Niko kwenye mahusiano na single mother yapata miezi mitatu Sasa, na lengo lilikuwa nimuoe. Huyu mwenzang naona kidogo hajatulia maana nilifuma SMS kwenye simu yake akiwa bado anaendelea kuwasiliana na mpenzi wake wa zamani nikauliza akapoa kidogo na kunambia kuwa jamaa amemtafuta kwa lengo la kumjulia hali. Ana mtoto mmoja mpaka sasa na umri wake ni miaka 20 hivi.
Wiki moja iliyopita sikuweza kuwasiliana nae ndani ya kama siku 5,maana kila nikituma SMS na ata nikimpgia simpati hewani nikashindwa kumuelewa kabisa. Siku ya jumatano alinipigia simu na kunijuza kuwa yuko Moshi kwa dada yake ikabid nimuulze ni kwa nini kaondoka bila kunipa taarifa lakin jibu lilikuwa "nimeondok ghafla pia nilishindwa kuja kukuaga sababu nilikuw busy,naomba unisamehe" kiukwel iliniuma sana nikaona sina thamani kwake kwa lolote lile. Lakini ikabidi nimsamehe tu baada ya kuzungumza nae.
Tangu niko nae amekuw ni mtu wa kutaka pesa tu kila wakati na jana kanipigia simu nimtumie elfu 80, nikauliza ni kwa ajili ya nini anasema matumizi,nikaona isiwe kesi hiyo pesa ntamtumia jioni. Imefika muda wa saa 10 Alasiri jana nikamjuza kuwa niko nje kidog ya mji na huduma za fedha uku ni ngumu kidogo hivyo anivumilie mpaka leo asubuh ndipo nimtumie. Lakini akajibu kwa jazba"najua hunipendi najipendekeza kwako ndo maana unashindwa nitatulia shida zangu kwa wakati" Wakuu nahisi kichwa kinaanza kuuma kwa mbali nikaona hii sehemu nilipo si sahihi hata kidogo,nikatoa laini ile hewani nikaweka laini mpya hivyo mawasiliano yakaishia jana jioni.
Asubuh kaja rafiki yangu ananijuza kuwa yule binti amempigia na kumuuliza kwa nin sipatikani ama niko na mtu mwingine na tangu yeye kaondoka labda kuna mtu alishawahi kuja kwangu na mambo mengi.
Sasa niko njiapanda nimtafute ama niachane nae,msaada tafadhali.