Nikimuacha huyu msichana nitakua nimekosea ?

Nyamalapa

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
206
448
Nina girlfriend wangu ambae tumedumu kwa muda wa miezi nane kwenye mahusiano na mpaka leo bado tupo pamoja.Mara nyingi huyu mpenzi wangu kabla hatujakutana kimwili huwa kuna vidonge anatumia ambavyo vinazuia yeye kupata ujauzito.

Kutokana na yeye kutumia vidonge hivi mara nyingi imempelekea yeye kuingia kwenye siku zake kwa siku nyingi zaidi kuliko mzunguko ule wa kawaida ambao unakua kati ya siku tatu hadi tano.

Nimemshauri ashike mimba lakini naona kama hayuko tayari kuzaa kwasasa.Nimeshaanza kumchoka sababu siwezi kuvumilia kusubiri kukatika kwa bleed ambayo inanifanya mimi nishindwe kukutana naye kimwili.

Je nikimuacha nitakua nimefanya kosa kulingana na maelezo hayo hapo juu ?
 
Mkuu
Nadhani kaa nae vizuri mzungumze. Kwanini hataki kushika mimba ...

Au anataka apate mtoto akiwa tayari katika ndoa... Hataki kuzaaa nje ya ndoa..?
Maana anahofia unaweza ukamtelekezaa kwakua sio mke wako kisheria.. Ingawa kukaa na mwanamke siku 90
inatosha kuaminika ninyi ni wachumba. ..

Jaribu kukaa nae na kumuuliza vizuri majibu atakayokujibu utafanya hitimisho lako wewe muhusika uendelee naye au lah..!?
 
Nina girlfriend wangu ambae tumedumu kwa muda wa miezi nane kwenye mahusiano na mpaka leo bado tupo pamoja.Mara nyingi huyu mpenzi wangu kabla hatujakutana kimwili huwa kuna vidonge anatumia ambavyo vinazuia yeye kupata ujauzito.

Kutokana na yeye kutumia vidonge hivi mara nyingi imempelekea yeye kuingia kwenye siku zake kwa siku nyingi zaidi kuliko mzunguko ule wa kawaida ambao unakua kati ya siku tatu hadi tano.

Nimemshauri ashike mimba lakini naona kama hayuko tayari kuzaa kwasasa.Nimeshaanza kumchoka sababu siwezi kuvumilia kusubiri kukatika kwa bleed ambayo inanifanya mimi nishindwe kukutana naye kimwili.

Je nikimuacha nitakua nimefanya kosa kulingana na maelezo hayo hapo juu ?

Kwa breed hii ya wanaume wa sasa hivi? Dada zetu watapata tabu sana!

Wewe nawe umetokea wapi? Tangu lini ukasikia Girlfriend azae? Dadaako akizalishwa utaona sawa?
Acheni kutesa watoto wa watu...
 
Vijana mna nguvu za kutafuta pesa lkn mnaogopa kulea?!

Mimi nataka kuongeza mtt wa pili sasa nasubiri nipate mama wa kueleweka tu
 
Sijaona sababu ya kumuacha , labda kama anashida ya kitabia.
 
Hayo ndio mapenzi yakuteheana, huyo demu wako bado hajawa na uhakika na wewe kwenye uhusiano wenu ndio maana anajihami kwa njia hiyo, ila unaweza kushawishi zaidi aache kutumia vidonge hivyo mara kwa mara,
 
eti hataki kushika mimba......shika wewe basi...unaogopa nini.....???
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom