Elections 2010 Nikimpa Slaa kura yangu atatawala vipi?

Think before you vote Diana, kupoteza kura maana yake ni nini? kama mwaka 95 ulimpa Mrema si upotevu huo, ni ukomavu
 
Mimi Diana na watanzania wengi tunataka kumpa kura Dr. Slaa oct.2010 lakini najiuliza nikimpa atatawala vipi huku wabunge wengi watatoka CCM? sitaki kuichezea kura yangu na watu wengi wanajiuliza swali hili naomba watu wa Chadema watueleze tukimchagua atavunja Bunge na kuitisha uchaguzi mwingine au atapitisha vipi miswada yake bungeni.Hii mbio ya kuingia ikulu cannot be an end by itself.

Diana

Asante kwa hoja yako.

Slaa akishinda atahakikisha kwamba, kwanza, anapunguza gharama za matumizi ya serikali kwa kuunda mfumo wa utawala wenye wizara chache, ili kuwa na mawaziri wachache, hata kama ni wa CCM. Hii itasababisha kupungua kwa bajeti ya serikali, ambayo imesheheni matumizi yasiyo ya lazima, kama vile ununuzi wa magari ya mawaziri - Toyota LandCruiser VX - ambayo yana gharama kubwa sana, licha ya kwamba kila mwaka wa uchaguzi wananunua magari mapya, ambayo pia yanahitaji mafuta, matengenezo, n.k.

Pia, Slaa nadhani amesema kwamba atahakikisha kwamba kutakua hakuna kitu kinaitwa Mkuu wa Mkoa. Yapo mengi ameyasema, lakini cha msingi ni kwamba, ataweka wazi milango yake, kwamba hata wewe - mwananchi wa kawaida - utakuwa na nafasi yako ya kusema jinsi nchi yako itakavyoendeshwa, kwani, kwa sasa, CCM haijafungua mlango huo wa wananchi kuwasiliana na rais wao moja kwa moja, kumshauri jinsi ya kuendesha nchi.

Slaa anataka Serikali Shirikishi. Kikwete hataki Serikali Shirikishi. Hii ni moja ya tofauti za msingi za kukufanya wewe uendelee na msimamo wako wa kumpa Slaa kura yako mwaka huu!

Asante kwa kumuunga mkono Dk. Slaa!

Tulete mabadiliko YA KWELI!

-> Mwana wa Haki
 
Mimi Diana na watanzania wengi tunataka kumpa kura Dr. Slaa oct.2010 lakini najiuliza nikimpa atatawala vipi huku wabunge wengi watatoka CCM? sitaki kuichezea kura yangu na watu wengi wanajiuliza swali hili naomba watu wa Chadema watueleze tukimchagua atavunja Bunge na kuitisha uchaguzi mwingine au atapitisha vipi miswada yake bungeni.Hii mbio ya kuingia ikulu cannot be an end by itself.

Diana utaaribu kura yako kumpigia Padri Slaa kwa sababu zifuatazo;

- Mkewe Slaa ni CCM damu, hamuamini mumewe, kwa hiyo kakataa kujiunga na Chadema na kura yake anampatia Kikwete

- Slaa kashindwa kusikiliza kero za wananchi waliotaka yeye Padre Slaa aondoe Udni, Ukabila kwenye chama chake

- Uchaguzi ufanyike kwa uhuru badala ya Mtei kumkabidhi uwenye kiti Mkwewe Mbowe

- Chama hakina sera badala yake kinategemea maombi

- NK....
 
Mimi Diana na watanzania wengi tunataka kumpa kura Dr. Slaa oct.2010 lakini najiuliza nikimpa atatawala vipi huku wabunge wengi watatoka CCM? sitaki kuichezea kura yangu na watu wengi wanajiuliza swali hili naomba watu wa Chadema watueleze tukimchagua atavunja Bunge na kuitisha uchaguzi mwingine au atapitisha vipi miswada yake bungeni.Hii mbio ya kuingia ikulu cannot be an end by itself.

Usipate shida ataongoza "swafi" kabisa na watani watapata kujenga vioski vya pombe mpaka ikulu....
Rais: Dr Padre Slaaa
PM : Mbowe
Mambo Ya ndani:Godbless Mrema
Uchumi na Fedha :Mtei (wa kuteuliwa)
Mambo ya nje : Zito
Mambo ya ndani:Joshua Nasare
wengineo....
MATIAS OLE KISAMBO
JOHN SHIBUDA
Kama watashinda ubunge kama hawapati basi wanafamilia watateuliwa kuwakilisha.......
 
Mimi Diana na watanzania wengi tunataka kumpa kura Dr. Slaa oct.2010 lakini najiuliza nikimpa atatawala vipi huku wabunge wengi watatoka CCM? sitaki kuichezea kura yangu na watu wengi wanajiuliza swali hili naomba watu wa Chadema watueleze tukimchagua atavunja Bunge na kuitisha uchaguzi mwingine au atapitisha vipi miswada yake bungeni.Hii mbio ya kuingia ikulu cannot be an end by itself.

Diana Swali lako ni zuri sana naomba nikujibu kama ifuatavyo. first remember that we need changes and changes starts with me and you an everybody else. we have seen alot and we have been deceived alot and now its time to say its over we need changes

now back to your question atatawala vp?

Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa Siasa utakubaliana nami kuwa raisi wa tanzania ana mamlaka makubwa sana katika serikali na bunge pia ni chombo chenye nafasi kubwa pia kwa upande wa kupitisha sheria na miswada. Kwa mantiki iyo kama tukiweza kuwaweka wabunge wengi wa upinzani miswada mingi itapitishwa ambayo yeye Dr. Slaa na jopo lake watakuwa waiandaa bial kupingwa kama ilivyo sasa kwa upande wa ccm. kwani mara nyingi bungeni wanapitisha kwa kuuliza wangapi wanapinga na wangapi wanakubali so kuhusu swala la miswada kupita usiwe na wasi ni wewe tu kuitumia kura yako vizuri. lakni pia kumbuka kuwa sio wabunge wote wa ccm wanaofurahia yanayojiri serikalini ivyo basi kama miswada ikiwa mizuri hawawezi kupinga coz kupinga kwao kunawazuia na wao pia kuwa affected na mswada waliotakiwa kuupitisha.

Dr. Slaa atatawala hivi
  1. Kama tukiweza kuweka wabunge wengi wa upinzani bungeni, serikali ya Dr. Slaa itakuwa na nguvu pia bungeni
  2. Kama Dr. Slaa akiamua kutenganisha Siasa na utendaji kama ilivyo china japan Russia na baadhi nchi nyingi zilizoendelea pia itakuwa ni added advantage
  3. Vilevile kama tukibadili chama tawala pia itakuwa ni jambo la busara zaidi kwani kwa kufanya ivyo tunaongeza wigo wa ushindani wa kuongoza nchi kwani aliyeko madarakani atalazimika kuhakikisha anatekeleza yale yoote aliyo ahidi kama sio kwa uchache ili aweze kushinda tena awamu ijayo, kama ilivyo kwa nchi kama USA and United Kingdom (UK)
  4. Kumbuka Dr. Slaa ni msomi na ana uwezo wa kuchekecha kwa kina kabla ya kufanya maamuzi. I tell u asingekuwa ivyo asingedhubutu kusema, Elimu bure, katiba kurekebishwa ndani ya siku 100 na mengine mengi ambayo umeyasikia

    Kumbuka hata USA ilipata maendeleo makubwa sana baada ya kubali uongozi wa juu and now is the time for Tanzania.

    Mimi mkereketwa wa maendeleo ya Tanzania na sina chama ila ninawapa Priority kubwa sana CHADEMA.

    WE NEED CHANGES AND IT STARTS WITH YOU AND ..................................

    MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE​

Si mpaka CCm wakubali?

Si mpaka uwe na wabunge wa kutosha ndio upitishe miswaada bungeni?

Nimetumwa na nani? nilitegemea wewe mwenye bendera ungejibu swali langu la msingi kwa unyenyekevu kupata kura yangu.

Jinsi unavyoendesha maisha yako na jinsi unavyoona maisha ya Watanzania wenzio ndo swala la msingi....wewe u mtu mzima na unajua kizuri na kibaya...hakuna sababu ya kutaka kunyenyekewa koz ya kura yako.....Kama vp kaa Nayo.....
 
Back
Top Bottom