Nikiona wanafunzi wa Sekondari na Vyuo wanaenda shule, naona kama wanaenda kupoteza muda na pesa

AlphaMale

JF-Expert Member
Oct 26, 2019
613
1,402
Maana sasa ajira hamna (statistically ajira zipo chache mno), wanaenda kusomea nini cha ziada? mm naona elimu ya form 4 inatosha kabisa kuishi kitaa, mtu akishajua hesabu ya kujumlisha, kutoa, kugawanya, kuzidisha, kusoma na kuandika kiswahili na kingereza, bookeeping inatosha vizuri tu, + kama profesionals wanahitajika, mtu akimudu practicals za kuwa mwanasheria/daktari/rubani etc inatosha sana, kuliko kupoteza miaka mitatu chuo ya kukariri theories za watu wengine.

Mtu akitaka kusoma theories za wengine asome kwa kupenda yeye na sio kwa kulazimishwa, kwa kuambiwa kuwa akifanya hivyo ataongeza chances zake za kuajiriwa wakati ajira hamna.

Huu mfumo wa kusoma na kulipia ada kuanzia shule ya msingi hadi chuo nadhani upo ili kuwafaidisha watu wachache.

Wale mtakaokuja ku-comment kunipa pole kwa ninayopitia mnakaribishwa.
 
Hata mimi huwa nawaangalia wanachuo kisha nasema hiiiiiiii!!

Kimsingi elimu ya sasa hivi inatakiwa itolewe ya kumsaidia mtu akiishia chuo kikuu, form six au form four imsaidie kujiajili.
Baadhi ya masomo kama vile Biashara, Kilimo, haya yangemsaidia muhitimu pamoja na taifa.
 
😂😂 akimaliza atakuja tu. Awamu ya 5 imechochea ukosefu wa ajira. Sasa nasubiria maoni ya Kawe Alumni nione atasemaje 😂.
Wakati Mwingine Tunapokuwa Kwenye Mitandao Tunaukataa Ukweli Unaosemwa Na Watu Ambao Wanapitia Magumu
Baada Ya Kupata Elimu Zao Nzuri Sana.

Ingawa Ukweli Uliopo Tunao Ndugu Zetu Wanahangaika. Sasa Ukitazama Unasema Hii Shida Kwasasa Hivi Ni Kubwa
Shuhuda, Za Jamiiforums.com Ni Nyingi Sana
 
Wakati Mwingine Tunapokuwa Kwenye Mitandao Tunaukataa Ukweli Unaosemwa Na Watu Ambao Wanapitia Magumu
Baada Ya Kupata Elimu Zao Nzuri Sana.

Ingawa Ukweli Uliopo Tunao Ndugu Zetu Wanahangaika . Sasa Ukitazama Unasema Hii Shida Kwasasa Hivi Ni Kubwa
Shuhuda, Za Jamiiforums.com Ni Nyingi Sana

Nipo nawaza hapa. Angalau serikali iruhusu watu turudishe vyeti halafu tupewe angalau robo ya ada ili tukafanye mambo mengine. Halafu vyeti vifutwe kabisa.

Maana ajira hazipo, na chache zilizobakia ni za connection na za sekta binafsi zinakufa maana sekta binafsi inakufa kwa kushambuliwa na makodi.

Ila kwa sasa tatizo ni kubwa na watu nyomi wanazidi kuingia vyuo na kumaliza.
 
Elimu ni muhimu, tena sana... Hata huko kujiajiri kama huna elimu na hujitambui utaishia kupata tu hasara na biashara itakufa.
Usije tu ukawanyima watoto wako haki yao ya kusoma kwa kuogopa kupoteza hela mkuu.
 
Bahati mbaya sana kwako akili yako inaamini waliofanikiwa ni wale walioajiriwa tu Bill gate mwajiri wake nani, Mo Dewji anafanya kazi wapi? Dangote mwajiri wake nani? je Reginand Mengi aliajiriwa ofisi gani mpaka anaitoka dunia?
 
Hao waliopo kwenye ajira wanaishi milele?

Hao waliopo kwenye ajira Hawatostafu?

Makampuni mapya yanaanzishwa
yatafanywa na hao hao waliopo sasa?

Kwahiyo Daktari anatakuwa yule aliyemaliza form four tu?

Hakimu yuleyule Form four ?

Muuguzi yule yule form four?

Nataka kujua tu Hivi umeacha kufanya mapenzi?kama bado unaendelea unataka mtoto anayezaliwa kutoka kwako akafundishwe na nani shuleni kama hutaki watu waende Chuo?

Hivi umeacha kutumia Internet? Unategemea tukifuata ushauri wako nani atatoa huduma kwenye field ya Network.

Umesahau kuwa bado Nchi inahitaji sana Uzalishaji katika kilimo ? Au unataka tutumie technolojia dhaifu katika uzalishaji nakukumbusha kuwa kwenye kilimo wakemia wanahitajika,Waandisi, na taaluma mbalimbali. Kwenye kilimo bado fursa ipo wazi kabisa tatizo lako umekariri kuwa lazima Uajiriwe.

Nakukumbusha tu kuwa Baada ya kumaliza Chuo akili yako ikilala mambo yatalala Ukichangamka na kutumia vizuri field yako Utatoboa haraka sana.Kila taaluma unaweza kufanya shughuli binafsi au kwa kuajiliwa.Acha Julia lia Peleka mtoto Shule.
 
Back
Top Bottom