Niko Njia Panda: Namchumbia msichana mwenye mtoto lakini kwetu sitaki wajue ana mtoto

Habari zenu, kuna binti niko naye kwenye mahusiano yapata miezi 8 sasa, nimefika hatua ya kutambulika kwao na yeye kutambulika kwetu,

Ila kipindi naanza naye mahusiano aliniambia Ana mtoto anaishi na Bibi, yaan mama yake msichana. Tukaendelea na mahusiano. Kadri nilivyokaa naye naona anafaa kabisa, niwe mkweli. Nikasema nyumbani kuwa nina mchumba wakafurahi, lakin nikihofia wakijua Ana mtoto nitakataliwa.

Baada ya kushibana kabisa nikaamua tuandae mshenga kwa ajili ya kwenda kusema. Akaniuliza kuwa lakin kwenu uliwaeleza kuwa nina mtoto. Nikasema hapana na mtoto wako ni kama wangu istoshe yuko kwa bibi huko tutamtunza tu kwa kuyatuma matumizi na ada ya shule akakubali

Tatizo likaja alipomweleza mama yake kakataa kata kata kwamba lazima mshenga aambiwe kuwa ana mtoto na akasema kwamba kwanza ameahirisha hataki kusikia habari za mshenga wala mgeni yeyote maana kashamchefua tiyari.

Binti akanirudia akiwa na machungu kwamba mama kakataa kasema tutashindwaje kusema kuwa ana mtoto? Pili Binti alimuelezea kuwa nimeshamshawishi kaacha kazi jambo ambalo ni kweli na nimempa mtaji wa 10M aanze biashara yake, lakin pamoja na hiyo mama kakataa

Binti kanipa mtihan kuwa niwaeleze sasa wazazi wangu ukweli na nirekodi wakati wa mazungumzo ajiridhishe kama ni ukweli. Pia kama sitafanya hivyo yeye anafuata familia yake inasemaje, na anasema kwamba anirudishie kila nilichompa aanze upya maisha huku akilia

Naombeni ushauri tunafanyaje, sitaki kwetu wajue , na ukizingatia tumeshaweka malengo makubwa
Kwani unaogopa nini kuwaambia?
 
Achana na huyo binti hakufai, kama utakaidi hili basi endelea nae ila jiandae na huo mji wako kuja kuendeshwa na mama mkwe! Hayo maamuzi aliotoa huyo mama wa binti yalitakiwa yatolewe na wajomba sio yeye at the first place. Inaonesha dhahiri ni wale wamama control freaks.

Pili tunaoa kwa ubini wa binti sio ubini wa mama. Achana na hilo zoezi usije kuja kujuta. Kama unampenda sana huyo binti endelea kumfanya hawara wako tu.
 
tatizo kubwa ambalo unakaribia kulifanya ni kuwaficha wazazi wakO ukweli wa mkeo,
Jua maisha ni kuishi na kwenye kuishi kuna mengi hapo badae yatakitokeza ukianza kwakumfichia ilo jua ipo siku utakuja kumfichia jambo baya zaidi ya ilo na utadhalilika wewe, usiogope wazazi watasema nini waambie upendacho,
Mzazi anapenda kumsadia mtoto apate anachokitaka naamini watakuelewa.
Mzazi anaejielewa hawezi kubali huo upuuzi esp. kwa mtoto wa kiume...ingekuwa wakike haina shida ikiwa mume ana mtoto wa ujanani.
 
Back
Top Bottom