Hauna tatizo lolote, you are very okay... Mimi na wewe tunafanana. Halafu ukiwa mtu wa aina yetu sijui ndo hivi visa unakutana navyo Sana hata siielewi... Unapita zako barabarani, Mara unaona mbwa anakatisha, Mara hee anatokea mtu mzima haswa anaokota jiwe anampiga mbwa. Hapo huwa sijali Yani nisipokukata jicho Kali Basi nitakusema. Mbwa hajakudokolea nyama Wala kukubugudhi kitu unampigia Nini?... Paka au mbwa yupo jalalani anatafta zake chakula angalau ale mtu mzima hovyo unamfyatua jiwe.... Mi nasemaga watakuwa na matatizo ya akili kiukweli.