Mimi ni mtumiaji wa pombe kwa muda wa miaka 26 hivi kwa muda wote nimekuwa nikinywa castle lager kama pombe niipendayo na mara chache sana pombe kali na wine wakati nasoma O-Level nilikuwa nakunya mara chache weekend na siku ya shughuli nyumbani au shule, nilipo kwenda A-Lavel Mazengo sec kidogo intake iliongezeka kwani weekend karibia zote nilikuwa nakunywa na mara chache katikati ya wiki nilipokwenda chuo pale DIT nakumbuka siku nisipo kumywa nakuwa kama mjinga na mbaya sana nilikuwa siwezi kufanya mtihani bila ya kupata kidogo nakumbuka ikifika ijumaa nilikuwa nakuwa kama mwenda wazimu kama nikiwa sina hela
Baada ya kumaliza chuo nakumbuka niliamua kupunguza kunywa baada ya kuobwa sana na familia na nilipunguza kwa kiasi kikubwa sana kiasi hata week mbili au mwezi ulikuwa unapita bila kunywa wakati huo nafanya kazi.
Tatizo la lunywa kila siku lilianza tena muda mfupi kabla ya kuoa na mpaka sasa naweza kunywa castle lager 15 nikanchanganya na konyagi lakini silewi zaidi ya kuchamka kidogo basi.
tengeneza cocktail mwitu.
Viungo ni kama ifuatavyo
castle lager 3
safari 2
konyagi vimobitel 2
sminorf 1/2 chupa
wanzuki lita 2
banana chupa 1
coca cola 1
halafu kunywa coctail hii iishe ndani ya nusu saa.
Hapo tatizo lako litakwisha kabisa,kwa ushauri zaidi tembelea ofisi yangu.kwa dar niko uwanja wa fisi.arusha napatikana matejoo na kambi ya fisi.
Pepo la ulevi, utabalisha vilevi vyote lakini haitakusaidia.
Angalia badget yako ya ulevi ilivyo nzuri:-
Castle 15 x 2000.00 = 30,000.00
Konyagi 1 x 5000.00 = 5,000.00
Castle 10 x 2000.00 = 20,000.00 kwa marafiki
Jumla 55,000.00
Kwa mwezi 1,650,000/=
Unataka alewe au afe kibudu....so they say in pare hills.
Kama ulewi tatizo liko wapi? Au safari zako za kwenda ATM zimepungua???
Beer hazikufai,kunywa whisky na wine lakini home msosi uwepo.Sio unakunywa afu unakula ugali maharage zitakurudi.kama huna pesa kunywa gongo.
Hakuna ulazima wowote kwa wewe kunywa pombe, unaharibu bajeti ya familia yako, nakushauri uiache mara moja.