Asemavyo
JF-Expert Member
- Oct 22, 2017
- 312
- 821
Jamaa anaomba ushauri Habari zenu, kuna binti niko naye kwenye mahusiano yapata miezi 8 sasa, nimefika hatua ya kutambulika kwao na yeye kutambulika kwetu,
Ila kipindi naanza naye mahusiano aliniambia Ana mtoto anaishi na Bibi, yaan mama yake msichana. Tukaendelea na mahusiano. Kadri nilivyokaa naye naona anafaa kabisa, niwe mkweli. Nikasema nyumbani kuwa nina mchumba wakafurahi, lakin nikihofia wakijua Ana mtoto nitakataliwa.
Baada ya kushibana kabisa nikaamua tuandae mshenga kwa ajili ya kwenda kusema. Akaniuliza kuwa lakin kwenu uliwaeleza kuwa nina mtoto. Nikasema hapana na mtoto wako ni kama wangu istoshe yuko kwa bibi huko tutamtunza tu kwa kuyatuma matumizi na ada ya shule akakubali
Tatizo likaja alipomweleza mama yake kakataa kata kata kwamba lazima mshenga aambiwe kuwa ana mtoto na akasema kwamba kwanza ameahirisha hataki kusikia habari za mshenga wala mgeni yeyote maana kashamchefua tiyari.
Binti akanirudia akiwa na machungu kwamba mama kakataa kasema tutashindwaje kusema kuwa ana mtoto? Pili Binti alimuelezea kuwa nimeshamshawishi kaacha kazi jambo ambalo ni kweli na nimempa mtaji wa 10M aanze biashara yake, lakin pamoja na hiyo mama kakataa
Binti kanipa mtihan kuwa niwaeleze sasa wazazi wangu ukweli na nirekodi wakati wa mazungumzo ajiridhishe kama ni ukweli. Pia kama sitafanya hivyo yeye anafuata familia yake inasemaje, na anasema kwamba anirudishie kila nilichompa aanze upya maisha huku akilia
Naombeni ushauri tunafanyaje, sitaki kwetu wajue , na ukizingatia tumeshaweka malengo makubwa