Nikimpata Ha, sitomwacha...
Nikimpata huyu Mtoto MATATA...
Nikimpata mbona mtaipata...
Nikimpata siji tena kutapa tapa...
Maana MTOTO anavyolipa mie hapa NADATA...
Sijawahi mgusa nawaza ni Mtamu kama KASHATA...
Bado sijamgusa ila hapa nimeshadata...
Chochote tu aseme hata akitaka DATA...
Sijawahi kwenda chini...
Usiulize kwanini...
Siongelei MADINI...
Wala machimbo ya MIGODINI...
Kama hukunipata ujue hiyo CHUMVINI...
Nikimpata, mbona nitanenepa...
Nikimpata, mbona mie nitapeta...
Nikimpata, mbona nitaneemeka...
Nikimpata, kamwe sitasononeka...