upo mahali hapo ulipo, na pamefaa/endanq kabisa kwa kazi yake—haikutokea ukawepo begani, tumboni, au katikati ya miguu—na mdomo una meno, ulimi, na ukaunganishwa na mfumo kamili wa usagaji chakula. Na mfumo huo ukabeba viungo mbalimbali vyenye sifa/muundo maalumu unaopelekea ufanisi wa kazi mfumo huo.

2. Mfumo wa usagaji chakula ukaunganishwa kikamilifu na njia ya kupumua na kuzungusha virutubishi mwilini, kwa usahihi wa ajabu (imetokea kibahati bahati tu?).

3. Viungo vya uzazi vipo katikati ya miguu, sehemu inayovilinda, na sio kichwani mfano pale penye mdomo au macho au utosini. Na kila jinsia ina mpangilio wake wa kipekee na adaptations zinazowezesha uzazi kufanikishwa.

4. Mfumo wa seli na sehemu zake zote, ikiwemo DNA (ndani ya chromosomes)—ambayo imehifadhiwa sana (highly conserved) na hubeba taarifa muhimu zinazofafanua sifa na muundo wa binadamu (traits).

Ikawa ktk uzazi, idadi za chromosomes (46) kwa kila jinsia zinagawanyika kuwa nusu, na zinaungana na nusu za jinsia ya pili kuwa 46 kamili?

Hivi vyote, vinavyofanya kazi kwa usahihi na kwa kushirikiana, vingewezaje kutokea tu kwa bahati bahati pasi na kuwepo aliyevitengeneza na akaamua kuvipanga ktk huo mpangilio wa ajabu usioleta mushkeli ktk ufanyaji wa kazi wa vitu/viungo/mifumo hiyo kwa ujumla?

Mkuu, Vipi nyumbani kwako au chumbani kwako, imewahi kutokea vitu vikajipanga vyenyewe kibahati bahati? Asiwepo aliyevipanga?

Au sofa likajitengeneza lenyewe pasi na kuwepo mtengenezaji (fundi), rangi ya nyumba ikatokea yenyewe kwenye kuta za nyumba yako pasi na kuwepo mtengenezaji wala mpakaji?
No body knows huu ulimwengu ulianzaje

Kila mtu huwa anajikuta amezaliwa, nayeye atazaa kisha atakufa na aliowazaa wataendelea kuzaliana

Huna unalolijua kuhusu mababu zako vizazi hata 100 nyuma tu, na watoto wa watoto wako vizazi 100 hawatajua lolote kuhusu wewe

Binadamu kiumbe mdadisi(intelligent) haishi kujiuliza mwanzo wa kila kitu, na matokeo yake zikazaliwa DHANA mbili jinsi ulimwengu ulivyoanza
IMANI ikamtengeneza Mungu ndio muumbaji wa kila kitu, na
Sayansi ikatengeneza nadharia(theory) ya namna ulimwengu unvyoweza kuwa ulifanyika

So mimi kutokujua ulimwengu huu ulifanyikaje kwa mpangilio huu wa ajabu HAKUHALALISHI uwepo wa Mungu wako wa mchongo,........ Kwasababu kama unalazimisha kila kitu LAZIMA kina chanzo chake basi unatakiwa uthibitishe na huyo Mungu ni nani kamuumba na maijuzi yake yote hayo ya kuumba ulimwengu smart namna hii, na ukianza kuuliza hivyo hakutakua na mwisho sababu kila kitu lazima kina chanzo
 
Kwanza kabisa lengo la kuishi ni kwenda mbinguni, na ili uwende mbinguni inabida uwe Mkristo kwa maana ya uwe umeokoka yaani umepewa uwezo wa kushinda dhambi ambapo utaongozwa Sara ya toba baada ya hapo inabidi ubatizwe maji tele (unazamishwa mwili mzima) kama biblia inavyosema kwenye Marco 16:16 Aminiye na kubatizwa ataokoka asiye Amin atahukumiwa. Karibu kwa maswali
 
Kwamba Ni maswali yasio na Majibu ndio yamefanya uame imani, na Maswali hayo umeona yana mzozo, na ukaona uislamu unajibu vizuri.

Basi sawa.

Kumbuka kuwa imani aiishihii Mdomoni na kwenye hoja, Bali huenda hadi kwenye nguvu za rohoni.
 
Habari mtoa mada bila kukufanya ujisikie vibaya, kama hutojali nipate umri wako na mahala unapoishi naweza kukushauri kitu.
 
Usiabudu dini abudu Mungu wa kweli dini ni kama taratibu za jamii fulani zinazotokana na imani ya Mungu wao. Ndiyo maana utaona zinatofautiana kwa sehemu na zinafanana kwa sehemu.
 
Karibu katika uislam lakini ukae ukijua dhima kubwa ya kuwa muislam ni kuitafuta akhera yako (wengine wanaita mbinguni) kwahiyo utamiss vitu kama vile

1. Ushuhuda
2. Miujiza
3. Unabii na manabii wa duniani
4. Maombezi kwa ajili ya kupata utajiri
5. Maombezi ya kuponya magonjwa na miujiza ya kuponya vilema

Kiufupi utajinyenyekeza kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kupata pepo yake na sio starehe za dunia
Na siyo kila mkristu anaamini katika hayo mambo matano uliyoandika.
 
Back
Top Bottom