Nikikumbuka huwa naumia sana

Nikikumbuka huwa naumia sana

Walimu ndo wasio faa oa wana wezana wenyewe kwa wenyewe ndo maana ukichunguza utakuta walimu ndo wafanya kazi wa serikali wanao ongoza kwaku oana sababu yakukaa karbu maofisini bila kazi...uwez mkuta mwalimu wakike ambaye ana bwana mwanaume...!!!
Mitazamo ya watu wasio elimika hii tabu sana,
Mnaongozwa na hisia halafu mnataka kulazimisha hisia zetu kuwa uhalisia,
NOTE: ninapo sema wasio elimika simaanishi elimu ya darasani namaanisha elimu ya uraia.
 
Kweli mkuu.
Usipo tumia uwezo wako wa akili kutafakari ukasubiri ushauri wa humu ndio uufanyie kazi ,jiandae kupotoshwa sana ,kama wewe ni mtu mzima tumia pia uwezo wako wa akili kutafakari mambo maana naona umeshauriwa mambo mengi yasiyo faa humu na unayakubali.
Tafuta namna sahihi ya kupata mpenzi wa maisha achana na uhuni utakao kufanya usiwe na heshima katika jamii , na kujikuta unachelewa hata kimaisha.
 
Habari wana JF

Kila ikifika tarehe kama ya leo tarehe 8/7/ huwa nikikumbuka naumia sana. Mwaka 2012 niliachana na mpenzi wangu Suzie Mapesa, nilikaa muda mfupi sana nikaingia tena katika uhusiano mpya na Mwalimu mmoja wa shule ya msingi ambaye mwanzoni sikumpenda ila siku zilivyozidi kwenda, moyo wangu ulizidi kumpenda.

Nilimpenda sana, ndio kwanza tu alikuwa kaajiriwa binti huyu alikuwa hana kitu, mimi nikawa nikimuhudumia kwa kila kitu, mwaka huo 2013 nilimtafutia chumba nikampangishia, nikamnunulia vitu vya ndani sofa, Tv, kitanda n.k.

Nilimuamini sana nikiamini huyu ndiye mke wangu mtarajiwa kumbe huyu mwanamke utafikiri ana pepo la ngono muda wote yupo busy na ma bwana hakuwa na mmoja, kumbe mimi Inno watu wananiona.

Ni ngumu kufahamu maana watu hushindwa jinsi ya kukueleza siku fahamu mienendo yake. Siku moja nilikuwa katika kijiwe kimoja cha boda boda, kuna boda boda aliniita kufika pale simu ya boda boda ikaita akapokea baada ya kukata yule boda akasema "huyu dada nae kazidi umalaya kila siku nampeleka kwa mabwana tofaut tofauti" wenzie wakamuuliza pale nani huyo, akasema "si yule mwalimu wakataja jina lake, mapigo ya moyo yalienda kasi, roho ikaniuma na furaha ikakata ghafla nikaondoka pale.

Sikuwa na raha kabisa chakula hakiendi mapenzi mabaya, nilipofanya uchunguzi niligundua ni tabia yake na kuna mwalimu mwenzie anatoka nae pale pale shuleni.

Nikamdanganya nasafiri na nitarudi baada ya wiki mbili, usiku wa tarehe 8.7.2013 nilienda kwake bila taarifa nikakuta njemba linakula mzigo nikaona nikigonga mimi hatofungua nikaita katoto ka pale jirani kakagonga takribani dk 20 hivi ndio akaja kufungua mlango.

Nikaingia ndani akashituka, nilipitiliza mpaka chumbani nikakuta njema imekaa kwenye kitanda ina boxer tu roho iliniuma sikufanya fujo nikaondoka zangu.

Nisingekuwa na uvumilivu na subira ningechukua maamuzi magumu pengine leo hii ningekua Jela.
if u want 2b happy in u'r life, stay away from luv
 
Back
Top Bottom