Niking'atwa na nyoka usiku nifanye nini?

Paramagamba

Member
May 12, 2017
85
129
Mwaka kesho natimiza umri wa miaka 40 na kama bajungu basemavyo kwamba Life begins at 40 kwa hiyo ninampango wa kuhamia na kwenda kuishi kijijini mbali kabisa nimeishaanza kujenga jumba langu la kifahari palace ndogo yani msoga of my own making hekalu kwa namna nyingine.

Sasa huko ninapotarajia kuhamia ni porini sana na inasemekana koboko wapo.

Nimeona ni vema kuja kuchukua maarifa kwenu wandugu nikipatwa na dharula kama hiyo ya kung'atwa na nyoka hasa usiku nijiokoe vipi?
 
Mwaka kesho natimiza umri wa miaka 40 na kama bajungu basemavyo kwamba Life begins at 40 kwa hiyo ninampango wa kuhamia na kwenda kuishi kijijini mbali kabisa nimeishaanza kujenga jumba langu la kifahari palace ndogo yani msoga of my own making hekalu kwa namna nyingine. Sasa huko ninapotarajia kuhamia ni porini sana na inasemekana koboko wapo. Nimeona ni vema kuja kuchukua maarifa kwenu wandugu nikipatwa na dharula kama hiyo ya kung'atwa na nyoka hasa usiku nijiokoe vipi?
Tafuta jiwe la nyoka linazuia kuumwa na nyoka.
 
Nakumbuka kuna shule nilisoma olevel ina nyoka balaaa. Kwenye Joining instruction wameagiza mwanafunzi aje na jiwe la nyoka.

Toka naanza form 1 hadi form 4 nilikuwa natembea na jiwe kiuoni kama hirizi. Huko kwenye viunga ni kukutana na nyoka mwanzo mwisho
 
Nisali sala ipi mkuu? Na vipi kama ni nyoka aina nyingine.
Maombi tu ya kufa salama mkuu ili roho yako ipokelewe na kuwekwa mahala pema peponi na aliye juu,kuhusu nyoka wa aina nyingine ombea tu asiwe na sumu kali kama ya huyo mjomba koboko,manake akikugonga hutoboi ndani ya robo saa tokea akugonge
 
Yanauzwa wapi na Je ni kweli linafanya kazi vizuri au ni uzushi tu stori za kuwaondolea hofu watoto waende shambani wakalime?
Ni kweli kwenye treni ya reli ya kati wauzaji wanayanadi sana yanasaidia na kuumwa na nge pia.
 
Maombi tu ya kufa salama mkuu ili roho yako ipokelewe na kuwekwa mahala pema peponi na aliye juu,kuhusu nyoka wa aina nyingine ombea tu asiwe na sumu kali kama ya huyo mjomba koboko,manake akikugonga hutoboi ndani ya robo saa tokea akugonge
Life begins at 40 na maombi ya kufa salama wapi na wapi mkuu?
 
Kama nyoka wenyewe ni koboko,kinga ni bora kuliko tiba.

Nunua helmet uwe unashinda nayo ukiwa masikani,wale jamaa hupendelea kugonga utosi/kichwa zaidi.

Halafu tafuta na hili buti chini kwa ajili ya wenginao.
 

Attachments

  • PMO_7315+%281%29.JPG
    PMO_7315+%281%29.JPG
    45 KB · Views: 3
Kama nyoka wenyewe ni koboko,kinga ni bora kuliko tiba.

Nunua helmet uwe unashinda nayo ukiwa masikani,wale jamaa hugonga kichwa zaidi.

Halafu tafuta na hili buti chini kwa ajili ya wenginao.
Usijidanganye koboko akikurukia sio lazima awe ametokea juu ya mti. Anaweza kukurukia kwa kutokea chini akapiga mgongo wako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom