Niking'atwa na nyoka usiku nifanye nini?

Mkuu umeanza vizuri hasa ulipodai maisha matam yanaanzia miaka 40 na wew umeshafika umri huo. Ambacho sijaelewa unaendaje kuishi na manyoka wkt umeshafika umri wa kutambua thamani na raha ya maisha?
 
Yanauzwa wapi na Je ni kweli linafanya kazi vizuri au ni uzushi tu stori za kuwaondolea hofu watoto waende shambani wakalime?
Ukiumwa na koboko ukaleta story za kuweka hilo jiwe,hakikisha umetafuta waimbaji kabisa wa nyimbo za msiba ndo uendelee na mengine
 
Mwaka kesho natimiza umri wa miaka 40 na kama bajungu basemavyo kwamba Life begins at 40 kwa hiyo ninampango wa kuhamia na kwenda kuishi kijijini mbali kabisa nimeishaanza kujenga jumba langu la kifahari palace ndogo yani msoga of my own making hekalu kwa namna nyingine.

Sasa huko ninapotarajia kuhamia ni porini sana na inasemekana koboko wapo.

Nimeona ni vema kuja kuchukua maarifa kwenu wandugu nikipatwa na dharula kama hiyo ya kung'atwa na nyoka hasa usiku nijiokoe vipi?
Mkuu kama una vipesa, andaa hata ng'ombe 3 nenda vijijini huko katafute mababu uwape wakuoneshe dawa.

Kati ya dawa ambavyo very effective za kienyeji nilizowahi kushuhudia ni DAWA YA NYOKA na KUUNGA MIFUPA.

Aisee kwa hivyo vitu viwili, kuna dawa za asili nu BALAAA.

Kuna babu mmoja yeye ukiumwa na NYOKA, anatembeatembea huko anachuma majani fulani, anayatafuna akija anakutemea temea tu ulipoumwa, kwishaa.

2012 nusura nimpoteze shemeji yangu, aliumwa na nyoka usiku akapelekwa hospital mizunguko mingi hadi ulimi ulikuwa ushaanza kuvimba.

Wakamtoa faster na kumpekeka kwa babu, ni nomaaa.

Maana hospital wanachofanya ni kukutundikia tu Drip la maji ya kuondoa sumu, wakichelewa unakata moto.
 
Hivi kuna ulazima wa ku-comment kama huna point ya msingi???

Back to the thread.

Pale nyumbani upande majani aina ya ukoka. Ukiumwa na nyoka tafuta jani la ukoka (mrefu Kama kamba) zungushia juu/chini kidogo ya ulipoumwa, baada ya hapo kunywa mkojo.


Jani la ukoka linazuia sumu ya nyoka kupanda/kusambaa mwilini
 
Fanya fumigation na kuweka dawa zinazofukuza nyoka,fyeka vichaka vyote karibu na nyumba.
dhibiti wanyama wadogo kama panya hawa huwavutia sana nyoka.Hakikisha nyumba yako
haina matundu au uwazi ambao nyoka anaweza kuingia na jitahidi kutoacha milango wazi hasa majira ya jioni na usiku.

Ikitokea ukamuona yupo nje au ameishaingia ndani,sio vizuri kufanya jaribio
la kumshambulia moto wake sio mdogo,ni heri utafute wataalam wa wanyama pori,kama hujajipanga basi usihamie
mpaka uongee kwanza na wenyeji wa huko wakujuze wao wanaishi nao vipi.
kwa leo ndo hayo.
 
Ushauri wako ni upi tofauti na jiwe?
asilimia 85 ya nyoka wote hawana sumu,hivyo mtu alipoona ameumwa na nyoka bila kujua ana sumu au hana
alipoweka jiwe akaona hakupata madhara akajua jiwe ni dawa,kumbe ilikuwa bahati tu.
Pia ikumbukwe sumu za nyoka zinatofautiana ukali wake.Kuna nyoka akikuuma sumu yake inaozesha nyama mahali pale alipokuuma,
kuna anayekuuma sumu ikaingia kwenye damu,na kuna hao akina koboko,cobra n.k hawa sumu yao inashambulia neva na inaua haraka sana
usipopata matibabu.
 
Nakumbuka kuna shule nilisoma olevel ina nyoka balaaa. Kwenye Joining instruction wameagiza mwanafunzi aje na jiwe la nyoka.

Toka naanza form 1 hadi form 4 nilikuwa natembea na jiwe kiuoni kama hirizi. Huko kwenye viunga ni kukutana na nyoka mwanzo mwisho
Mkoa gab huo chief
 
Choma mipira ya matairi kuzunguka sehemu za nyumba mara kwa mara. .husaidia Sana kuwafukuza nyoka lakini pia jitahid usikose mafuta ya taa na chumvi pindi ikitokea nyoka amekuja maeneo ya nyumbani .njia rahisi ya kumuua ni kumwagia chumvi na mafuta ya taa ...hufanya awashwe Sana na kuanza kujipiga piga mwenyewe ...so inakua rahisi kumuua ...
 
Nakumbuka kuna shule nilisoma olevel ina nyoka balaaa. Kwenye Joining instruction wameagiza mwanafunzi aje na jiwe la nyoka.

Toka naanza form 1 hadi form 4 nilikuwa natembea na jiwe kiuoni kama hirizi. Huko kwenye viunga ni kukutana na nyoka mwanzo mwisho
Shule ipi hiyo?
 
Kwa kule kwetu Songea kuna majani na mizizi ya mti wa mpoto mpoto, unayachuma na kuchimba na kuyaunguza hadi yatoe harufu na kuwa jivu, then unamwaga ktk eneo lako unaloishi, nyoka wa aina yeyote hasogei hapo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom