Zee Korofi
JF-Expert Member
- Oct 5, 2021
- 1,604
- 1,440
Sijui kama ni ugonjwa au sio ugonjwa. Tangu nikiwa mtoto nilikuwa napenda mno wanyama hasa mbuzi, ng'ombe na mbwa. Na nilikuwa na huruma nao mno kiasi cha kulia machozi nilipoona wananyanyasika.
Hali hii nimekua nayo mpaka umri huu, naumia nikiona mtoto mdogo anateseka na magonjwa au anashinda njaa. Huwa nalia machozi nikiwa peke yangu!
Mimi nina behave in a way that jamii inasema nina matatizo ya akili, japo sijawahi kufanya jambo lolote linalothibitisha hilo, kujali kwangu huku kunafanya watu wanione wa ajabu mno.
Huwa napata mawazo ya kufungua kituo cha yatima pindi nikiwa na vihela, huwa nakwenda maeneo ya hospitali kuona wagonjwa, huwa nawanunulia zawadi watoto hata kama siwafahamu. Napenda sana hili!
Nisaidieni, nitafute msaada wa saikolojia? Kwa sababu huwa nikila nawaza watoto wanaokufa njaa huwa nalia mno machozi. Kifupi sina amani ya moyo bado, najilazimisha tu kufurahi na kupitia thread za vichekesho humu JF!
Nipo chuo kwa sasa, ni kijana tu!
Hivi kuna mtu anapitia hali kama hii kweli? Au ni peke yangu? Ni Mungu ananiadhibu? Nimefanya kosa gani?
Naumia mno, hapa ninapoandika nimetoka kulia muda mfupi uliopita.
Nina wazazi wote, sina stress za pesa, nina vihela kidogo vya kunitosha, sina stress za mahusiano, sina chochote cha kusema niwe hivi ukiacha hilo nililoongelea!
Nafikiria kwenda kwa Mwamposa huenda nina mapepo kwani watu wananishangaa mno, ikibidi nimepanga niende usiku wa leo saa 10 alfajiri, nimechoka na hii hali.
Najihisi mpweke, mkiwa na sina amani, chakula hakinogi sana, kifupi kichwa changu hakipo sawa, kila nikiona watoto wanateseka nalia mno, naomba niishie hapa!