Niko busy mpaka hapo umesema kiswahili, nenda kwenye kamusi ya kingereza - kiswahili halafu tafuta neno busy utapata maana yake kisha itangulize niko - maana ya busy. Umenipata aiseeee.
Umeuliza "linatamkwaje", na sio lina maana gani.
Matamshi yake ("pronunciation") kama utalitamka kwa kiswahili japo litabaki limeandikwa kwa kiingereza litakuwa "bizi".
Ila: maana yake (translation) kwa kiswahili ni "kutingwa na shughuli".
Kwa hiyo:
I am busy=Nimetingwa na shughuli
I am very busy=Nimetingwa sana na shughuli.