Nikikumbuka huwa nacheka sana

Nikikumbuka huwa nacheka sana

Wifi huyu jamaa nimempenda ana mapenzi mazito na huyo mwanamke, pamoja na changamoto ya uzazi lakini bado anakomaa naye ila ana kauoga flani..!!
Achukue jiko hilo wote wanapendana hao 😊
Anajichekesha tu 😂😂😂
 
Sina kauoga shemeji, kwa sasa kuna dawa anakunywa kidonge kimoja 10,000 ila navichukua sehemu wananiuzia 7000 maana ni daily dozi. Imani yangu ipo kwenye miziz nikipata mtaalamu tu najua atakaa sawa. Kuna babu yangu tulimpeleka hospital wakasema hali yake haitibiki tumlee tu mpaka afe lakini sangoma alicheza nae mpaka sasa yupo poa kiasi lakini sio kama alipokuwa anatumia dawa za hospital alikatisha matumaini. so nina imani hakuna kinachoshindikana. Uzuri alikuwa mkweli hakutaka kunijaza ndio maana nahangaika nae, mabinti wengine angeficha na akawa analalamika kwa nini hashiki mimba kumbe anajua chanzo. Kwa sasa ana 32 yrs and i am not abandoning her no matter what, japo kwa sasa ni kama rafiki ila kwa kuwa maisha hayatabiriki you never know what is in the store for you.
Muoane tu
Mungu Huwa hashindwi na jambo mtapata watoto
 
Niliwahi kuwa na mpenzi mmoja, kwa maelezo yake akawa anasema ana shida ya uzazi hawezi kushika mimba, basi nikawa natoka nae cha ajabu kuna siku anakwambia yuko siku za hatari so tusifanye.

Basi akawa anasema anatamani sana mtoto na akawa ananiambia kama sijali kuhusu shida yake nimuoe nimtibie tuzae, nilikuwa site kwa miezi kama 7 mkoa huo akawa anataka nikiondoka nisepe nae.

Basi bwana nikafatilia hospital ikaonekana shida yake ni kubwa sana na itachukua muda kuwa tayari kuzaa, hapo alikuwa na 28yrs. Watu fulani wakanielekeza kwa mtaalamu wa tiba asili na wakasema anaijua dawa na alishasaidia case kama hiyo. Issue ikawa kupata mawasiliano yake.

Wakati tunamtafuta mie mda wangu ukaisha ikabidi nisepe, ajabu baada ya kama wiki 3 yule dada akanipigia anasema ana mimba. Akataka aje kwangu nikakmwambia subiri nije kwenu tumalize utaratibu nikuoe kabisa, yeye akawa hataki niende kwao anataka aje kwangu kwanza.

Mimi nikaona jau kukaa na mtoto wa mtu bila u rasmi nikamwambia asubiri ntamjuza aje lini. Yule dada akanikatia mawasiliano kila nikimtafuta simpati. Kaja kunipigia 2 yrs later anasema amenimiss, nikamwambia its okey, utakuja na mtoto? Akauliza mtoto gani, nikamwambia si ulizaa, akajibu we unajifanya hujui tatizo langu, ningezaaje sasa na wewe ndio ulikuwa unanitafutia tiba ukaondoka kabla hatujampata muhusika.

Sikutaka kumkumbusha kuhusu aliponiambia ana mimba anataka aje kuishi kwangu, lakini nimeona nimuache tu.

Kwa sasa nipo naye kama rafiki na sija do nae, Weekend nilimtoa out nikamkumbusha matukio yake basi kachekaaaa, mi mwenyewe kila akipiga simu nacheeeekaaaaa.

KIUKWELI NIKIKUMBUKA NACHEKA SANA.
Achana nae tafuta mwingine
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom