moonlightj12
Member
- Dec 6, 2022
- 33
- 90
[emoji120][emoji120][emoji120]Wewe ni thamani,
Hapa duniani hujaja kupita Ili mradi,
Umekuja kwa malengo,
Na lazima uyatimize,
Endelea kujitamkia mazuri,
Maana kinywa chako kina nguvu.
NAKAZIA.Shida nini mama la mama?
Semelea yaliyo moyoni wadau wakusaidie,ukiyatoa ya moyoni nafkiri ni moja ya tiba nzuri kwa kuanzia
Unaonekana una tatizo/matatizo muda mrefu
Afya ya akili(mental health)
Habari Wana jamvi, Msongo wa mawazo na huzuni ni jambo ambalo karibia kila mtu anapitia, ila pengine tunatofautiana ujasili na jinsi ya kukabiliana na changamoto za kila siku. Kumekua na matukio mengi watu wanajiua na wengine wanawadhulu mpaka watoto wao. Nikiangalia huzuni nilioibeba moyoni...www.jamiiforums.com
Mungu ashukuluwe kwa ajili Ako,Polee sanaa Dear,
Niliwahi kumbwa na hali hiyo 9yrs ago,
Nilikua naomba nife, dunia ipasuke niingie, nipotee machoni pa watu, yaan nilikua najichukia.
Ila nashukuru mtu m1 alinishika mkono na kuwa mkombozi wangu, hadi leo hii nipo hapa nikiwa na ujasiri, ari, nguvu, kasi ya kupambana na lolote linalokuja mbele yangu.
Nawee naomba uondoke ktk hali hiyo, kukawe na wepesi ktk hilo.
[emoji120][emoji120][emoji120]
Kuna watu wanazingua, sawa anapitia magumu ila sio kuishia kulaumu tu, kuna wanaopitia magumu zaidi yake na wanaendelea kupambana.Ukiwa Huna neno zuri la kusema kuhusu jambo fulani ni bora ukakaa kimya.
Tambua ya kuwa binadamu tuko tofauti, kila mtu Ana namna yake ya ku cope na changamoto zinazomkabili.
Hujui ni magumu gani anayoyapitia.
kumpa moyo na kumfariji nahis ingekuwa jambo jema zaidi
Nilipitia kipindi Kama chako..Sio mtaalam sana wa kiingereza, lakini kama nipo hai saivi ni kwa sababu naona hamna mtu atakaelea huyu kiumbe niliemleta Duniani.
Kwa huzuni, majukum na uchungu niliobeba ningeweza kumuomba Mungu nife ata leo nipumzike but ni vile Nina jukum la kulea na kumlinda huyu kijana wangu
Basi niseme tu Mungu tusaidie Mungu tukumbuke
Nyie mi nimechoka kua jasiri
Kinywa si lazima sana... Lakini mawazo anayowaza ndio yataamuaWewe ni thamani,
Hapa duniani hujaja kupita Ili mradi,
Umekuja kwa malengo,
Na lazima uyatimize,
Endelea kujitamkia mazuri,
Maana kinywa chako kina nguvu.