Niko Njia Panda: Namchumbia msichana mwenye mtoto lakini kwetu sitaki wajue ana mtoto

Nimesoma comment haraka haraka, nimesikitika sana.
Kumbe tatizo la single mother ni kubwa hivi?

Mkuu kama umempenda wewe muoe tu, ila ni vizuri mkaweka mambo sawa baina ya familia zenu.

Kuwa na mtoto sio ukilema mkuu, kuna hadi wadada wanalalama hapa kuhusu wewe kutaka kuoa mwanamke mwenye mtoto. Ni bora huyo aliyezaa, kuliko wanaokushauri ujinga.

Dada unaropoka hapa na umeshachoromoa mimba zaidi ya 5 na unamwona mwenzio aliyepata mimba moja na kuilea kama ana bahati mbaya.

Usipomuoa simply kwasababu ana mtoto basi hakikisha unayekuja kumwoa awe bikra na si vinginevyo.
 
10m unampa mtaji dem ambae hujamuoa? kama nikweli basi hujawajua wanawake bt kama si kweli basi hii ni chai TAKATIFU
Wacha niendelee tu kunywa chai na mim,
Maana duu

Mwanaume mzima hela unazo, unashindwa kuowa mke umtakaye kisa ana mtoto?
 
Nimesoma comment haraka haraka, nimesikitika sana.
Kumbe tatizo la single mother ni kubwa hivi?

Mkuu kama umempenda wewe muoe tu, ila ni vizuri mkaweka mambo sawa baina ya familia zenu.

Kuwa na mtoto sio ukilema mkuu, kuna hadi wadada wanalalama hapa kuhusu wewe kutaka kuoa mwanamke mwenye mtoto. Ni bora huyo aliyezaa, kuliko wanaokushauri ujinga.

Dada unaropoka hapa na umeshachoromoa mimba zaidi ya 5 na unamwona mwenzio aliyepata mimba moja na kuilea kama ana bahati mbaya.

Usipomuoa simply kwasababu ana mtoto basi hakikisha unayekuja kumwoa awe bikra na si vinginevyo.
Kama kuna kitu hujaelewa hapa ni kua huyo mdada ndio hataki kuolewa na jamaa sababu pengine yuko na mawasiliano na baba mtoto wake alikua anajua jamaa atakua wa temporary sasa jamaa anataka kuwekeza kabisa au mama yake hataki migogoro hapo mbeleni kutokana na sababu anazozijua ndio mana huyo bint anaweka kigezo cha mtoto mbele, et arekodiwe na sauti akasikilize maongezi ya familia ya kiume sio undezi huo?
 
Aiseeeee!! Narudia tena Aiseee!!!
Mwanamke/ mwenye Mtoto ni mtiti..
Kama Anakataa kuolewa Temana naye Fasta.
Unatoa 10ML Kumpa single Mother
Baharia Unakwama wapi.
Unachokitafuta utakipata.
Ila kama ni Chai tunasubiri ipoe kwanza,, Mzigo wa Malimao upo wa kutosha Nimemaliza.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
True love gives a power to fight for it.
Mkipendana kwa dhati mtashikamana na swala la mtoto halitawasumbua na halitakua na ulazima wa kulifanya liwe siri.

Hisia zinasukuma kukwambia kuwa huyo mwanamke atakusumbua sana. Si kwavile ni singo mama bali hana utayari wa kulilinda penzi.

Satan


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mada nyingine unasoma unakasirika.

Una miaka mingapi?

Kwa nini uliamua kuwaficha wazazi wako in the first place kuhusu mchumba wako kua na mtoto? Uliwaza nini?

Uliona ukiwafichwa unawakomoa au utafanikisha malengo yako ya ujinga vizuri?

Na ni kwa nini unadhani watakataa?

Ndio mara yako ya kwanza kua na mwanamke?

Wewe kinachokusumbua ni ulimbukeni wa mapenzi.

Ushauri wangu, wala usiwaambie wazazi wako, subiri hadi utakapokuja kujua baba mwenye mtoto anaendelea kumtafuna huyo binti uende nyumbani kwenu ukawaambie.
 
Si tumeisha kataa viwanja vyenye mgogoro visinunuliwe? Viwanja visivyo na migogoro vipo.
Hii kitu sielewi inakaaje ati wanawake Fulani wanavaa condom wanajinyima utamu, afu wanawake wengine hawajui hata matumizi ya ndomu utamu wote wale wao, ati kirahisi leo aolewe rasmi kwa Mara ya pili? Inaingia akilini jamani?

Sheria inasema achojoe ndani aliyetoa mahari tu kama mahari bado chojoa kwenye mfuko au asubiri ndoa. Si ndo jamani?
 
Habari zenu, kuna binti niko naye kwenye mahusiano yapata miezi 8 sasa, nimefika hatua ya kutambulika kwao na yeye kutambulika kwetu,

Ila kipindi naanza naye mahusiano aliniambia Ana mtoto anaishi na Bibi, yaan mama yake msichana. Tukaendelea na mahusiano. Kadri nilivyokaa naye naona anafaa kabisa, niwe mkweli. Nikasema nyumbani kuwa nina mchumba wakafurahi, lakin nikihofia wakijua Ana mtoto nitakataliwa.

Baada ya kushibana kabisa nikaamua tuandae mshenga kwa ajili ya kwenda kusema. Akaniuliza kuwa lakin kwenu uliwaeleza kuwa nina mtoto. Nikasema hapana na mtoto wako ni kama wangu istoshe yuko kwa bibi huko tutamtunza tu kwa kuyatuma matumizi na ada ya shule akakubali

Tatizo likaja alipomweleza mama yake kakataa kata kata kwamba lazima mshenga aambiwe kuwa ana mtoto na akasema kwamba kwanza ameahirisha hataki kusikia habari za mshenga wala mgeni yeyote maana kashamchefua tiyari.

Binti akanirudia akiwa na machungu kwamba mama kakataa kasema tutashindwaje kusema kuwa ana mtoto? Pili Binti alimuelezea kuwa nimeshamshawishi kaacha kazi jambo ambalo ni kweli na nimempa mtaji wa 10M aanze biashara yake, lakin pamoja na hiyo mama kakataa

Binti kanipa mtihan kuwa niwaeleze sasa wazazi wangu ukweli na nirekodi wakati wa mazungumzo ajiridhishe kama ni ukweli. Pia kama sitafanya hivyo yeye anafuata familia yake inasemaje, na anasema kwamba anirudishie kila nilichompa aanze upya maisha huku akilia

Naombeni ushauri tunafanyaje, sitaki kwetu wajue , na ukizingatia tumeshaweka malengo makubwa
Umekubali mechi ianze huku upande wake unaongoza goli moja,hongera kwa hilo tatzo ni kuwa wenye watoto wanakuaga na shida 1 akija BABA wa mtoto hawamnyimagi utadhani bado wapo kwny uhusiano vile
Kwahiyo kikubwa chunguza uhusiano alionao kwanza na BABA wa mtoto halafu ndo uingie sasa
 
Unawekewa mashart na single mother? Ungekua karibu ningekunasa kofi la machoni.

Mtaani kuna mabint wazuri tu wamejitunza na wanahitaji kuwekwa ndani we unataka uoe engine iliyofunguliwa, umeniharibia asubuh yangu.

Najisikia vibaya sijafanikiwa kukunasa vibao machoni
 
Back
Top Bottom