kerubi afunikaye
JF-Expert Member
- May 20, 2013
- 1,183
- 1,061
Mimi ni mwananchi wa kawaida kabisa.Huku mitaani haya ndio mambo muhimu ambayo sisi wapiga kura tunahoji.
Ni kweli kwamba wengi wetu tumeichoka hii serikali dhalimu,lakini,jambo moja linalotutatiza sana ni pale tunapoona hakuna mtu mwenye uwezo wa kutuongoza kufikia lengo letu la kukomesha utawala huu wa kidhalimu wa watu wachache kuiendesha nchi watakavyo tena kwa wizi wa kura.
Nipo hapa kama mmojawapo wa wapiga kura hao wenye maswali mengi kichwani na kwa mantiki hii,nawauliza viongozi wa vyama vya upinzani,na hasa CHADEMA,CUF na NCCR-MAGEUZI;
(1)Mmejiandaa vipi kulinda kura zenu na kuzuia uchakachuaji wa kura?
Katika uchaguzi wa mwaka 2010 mlilalamika sana matokeo kuchakachuliwa kwenye kuhesabu kura ngazi ya jimbo na NEC.Kwa muktadha wa maelezo yenu wakati ule,inaonekana kwangu kwamba mahala pekee ambapo mawakala wa vyama vyote wanaweza kusimama kidete na kuhakikisha matokeo yanabaki kama yalivyo ni huku chini katika vituo vya kupigia kura.Nawauliza,hivi wazo la matokeo ya uchaguzi ngazi zote hadi ya rais kutangaziwa vituoni limefikia wapi?
Ninachokiona kwa upeo wangu mdogo,ni kwamba CCM inacheza na taratibu za upigaji na kuhesabu kura ili kuiba.Ni lazima kama unataka kupambana nayo,uhakikishe taratibu zinabadilika ili kuleta fair grounds,au na wewe ujipange kutumia udhaifu ule ule wa taratibu zilizopo kushinda.
Binafsi naona uhakika upo katika kubadili taratibu ili ziwe fair,na mojawapo ya mambo ambayo naamini yataibana sana CCM ni matokeo kutangazwa vituoni.
Ni lazima utaratibu uonekane kuwa fair kwa wote,na sio tu kuamini kwamba uko fair.
Hadi sasa,mmeshafanya nini kuhakikisha taratibu ziko fair kwa wote?
Ni nini mengine mnafanya ili kutuonyesha wapiga kura kuwa "You will give CCM a fight of life" especially katika kuzuia wizi?
Nataka kusikia kutoka kwenu kabla sijaenda kupanga mstari,kupigwa na jua kali,na kupiga kura yangu.
Nataka uhakika kura yangu itakuwa ya maana kwa nitakayempigia.
Kulalamika tu hakutoshi,mnafanya nini kuizuia CCM kuiba kura?
Hapa tulipo tuna majeraha ya bunge la katiba,wizi wa mchana kweupe kabisa,and yet bado jamaa wanapeta na rasimu yao mpya?
Sasa mtaendelea kulalamika na kususa,au mnafanyaje kuhakikisha wizi huu unakoma?
(2)Mojawapo ya mambo yanayoniumiza kichwa sana ni hili:
Iwapo mtashinda uchaguzi na kuunda serikali,kwa hali niionavyo,ni lazima mjipange kuhakikisha kwamba CCM kama chama cha upinzani chenye uzoefu wa kutawala nchi,hakitakuwa THREAT kubwa kwenu.
Mbinu za CCM mnazielewa vema,nina wasiwasi,as long as ni kura zetu wananchi zinamtoa huyu na kumuingiza huyu,tusijekuwakabidhi nchi watu ambao hawajajipanga kuongoza nchi hii kwa mapana yote ya neno "kuongoza",ikiwa na maana ya kusimamia wote,wale wanaokupenda,wasiokupenda,wazuri,wabaya,wenye nguvu,wasio na nguvu,na hao CCM,hawa wananchi wanaoikubali,hawa wezi,hawa mafisadi,wote ni sehemu ya jamii itakayokuwa chini yenu.Wengine ni watu muhimu ambao hamtaweza kuwakwepa kushirikiana nao katika serikali yenu,and yet,wana kadi za CCM mifukoni mwao,ninaamini kabisa kwa mwenendo wa mambo niuonavyo nchini,kuiondoa CCM madarakani si lazima sana iwe kifo chake,bali ikabaki na nguvu za kujipanga na kuitikisa serikali iliyoko madarakani.
CCM inalinda maslahi ya kiuchumi ya watu wazito nchini na nje ya nchi,kuiondoa madarakani ni kutia mchanga kitumbua cha wakubwa.Haiwezi kuwa kazi rahisi kuipoteza completely unless serikali yenu pia iwe na mianya ya kuwavutia wakubwa hawa kuitumia na kuachana na CCM,lakini kama mtasimamia haki kwa ustawi wa taifa lote,ni wazi mtatangaza vita na hawa wakubwa,watahakikisha wanatumia uwezo na uzoefu wao kuitikisa serikali yenu,iwe kwa kutumia CCM kama chama cha upinzani,au any other machinery ambayo itakuwa bado available kwao kuitumia effectively.
Hili ni muhimu kwenu kulitambua,kwamba kuna watu so powerful,ambao CCM ni kijiko chao cha kulia chakula.
Mmejipanga vipi kuhakikisha nchi inatawalika kufuatia kukiondoa chama tawala kinacholinda maslahi ya wakubwa madarakani?
Majibu yenu yatatufanya wapiga kura kujua kwamba mmejipanga KUENDELEA KUWA WAPINZANI? au KUSHINDA UCHAGUZI TU? au KUSHINDA UCHAGUZI NA KUONGOZA NCHI?
Halafu tutajua tuitumie vipi haki yetu ya kupiga kura,ikiwa ni pamoja na kuitumia au kutoitumia kabisa.