Hauhitaji dini ili kuwa karibu na nguvu kuu, bali uwepo wako tu ni sehemu ya hiyo nguvu... Kanuni kuu ni "upendo", upendo kwa viumbe vyote vilivyo hai na visivyo hai. Ukiishi hivi ni unatimiza mapenzi ya MUNGU.
Ila kama unajihisi mpweke na unahitaji ufuasi (sense of belonging)
basi inatakiwa uwe karibu zaidi na chimbuko lako /utamaduni (huko ndiko una-chemistry nako nzuri kuliko huko kungine).
Tangu na tangu(millennia) watangulizi wako walikua wanawasiliana na huyo Mungu kwa namna yao. Na walilindwa Na ndio sababu hadi hii leo kizazi chao kipo(upo)...
Na kama unaona tamaduni zenu ni potofu na zimepitwa na wakati, kwa mujibu wa wapinzani wako kiutamaduni, basi unaweza ukachagua tamaduni nyingine yeyote Ile... kwasababu hakuna iliyo ya ukweli na hakuna iliyo ya uongo...
Jibu/nguvu ni moja tu ila njia tofauti(tamaduni), njia nyingine ni nyepesi, zingine za wastani ila nyingine ni ngumu zaidi kulingana na asili silka hulka ya jamii husika.
Ndio maana nikakwambia hata huko ulikokua mwanzo kuzuri pia (kuna nguvu ya ushawishi na nguvu ya wafuasi wenye maarifa mbalimbali.