Nikiwa na umri wa miaka 5, Mimi Deo Kisandu nilimeza Shilingi moja

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,334
Mwaka 1985 hapa wilayani Kahama kulikuwa na Ukumbi maarufu wa Serikali ulikuwa Nyihogo ulikuwa unaitwa "WELFAIR" (OLOFEA) kwasasa ndio ilipo Halmashauri ya mji wa Kahama.

Mwaka 1985 nikiwa na umri wa miaka 5 tulikuwa tunapenda sana kwenda kupanda manguzo ya chuma yaliyokuwa yanashikiria vibaraza, nilikuwa na rafiki zangu wa utotoni Sued Khamis na Baltazan(mwarabu), siku hiyo nilikuwa na Shilingi moja nimeshika mkononi na kaputura yangu haikuwa na mifuko na nilikuwa nimevaa fulana.

Kama kawaida tulianza kukwea nguzo, unakwea mpaka juu halafu unarudi kwa kuteleza chini. Ikafika zamu yangu Mimi Deo Kisandu, nikaweka Shilingi moja mdomoni yaani nikaiuma halafu nikaanza kukwea, katikati ya kupanda nguzo pumzi zikaisha, ile nataka kuvuta pumzi nikaimeza ile Shilingi moja, nikatelemka kwa kasi sana huku na hema. Wenzangu waliniwahisha nyumbani.

Mama alichanganyikiwa sana, Mzee wangu alipopewa taarifa aliuliza tu, amemeza nini. Wakamwambia Shilingi moja akawaambia Huyo hafi namjua Mimi, kama ange meza Sumuni ingeziba koromeo na angekufa. Mzee akaagiza nipewe ndizi za kuiva nile ili niitoe kwa haja kubwa.

Nilipelekwa Hospitali ya wilaya hapa Kahama na kupigwa X-RAY na hela ilionekana iko karibu kutoka, nilishauriwa niwe nanyea nje ili tuione. Baada ya siku mbili ile Shilingi ilitoka na tukaiona.

Kwa kweli sijui Mungu ameniwazia nini, maana ulitokea ugomvi kati ya baba yangu mzazi na baba wa kambo, baba wa kambo alimtamkia baba yangu mzazi kuwa toto lako linakufa, nakumbuka MZEE alisema huyu najua Mimi akifa na babu yangu anakufa(babu yake baba yangu MZEE Kisandu mwenyewe).

Ulikuwa ni mpango wa Mungu kwa kweli mpaka Leo Niko hai. Na mshukru Mungu kwa wema wake.

NB: Nimejifunza kuwa watoto bila malezi ya Baba mzazi ni hatari sana. Na imenifunza zaidi baada ya kuondoka utawani Morogoro kwa mapekupeku(Kwa Padre Ricardo Maria) mwaka April 1999 na kuja Kahama kuendelea na masomo, niliyo yaona na kuya shuhudia ni funzo tosha. Tunapokaa na watoto tujifunze kuwaweka kuwa Hadhina na huo ndio Utundu niliojifunza kutoka kwa DJ wa miaka mingi hapa Kahama mjini na Fundi Radio, baba yangu mzazi Nalimi Kisandu.

Deogratius Nalimi Kisandu
1 Januari 2018.
download.jpg
 
Hiyo shingo kwa umri ulotaja hapo ilikuwa kubwa kiasi gani maana kwa mwaka ulitaja hapo shilingi moja umbo lake kipindi hicho lilikuwa na ukubwa kama shilingi 500 ya sarafu
 
Mwaka 1985 hapa wilayani Kahama kulikuwa na Ukumbi maarufu wa Serikali ulikuwa Nyihogo ulikuwa unaitwa "ALL FAIR" (OLOFEA) kwasasa ndio ilipo Halmashauri ya mji wa Kahama.

Mwaka 1985 nikiwa na umri wa miaka 5 tulikuwa tunapenda sana kwenda kupanda manguzo ya chuma yaliyokuwa yanashikiria vibaraza, nilikuwa na rafiki zangu wa utotoni Sued Khamis na Baltazan(mwarabu), siku hiyo nilikuwa na Shilingi moja nimeshika mkononi na kaputura yangu haikuwa na mifuko na nilikuwa nimevaa fulana.

Kama kawaida tulianza kukwea nguzo, unakwea mpaka juu halafu unarudi kwa kuteleza chini. Ikafika zamu yangu Mimi Deo Kisandu, nikaweka Shilingi moja mdomoni yaani nikaiuma halafu nikaanza kukwea, katikati ya kupanda nguzo pumzi zikaisha, ile nataka kuvuta pumzi nikaimeza ile Shilingi moja, nikatelemka kwa kasi sana huku na hema. Wenzangu waliniwahisha nyumbani.

Mama alichanganyikiwa sana, Mzee wangu alipopewa taarifa aliuliza tu, amemeza nini. Wakamwambia Shilingi moja akawaambia Huyo hafi namjua Mimi, kama ange meza Sumuni ingeziba koromeo na angekufa. Mzee akaagiza nipewe ndizi za kuiva nile ili niitoe kwa haja kubwa.

Nilipelekwa Hospitali ya wilaya hapa Kahama na kupigwa X-RAY na hela ilionekana iko karibu kutoka, nilishauriwa niwe nanyea nje ili tuione. Baada ya siku mbili ile Shilingi ilitoka na tukaiona.

Kwa kweli sijui Mungu ameniwazia nini, maana ulitokea ugomvi kati ya baba yangu mzazi na baba wa kambo, baba wa kambo alimtamkia baba yangu mzazi kuwa toto lako linakufa, nakumbuka MZEE alisema huyu najua Mimi akifa na babu yangu anakufa(babu yake baba yangu MZEE Kisandu mwenyewe).

Ulikuwa ni mpango wa Mungu kwa kweli mpaka Leo Niko hai. Na mshukru Mungu kwa wema wake.

NB: Nimejifunza kuwa watoto bila malezi ya Baba mzazi ni hatari sana. Na imenifunza zaidi baada ya kuondoka utawani Morogoro kwa mapekupeku(Kwa Padre Ricardo Maria) mwaka April 1999 na kuja Kahama kuendelea na masomo, niliyo yaona na kuya shuhudia ni funzo tosha. Tunapokaa na watoto tujifunze kuwaweka kuwa Hadhina na huo ndio Utundu niliojifunza kutoka kwa DJ wa miaka mingi hapa Kahama mjini na Fundi Radio, baba yangu mzazi Nalimi Kisandu.

Deogratius Nalimi Kisandu
1 Januari 2018.View attachment 665667

HUYU MUNGU AMFANYIE WEPESI, MAANA HALI HII SI YA KAWAIDA !!!
 
Back
Top Bottom