Niko njiapanda Sijielewi Jamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Niko njiapanda Sijielewi Jamani

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Freeland, Jan 24, 2012.

 1. Freeland

  Freeland JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 14,468
  Likes Received: 6,761
  Trophy Points: 280
  Wana jamvi'

  Napiga hodi Jukwaani'

  Nina tatizo la kimapenzi la mda mrefu ambalo naamini humu JF ndo mahala naweza kupata ufumbuzi wa tatizo langu.

  Inahusu maisha yangu ya kimapenzi, Miaka minne iliyopita (2009) niliingia kwa mara ya kwanza katika ulimwengu wa mapenzi,Nikakutana na Leah akiwa mwaka wa kwanza chuoni mimi nikiwa mwaka wa pili.Huyu binti nilimpenda sana naye alionesha kuwa ananipenda,tukakubaliana kwa pamoja kuwa wapenzi,tukaweka misingi ya kutofanya mapenzi hadi tukioana,tukafanya mambo mengi pamoja,tukawa pamoja mda mwingi,fedha kidogo niliyokuwa nayo nilijibana kwa ajili ya kumtimizia mahitaji yake madogo madogo.Tulitambulishana kwa ndugu zetu wa karibu,kweli tukawa wawili.Mimi binafsi nilimpenda sana kuliko mnavyoweza kudhani.

  Nikiwa mwaka wa tatu na yeye akiwa mwaka wa pili nikaanza kuona mabadiliko kidogo,lakini siku namaliza mtihani wa mwisho chuoni na kumaliza degree ya kwanza akaniacha rasmi bila sababu ya msingi.Aliniathiri sana mambo yangu mengi wakati huo nilikua na scholarship ya masters UK nikashindwa kwenda kwa sababu nilimiss deadline kwa sababu nililazwa hospitali kwa muda wa mwezi mzima na ushee.

  Nilikua na bahati kwani mara tu baada ya kumaliza shule nilipata na ajira wakati huo nikiwa nimelazwa.Nikaanza kazi lakini nikiwa bado siwezi kukaa bila kumfikiria Leah,efficiency yangu kazini ikawa sio nzuri.Bosi wangu akaniita akanisihi nimwambie nini kinanisibu,ilinibidi nimweleze.Kwa busara zake akaamua kunipa likizo ya mwezi mzima na leave allowance hapo nikiwa na miezi miwili tu kazini.

  Nikarelax kidogo.Baada ya miezi mitano nikapata msichana mwingine,huyu ndiye alikuwa msichana wangu wa kwanza kufanya nae mapenzi.Lakini nikawa bado simpendi kutoka moyoni.Hakuna siku wala saa inapita bila kumuwaza Leah.Nikawa nashindwa kum care huyu msichana kwa sababu moyo wangu hauko kwake.Tukaamua kuvunja uhusiano.

  Mwaka 2011 Februari nikawa na msichana mwingine ambae niko nae hadi sasa,huyu ananipenda kwelikweli hadi mimi hua naogopa.Lakini moyoni mwangu nalazimisha kumpenda.Ukweli nampenda Leah.Bado siwezi bila yeye.

  Naomba mnisaidie;

  1.Huyu wa sasa ananipenda sana lakini moyo wangu haupo kwake,nifanyeje?
  2.Leah anaonesha kutonipenda kabisa kwa sababu hata nikimpigia simu hapokei,lakini nampenda kulikoni,nifanyeje?
  3.Naogopa kuja kuwa mume msumbufu kwa familia pale nitakapooa nisiyempenda kwa dhati,nifanyeje?

   
 2. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Not every r'ship means to last forever..so mpotezee 2 huyo leah mkuu.
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Duh mkuu pole sana
  Pamoja na kutendwa bado unamuwaza mtu ambaye hakujali wala kukuthamini
  hakuthamini lolote ulilomfanyia na still bado unapata msichana mwingine ambaye anakupenda unamuwaza yule yule aliyekutosa
  Nikuuliza toka amekuacha ashawahi kukujulia hali au kujua unaendeleaje
  Ashawahi kukukumbuka au kukusalimia tuu
  Anajua hata thamani yako kwa wakati huu na maisha yako
  Unakubali kweli kuomba likizo kazini tena ambako umeanza karibuni kisa msichana ambaye hakutambui wala hatambui thamani yako
  Na ulichoona anakupendea ni nini wakati hakuthamini yaleyote uliyomfanyia na akakuacha
  Je huko aliko na mwanaume wake anakujua tena wala kukukumbuka wewe
  Mkuu songa mbele na maisha pambbana na kazi na thamini kakzi yako na thamini penzi la huyo dada uliye nae
  maana unamkatili sana
  Unafanya nae mapenzi huku unamuwaza Leah wako wa zamani
   
 4. M

  MUMY A JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 234
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyo leah mpotezee..utapoteza penzi la kweli la huyo msichana mpya kwassbb ya mtu ambaye unajua kabisa kwamba hana time na wewe......try to concetrate kwny hiyo new relationship and slowly uatamsahau leah.....aaah,kweli mapenzi kizungumkuti
   
 5. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  napita hapa..............
   
 6. xcul

  xcul Member

  #6
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unajua leah anakuona upo weak kwa kumtafuta wakati kesha kutenda ww sepa mkuu koma na huyo mdada mpya tena ni bora huyo unayejua nakupenda kuliko leah ambaye akajali na ukumbuke mkataa pema pabaya panamwita sasa sijui unataka nn akati kama mpenzi ushampata acha uboya kijana
   
 7. isamilo1982

  isamilo1982 Member

  #7
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukishikwa shikamana,mpende akupendae,alafu ukae ukijua mapenzi ya ivo siku iz hakuna mwanamke/mwanaume akikukataa achana naye songa mbele.
   
 8. Freeland

  Freeland JF-Expert Member

  #8
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 14,468
  Likes Received: 6,761
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu.Najitahidi sana kumpotezea ndo maana nimekuwa na msichana huyu mwingine.Tatizo hatoki akilini.Hata sielewi.Nipe mbinu mkuu
   
 9. Freeland

  Freeland JF-Expert Member

  #9
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 14,468
  Likes Received: 6,761
  Trophy Points: 280
  Mkuu Asante sana,Post yako imenijenga.Leo hii wakati napost hii thread ndo kwanza kanipigia baada ya miezi kama nane hivi,ati ananisalimia.Najua simtendei haki msichana wangu wa sasa.Tatizo ni mindset ambayo inanishinda kuibadili.
   
 10. Freeland

  Freeland JF-Expert Member

  #10
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 14,468
  Likes Received: 6,761
  Trophy Points: 280
  Karibu mkuu,nahitaji walau mawazo yako yatanisaidia
   
 11. Freeland

  Freeland JF-Expert Member

  #11
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 14,468
  Likes Received: 6,761
  Trophy Points: 280
  Mumy,

  Asante nakuelewa unachosema.Lakini mbona sasa ni karibu miaka minne hajatoka moyoni na akilini.Itawezekana lini.Nataka kuoa,lakini je nikioa sitakuja kumtesa mke wangu? Mi sipendi ateseke,tatizo moyo
   
 12. Bourgeoisie

  Bourgeoisie JF-Expert Member

  #12
  Jan 24, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 611
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Nani eti? Leah?kipi alichokupagawisha nacho?
   
 13. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #13
  Jan 24, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu msahau na songa mbele na maisha yako na huyo uliyempata na akikutafuta tena mwambie wazi una maisha yako
  Maana kama ndo leo anakutafuta baada ya muda mrefu inaelekea huko aliko mambo yamekuwa sio kama alivyokuwa anategemea na anataka akutafute apate huruma zako
  Mkuu songa mbele acha kuwaza mambo yaliyopita na ambaye ameshapita kwako
  Ingekuwa mlionana kimwili ningeweza kusema mengine ila kwa mtu ambaye hata hamkuwahi kukutana sijui unachomkumbuka ni nini hasa alichokufanyia umkumbuke
  Kwa aliyokufanyia ilikuwa ni sign mojawapo nzuri sana ya kmsahau
  Ila unakubali kumuumiza msichana wako kisa ni msichana mwingine aliyekutosa wakati ukiwa unamuhitaji
  Mkuu acha hizo bana
   
 14. M

  MUMY A JF-Expert Member

  #14
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 234
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama ni miaka minne na bado hajtoka kwny bongo yako nakushauri upige maombi sana,mischana mingine inakupiga limbwata halafu yenyewe inajisepa,so yawezekana amekupulizia...sali sana ndugu yangu na umweleze mungu wako kwnye sala nia yako ni ipi.....it will work...kaza buti
   
 15. Freeland

  Freeland JF-Expert Member

  #15
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 14,468
  Likes Received: 6,761
  Trophy Points: 280
  Mkuu Asante tena.KUMSAHAU.Hili neno ni rahisi sana tunapolisema lakini limekuwa gumu kwangu kulitekeleza.Naelewa huko atakua haja meet expectation may be ndo ananitafuta.Lakini haiwezekani akawa ame make up her mind?
   
 16. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #16
  Jan 24, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Leah si wako
  Hata ukiishi naye atakutesa bure
  Tafuta mwingine ambaye utampenda kama huyu uliyenaye humpendi hata kidogo
   
 17. Freeland

  Freeland JF-Expert Member

  #17
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 14,468
  Likes Received: 6,761
  Trophy Points: 280
  Mkuu,Ndio ni LEAH. Ukiniuliza ni kipi hasa sitaweza kukisema hasa na hata mimi sikijui ni kipi hasa.Kwa sababu kama ni uzuri wa sura huyu wa saivi kamfunika,tabia jibu sina kwa aliyoyatenda.Lakini moyo wangu unakuwaga na amani na furaha ya pekee ninapokuwa nae hata kabla sijafanya nae mapenzi.Ndo hivo mkuu
   
 18. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #18
  Jan 24, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  So kama amemake up her mind still you want to return back to her
  bado hujafunguka mkuu kuwa huyo dada hakupendi
  After four years still u want her back in your life
  tena baada ya kuona mambo sio mambo huko alikoenda
  Je kama amepata ngoma ndo anataka aje akupatie kidogo
  Je kilichomuondosha kwako kipindi kile ni nini mpaka aje arudi kwa kuonewa huruma
  na je akikipata na akakudump tena utajiua kwa sasa au utafanyaje
  Mkuu duh wewe mgumu
  Kumsahau mtu ni uamuzi mkuu na tena unaouchukua baada ya kuona kuwa hakuna kinachowezekana kwa mtu kama huyo
  Umetumia mali zako na resources zako kumnenepesha punda ambaye sana sana at the end of the day hata nyama huwezi kumla
  Ulimsaidia na kumfikisha kwenye kilele cha mafanikio na akakudump kwa kukuona huna mlpango na akapata mtu aliyemuona wa maana kuliko wewe huku akifikiria kuwa mambo yatakuwa safi milele sasa ameona mambo sio mambo anakutafuta tena na still bado unataka kurudi
  Funguka mkuu
   
 19. Freeland

  Freeland JF-Expert Member

  #19
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 14,468
  Likes Received: 6,761
  Trophy Points: 280
  Mkuu,Unajua " Gravitation is not responsible for people falling in love"

  Asante kwa ushauri wako,Kwamba nikimlazimisha ntateseka,sio? kwamba huyu wa sasa anaenipenda sana nikimwacha naye ataanza kuteseka kama mimi ninavyoteseka.Sipendi aumie ingawa kumpenda sio kivile.
   
 20. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #20
  Jan 24, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Woow. Proble. ms of first love. Wewe humpendi Leah bali unafikiri kuwa unampenda. Love maana yake ni sacrifice. Sasa ujuwe kuwa Lea kapata mwingine. Kwa hiyo, concentrate efforts na resources zako zote kwa huyu uliyekuwa nae sasa anaekupenda. Everthing will turn out OK for you and your new valentine.
   
Loading...