Nikionacho Dodoma mjini kinanishangaza!

Nikionacho Dodoma mjini kinanishangaza!

kidi kudi

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2011
Posts
2,769
Reaction score
2,497
Ni mabendera tu ya CCM kila kona ya kuingia na kutoka mjini. Maswali kadhaa nimejiuliza:

1. Dodoma ni nchi nyingine ndani ya Tanzania yenye chama kimoja tu?!
2. Hii jeuri ya kupeperusha mji mzima na ishara ya kuonyesha wapinzani kuwa dodoma mji mzima ni mali 'halali' ya ccm na ole kwa wapinzani wasijaribu kujionyesha kama wapo?!
3. Hiki kinachofanywa si moja ya ishara ya kuonyesha dhana ya ukanda wa kivyama na mwishowe kuhitimishwa na mgawanyo wa wananchi kulingana na kanda inayotawaliwa na chama fulani?!
4. Vp nafasi ya vyama vya upinzani katika upeperushaji wa bendera zao katika miji mbalimbali,je hawatabugudhiwa na vyombo vya serikali?!

Nina maswali mengi sana lakini ngoja nisiendelee zaidi maana sasa hivi nahisi kizunguzungu maana napita maeneo ya DOWASA kuelekea makuru kama unaenda UDOM kuna site panataka kushushwa mijengo, pametapakaa bendera mpaka najiuliza kinachotaka kujengwa hapo mahali ni majengo ya chama au serikali{nna uhakika yanajengwa majengo ya serikali}

Tanzania tunajenga uchama au u-tanzania?

Nawasilisha!
 
Ndo hela za watanzania zinavyoliwa, wala huna haja ya kushangaa. Kama mji wa DODOMA ungefungua mdomo na kusema maovu ya CCM yaliyotendeka hapo hakika hata miji ya SODOMA na GOMORA ingeweza kusamehewa kuliko Mji huo. Ni mji wa kuhararisha wizi, majungu, fitina, mauaji, ........... you name them.
 
mji huu huboreshwa miundo mbinu yake kwa msimu,,kipindi cha bunge,,kipindi cha vikao vya ccm n.k hapo ndipo utaona mamlaka zikiwa bize kukarabati miundo mbinu,,unafiki huu sijui utatutoka lini wabongo
 
Ni bendera tu hizo, ukiwaona kama wamoja kumbe ni mahasimu wa kufa mtu.
 
Hela yako tu. Hata wewe unaweza kuprint bendera zako ukampa jamaa wa bodaboda akazitawanya mji mzima kwa buku ten tu
 
CCM ni Chama cha bendera, kanga, kofia, rushwa. mabango na kila aina ya uchafu unaoufahamu, si cha watu wema, wizi mtupu
 
kidi kudi

Ndugu yangu unaifahamu vyema demokrasia au umejikuta tu ukiwa mshabiki wa chama fulani?
 
Last edited by a moderator:
Wanaweza kusambaza bendera kila mahali hata chini ya uvungu wa kitanda lakini si katika kila mioyo na nafsi za watanzania wote!
 
Ni bendera tu hizo, ukiwaona kama wamoja kumbe ni mahasimu wa kufa mtu.

hakika lakini wanachonishangaza wote wanasema KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI huku matendo yao yakikihujumu chama badala ya kuhujumu HASIMU!
 
Hakika mji umependeza kwa kutawaliwa na kijani, kutoka town kuelekea Nkuhungu , town to airport kote nimeona bendera zikipepea, ulinzi umeimarishwa kila kona, hakika ni chama tawala kinafanya mkutano! Nafikiri na wapinzani wakifanya hivi kusiwepo na shutuma
 
Tatizo kubwa kwa watu wa dodoma hasa warangi na wagogo ni ujinga na udini..........................
Dodoma ni janga la kitaifa kwa ukombozi wa nchi hii......................... Chadema watatakiwa kueneza elimu ya kiraia na kuupiga vita ujinga na udini dodoma kwa nguvu zote
 
CCM ni Chama cha bendera, kanga, kofia, rushwa. mabango na kila aina ya uchafu unaoufahamu, si cha watu wema, wizi mtupu

We mwenyewe mwizi hapo ulipo,tatizo lenu hamtaki kusikia yale msiopenda kusikia,matusi na kejeli yanatoka wapi???acha uzabizabina wewe kalale.
 
sio bendera....ni masanda yao hayo wanayaandaa tayri kwa 2015 wazikwe nayo!
 
Back
Top Bottom